masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,410
- 14,119
- Thread starter
- #21
Hili tatizo la Panya Road liko juu ya uwezo wa Polisi peke yao kulitatua.Hata hapa kwangu napoishi, muda mfupi uliopita tulikuwa tunazungumzia swala hili na mwanamama mmoja na nikamueleza chanzo kimojawapo cha matukio kama haya ni watu kukosa ajira na kukata tama.
Bahati mbaya sana,kama ilivyo kwa wana-CCM wengi,mama huyu alipinga hoja yangu na kutoa sababu zake kama vijana kuvuta bangi n.k.
Huyu mama angekuwa na akili angejiuiliza kwanza ni kwanini vijana hawa wavute bangi n.k.
Najua kuna wengine hata akiwa na maisha mazuri kuvuta bangi na mambo ya aina hiyo ndio hulka yake.Lakini je,wote hawa kwa makumi au mamia wanafanya vitendo kama hivi kutokana na hulka zao tu?
Polisi kama wana akili,vijana waliowakamata wawahoji kistaarabu ili wawape sababu za wao kufanya walioyafanya na taarifa wazipeleke serikalini kwa utatuzi kama tunataka haya yasijirudie tena.Tofauti na hapo ni kujidanganya tu.
In short,civil disobedience in our country is around the corner.
Kwanza hakuna polisi wa kutosha kuwadhibiti vijana hawa kama wakiamua kuingia barabarani na kuanza kupora kama ilivyoonekana majuzi.
Hili ni swala la kulitatua kimipango zaidi na kimkakati ili kwa muda mrefu sana ujao vijana hawa waajirike au wajiajiri ili nguvu yao itumike kwa manufaa kwao na kwa nchi.