Wallet
Mkuu ni vigumu sana ukiwa kundi jingine kuweza kuona ya upande wa pili na yamkiniki wewe hukutoka kt kundi la walalahoi hivyo huwezi kutambua hawa Pnya road wametokana na nini? Ufahamu tu kwamba hawa vijana ni kati ya umri wa miaka 16 hadi 20 ambao wanatakiwa kuwa shule kama ulivyodai lakini wameshindwa vipi kuwa shuleni? sidhani kama umefanya utafiti huo kwanza!
Na hata tukichukulia juu juu tu ya kwamba shule zetu ni za kulipia na zaidi ya hapo hawa ni failure wa mitihani ama mfumo wa Elimu nchini ambao umewaweka katika nafasi hiyo. Hata wale walioko vitani leo kule Syria na wameshika bunduki sio kwamba wao ni majambazi na terrorist isipokuwa kuwepo kwa vita kumewalazimu kuwa wauaji aidha baada ya kushindwa kukimbia nchi yao ama ile ari ya kuitaka amani.
Swala la class struggle nchini sii la kulifanyia mzaha hata kidogo, ni jinamizi linalokua kwa haraka sana na litakuja kutuangamiza sote maana kesho haitakuwa Panya road tena bali jirani yako ambaye kashindwa kujikimu mahitaji yake wakati wewe jirani yake unatanua. na hii imeanza pia kujitokeza maana kwa kila mwenye nacho leo hii hutafuta makazi mapya sehemu ambazo ataipata amani, hivyo amani inaaza kupotea baadhi ya sehemu za makazi yetu hapa hapa mjini.
haya makuzi ya Dar kuwa na maghorofa ni makuzi ya mwili tu, kama vile wewe huwezi kuwa sawa na ulivyokuwa miaka 12, leo umerefuka una ndevu, sharubu, unavaa suruali badala ya kaptula haya sio maendeleo bali makuzi ya mwili na vitu vinavyoendana na makuzi hayo kwa sababu afya yako bado inaweza kuwa dhoofu zaidi, maisha yako ya taabu zaidi ya utoto. Hata ukienda New York leo utaona mabadiliko makubwa zaidi ktk majengo, New York ya mwaka 1990 sio hii ya leo! wala maendeleo sio kuwa na Kentacky fried Chicken au maduka ya bidhaa kutoka nje, sisi ni mateja tu ktk soko la ubepari! Maendeleo ya nchi yetu, ukitazama miundombinu leo ni mibovu kuliko wakati wowote, mirefeji, barabara, reli, ukulima na hata vyanzo vya ajira. Tuna watu wengi wasokuwa na kazi leo kuliko wakati wowote ule na hii ndio alama kubwa ya maendeleo. Panya road ni sehemu kubwa ya kizazi cha wazazi wasiokuwa na ajira na hivyo kilema hicho kinaendelea chini na kuwa mnyororo wa walalahoi ambao kesho na kesho kutwa ndio watakuwa maadui zako!
Panya road ni tahadhali kubwa ya jamii tunayoijenga leo!