The inevitable class struggle between the haves and the have nots...!

The inevitable class struggle between the haves and the have nots...!

Mkuu nashukuri kwa kutumia muda wako kunipa feedback.

Mimi naamini kuwa lengo la Nyerere lilikuwa zuri sana la kujiendeleza lakini siamini kuwa siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea ingewatoa Watanzania katika umasikini na kuwaletea maendeleo kwa wote. Hapa ndio kuna upingamizi.

Pili, vita vya kagera vilianza miaka kumi baada ya yeye kuishika nchi. Kama Ujamaa ungekuwa na maendeleo, yangejionyesha.

Tatu, kumfuata Nyerere ni kumfuata Dikteta. Siwezi kufuata sera za Kiongozi ambaye hajanipa haki ya kumchagua. Pia, Elimu chini yake haikuwa elimu huru. Hata wananchi kama wamesoma bure, haki ya kufikiri ilikuwa hamna. Maoni ninayoyaandika leo hapa yangenipeleka kifungoni wakati wa Ujamaa.

Nne, sikubaliani kuwa mashirika ya umma ya Ujamaa yana uwezo wa kuzalisha kwa faida zaidi kuliko viwanda binafsi. Siasa ilikuwa mbele kuliko faida. Japokuwa lengo la Nyerere lilikuwa kuleta usawa, binadamu hakuzaliwa na lengo hilo. Hawezi kumshibisha mwenzake kabla yake.

Viwanda vilifilisika sio kutokana na viongozi wabovu ila kutokana na sera za Kijamaa za kutoheshimu faida. Pia, uchumi wa Tanzania ulikuwa mdogo. Hata leo, japokuwa uchumi unakua, tunazalisha $40 bilioni tu, wakati Nigeria pamoja na historia yake ya vita vya Biafra na kuendeshwa kijeshi miaka mingi, wanazalisha $500 bilioni.

Kwa kuwa wananchi walibanwa kuzalisha kibepari, kulikuwa hamba mzunguko wa fedha wa kuzalisha mali zaidi na kuipatia serikali mapato.

Tano, China ni Mjamaa kwa jina tu na waliporuhusiwa kujenga viwanda binafsi na Deng Xioping ( Getting rich is Glorious alisema) walijenga kwa kasi mno. Pia ukumbuke uwezo wao wa kifedha kama raia ni mkubwa kuliko sisi. Wao wana ndugu wengi nchi za kitajiri kukopa kufanya biashara na wamejisomesha vya kutosha na kuona faida ya sera za kibepari kwa ndugu zao Hong Kong, Macau , Singapore na Malaysia.

Sisi uchumi wetu, uwezo wa kifedha wa wananchi wetu na elimu yetu haikuwa sawa. Itakuwa kama unafananisha tufaha na chungwa. Biashara zao hata za umma zinaendeshwa kibepari. Wanafunzi wa Kichina ndio wanafunzu wa kigeni namba Moja vyuoni Marekani.

Naungana na wewe kuwa Watanzania ni wavivu wa kazi na fikra. Tunapenda kulalamika tu. Tunataka bure, spoon fed. Leo Mtanzania ana haki ya kufanya biashara yoyote lakini haifanyi mpaka aje mgeni. Leo ana uwezo wa kumchagua Kiongozi, lakini aidha hapigi kura au anachagua viongozi fisadi kwa kuwa amehongwa pesa na doti moja ya kanga. Wenzetu wanafanya maandamo na kuwatimua viongozi wabovu.

Nawakilisha.
Mkuu kuna fundamental mistakes katika hoja yako, Siasa ya Ujamaa na zkujitegemea ni msingi mkubwa wa mtu na nchi kujifikiria yeye kwanza katika kujiletea maendeleo.
Tatizo kubwa ni kufikiri kwa mlengo wa kijamaa kwa maana ya communalism na kugawana umasikini.
Kujitegemea kupana zaidi ni kufikiria kutumia rasilmali zetu kwanza kabla ya kufikiria misaada toka nje.

Pili, hapo you are dead wrong.
Mwalimu alishika nchi 1961, wakati vita ya kagera ilianza November 1978, miaka 17 baada ya Mwalimu kuwa Rais wa nchi hii.

Tatu, nyie mnaohadithiwa tu juu ya siasa za Mwalimu ni lazima mlikuwa na wazazi ambao walikuwa katika receiving end kutokana na ku underperform au kuhitilafiana na Mwalimu.
Kielimu mimi mwenyewe nimefaidika na sera za Mwalimu na nimepata the BEST education ever, FREE.
Katika shule zilizojendgwa baada ya uhuru, nimesoma hapo na kufundishwa vizuri, tena wa nchi za dunia ya kwanza.
Kwa hiyo postulation yako kuwa elimu haikuwa huru is dead wrong.
Chuo Kikuu cha Dsm wakati huo kilikuwa na uhuru wa kifikra pengine kuliko wakati mwingine wowote tangu kianzishwe.
Na wanafunzi wa UDSM walikuwa na uwezo wa ku influence policies za nchi hii.

Mengine uliyo andika siba uhakika kama una experince ya kutosha ya kuperform an opinion
Ni mambo ambayo naweza kusema ni hearsay, mambo uliyohadithiwa for all the wrong reasons.

Bado nasisitiza kuwa we can do better, ili kutatua matatizo yetu ya umasikini.
Mwalimu did put us on the right footing.
 
Mkandara kuna maeneo tunakwemda sawa ila yapo pia tunapishana. tatizo wala si ajira bali miundombini. na hapa sizungumzii barabara. social and physical infrastructure. rural area zimetelekezwa. hukumbukwa kipindi cha uchaguzi tu na walio madarakani. pangekuwa na mikakati ya dhati ya serikali wala pasingwkuwa na hii bright light theory. vijana wangebaki huko wakijilinia na shughuli zingine. dar imefurika. so how do we flex capacity while demand is high and dar is saturated. dar imejaa na ndio maana unadhani tatizo ni ajira. dar almost fursa zote zimeshawahiwa. zilizobakia ndio hizo unsesired kama uhalifu.

ukisema utokecurudi mikoani huko nako miundombinu ya kuzifikia fursa imedumazwa, therefore dar pamoto na mkoani pamoto, hasa kwa kijana wa type ya panya road.

na nikuhakikishie kuwa nchi hii haitakaa itikiswe na panya road type. nchi hii itaangushwa na wanasiasa tusipokuwa makini. hao wa somalia si vijana bali tatizo lilianzia kwenye ukabila na vita vya koo (clan).
uganda nako ukabila. kwa hiyo mfumo wetu na mipango yetu isiyo na uwiano ndio shida!
 
Last edited by a moderator:
PANYA ROAD NI JANGA LA MIJI MIKUBWA,
watumishi wa umma wengi mishahara ni 30% ya gharama za maisha,70%iliyobaki ni mishemishe na posho na mikopo,
mtaani watoto wa hawa watumishi wa umma,wanaishi vizuri kuliko watoto wa wasio watumishi wa umma,
Ajira za kujiajiri zimejaa uongo na wizi mdogomdogo.
Polisi inajiendesha yenyewe (vitendea kazi duni sana),inabidi Askari wawe wabunifu ili watimize Ajira zao,
MSHITAKI NA MSHITAKIWA INABIDI ACHANGIE HUDUMA ZA POLISI.
Jamii ya maskini wengi wanashindwa kufanya vurugu ni kwa kuwa na imani za kidini,ila sasa imefikia mahali hata viongozi wa kidini wanatuhumiwa na ufisadi (e.g Escrow), hivyo basi jamii maskini hazina imani na viongozi wao wa kidini, kumbuka viongozi wa kisiasa hawana imani nao tena.
Mtazamo wangu, Panya Road ni kiashiria cha machafuko ya wenye nacho na wasio nacho,ikiwemo wengi waliomo humu JF ni Wenye nacho( unaweza kuwa na computer,internet etc)
Tujipange kuishurutisha serikali sikivu ya CCM,ili 2015 Uwe mwaka wa kuleta Tumaini Jipya la Wananchi.
 
Mkuu kuna fundamental mistakes katika hoja yako, Siasa ya Ujamaa na zkujitegemea ni msingi mkubwa wa mtu na nchi kujifikiria yeye kwanza katika kujiletea maendeleo.
Tatizo kubwa ni kufikiri kwa mlengo wa kijamaa kwa maana ya communalism na kugawana umasikini.
Kujitegemea kupana zaidi ni kufikiria kutumia rasilmali zetu kwanza kabla ya kufikiria misaada toka nje.

Pili, hapo you are dead wrong.
Mwalimu alishika nchi 1961, wakati vita ya kagera ilianza November 1978, miaka 17 baada ya Mwalimu kuwa Rais wa nchi hii.

Tatu, nyie mnaohadithiwa tu juu ya siasa za Mwalimu ni lazima mlikuwa na wazazi ambao walikuwa katika receiving end kutokana na ku underperform au kuhitilafiana na Mwalimu.
Kielimu mimi mwenyewe nimefaidika na sera za Mwalimu na nimepata the BEST education ever, FREE.
Katika shule zilizojendgwa baada ya uhuru, nimesoma hapo na kufundishwa vizuri, tena wa nchi za dunia ya kwanza.
Kwa hiyo postulation yako kuwa elimu haikuwa huru is dead wrong.
Chuo Kikuu cha Dsm wakati huo kilikuwa na uhuru wa kifikra pengine kuliko wakati mwingine wowote tangu kianzishwe.
Na wanafunzi wa UDSM walikuwa na uwezo wa ku influence policies za nchi hii.

Mengine uliyo andika siba uhakika kama una experince ya kutosha ya kuperform an opinion
Ni mambo ambayo naweza kusema ni hearsay, mambo uliyohadithiwa for all the wrong reasons.

Bado nasisitiza kuwa we can do better, ili kutatua matatizo yetu ya umasikini.
Mwalimu did put us on the right footing.

Mkuu,

It is better to agree to disagree here.

You don't know me so you can't judge me or my parents based on our lives under Nyerere. Sijahadithiwa chochote, nimekaa mstari kama wewe kununua resheni ya chakula.

You are free to believe what you want but we had no freedom of thought under Nyerere. All the educational institutions were teaching his ideologies and socialism including UDSM. It is called indoctrination.

Again, what did your free education achieve? Nothing. Why? You had no right to think to improve production, innovate etc. Only follow Nyerere and achieve Utopia!

You have made my point about Vita vya Kagera. 17 years and we lived in extreme poverty by 1978. So to blame the war is silly when he had 17 years to prove that Ujamaa will bring us wealth, development and equality.

If you don't have experience to make educated judgement, you can at least read. You are free to read and practice freely now.

There is no other way to get development other than through free market. This is even truer to poor nations like Tanzania. Ujamaa failed and it failed miserably. Do not mix ujamaa ideology with practicalities of life. We are humans, not robots.

As an educated man, how can you sit here and defend his dictatorship? It is beyond my comprehension really.

You can justify nationalization of innocent people's property and wealth under Ujamaa and lack of political and human rights but arguing for the equal rights for common people TODAY! What irony!
 
Pia Mkuu, nionyeshe wapi nimekupa hadithi sio ukweli mtupu. Heresay ni uwongo, haina uthibitisho, mambo ya kimbeambea. Uwongo upi niliouandika?

Nimeandika:

1. Nyerere alikuwa Dikteta. Unahitaji uthibitisho kipi?

2. Tanzania ya Nyerere tulikuwa hatuna haki ya kisiasa wala ya kimawazo. Unapinga?

3. Uchumi wa China na Tanzania kamwe haukuwa sawa miaka ya Ujamaa. Nani alikuwa mwombaji? Nyerere au Mao.

4. Kama ulipata elimu huru na ya bure Tanzania, kwa nini kulikuwa hamna somo la kibepari UDSM? Marekani 1970, unaweza kusoma somo la Ujamaa darasani, wewe unaweza kusoma sera za ubepari darasani 1970? Kwa nini unyimwe uhuru wa kusoma biashara za kibepari Halafu unasema hujakabwa kimawazo darasani? Au hii pia ni heresay kwa sababu inaenda kinyume na fikra zako za Ujamaa?

5. Deng Xioping hakusema " getting rich is glorious"? Au huu ni uwongo pia?
 
Mkuu,

It is better to agree to disagree here.

You don't know me so you can't judge me or my parents based on our lives under Nyerere. Sijahadithiwa chochote, nimekaa mstari kama wewe kununua resheni ya chakula.

You are free to believe what you want but we had no freedom of thought under Nyerere. All the educational institutions were teaching his ideologies and socialism including UDSM. It is called indoctrination.

Again, what did your free education achieve? Nothing. Why? You had no right to think to improve production, innovate etc. Only follow Nyerere and achieve Utopia!

You have made my point about Vita vya Kagera. 17 years and we lived in extreme poverty by 1978. So to blame the war is silly when he had 17 years to prove that Ujamaa will bring us wealth, development and equality.

If you don't have experience to make educated judgement, you can at least read. You are free to read and practice freely now.

There is no other way to get development other than through free market. This is even truer to poor nations like Tanzania. Ujamaa failed and it failed miserably. Do not mix ujamaa ideology with practicalities of life. We are humans, not robots.

As an educated man, how can you sit here and defend his dictatorship? It is beyond my comprehension really.

You can justify nationalization of innocent people's property and wealth under Ujamaa and lack of political and human rights but arguing for the equal rights for common people TODAY! What irony!
For those like you who have met Mwalimu in text books have the right to be confused.
 
For those like you who have met Mwalimu in text books have the right to be confused.

Thats probably the best answer to a clown who does not have the slighest ideas as to where he is from and where he is going!
Halafu watu wanashangaa kammma wako feri , Panya Road wanatoka wapi!!!!!
 
Mkuu masopakyindi , hii ndo topic haswa za kisiasa, lakini hapa hutapata wachangiaji.
Members wengi humu wana tu digirii twa kuombea kazi, siyo za thinkers.
Ungeandika mkuu fulani wa kisiasa kaja.mba au kabaka comments zitajaa kama watu wanafukuzwa!

Ameeleza kirahisi nadhani kila mtu ataelewa.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kipindi aliandika Padre Privatus Karugendo kuhusu masihala ya yanayoendelea kukabili ongezeko la watoto wa mitaani (Alisema wanaitwa wamitaani utafikiri wamezaliwa na mitaa wakati kila mmoja kazaliwa na binadamu), alikuwa akielezea tahadhari inatakiwa kuchuliwa kwa busara kuhusu kundi kubwa la vijana sehemu za mijini wasio na sehemu maalumu ya kuishi na kujiapatiakipato. Alieleza kwamba, watoto wengi wanajipanga barabarani wakiomba wapita njia kwenye foleni za magari na watembea kwa miguu, akaendelea kusema, wanaodiriki kuomba ni wenye umri mdogo, lakini umri wa hao watoto unapoongezeka hawawawezi kuthubutu tena kuomba, wanajiunga na kutengeneza kundi ambalo linaweza kutumbia hata mbinu ya kuvania watu na kunyang'anya kwa sababu mtu mzima hata akiomba kama wanavyoomba watoto wadogo hawezi kupewa kitu, sana sana ataishia kutukanwa na kuambiwa hataki kufanya kazi. Makundi haya ya watoto wa mtaani ni vema yakatazamwa na kueleweka vizuri kwamba, huenda idadi kubwa hawakupata hata muda kwa kwenda shule, hivyo hata uelewa wa masuala mbalimbali ya kijamii ni mdogo zaidi ya tunavyofikiri. Makundi haya ni rahisi kushawishiwa kwa sababu hitaji lao la karibu ni kupata mlo.
Ni vema mamlaka zikalitazama kundi hili ambalo halina kazi zinazoelewaka na limejaa mjini.

Vikundi kama Panya Road na Watoto wa mbwa mwitu hayawezi kufutika kimya kimya katika jamii maana ni vigumu kuwabeba na kuwapeleka vijijini kwa sababu inaonesha ni idadi kubwa ya watu wanaunda kundi hili kama ambayo saka saka ya Kova ilivyoweza kukamata zaidi ya watu 500, si jajua kama operation hii iligusa maeneo yote ya jiji la Dar es salaam. Makundi haya yanaona wenye navyo jinsi wanavyostarehe mjini wakila vinono na jinsi wanavyowawezesha watoto wao kwa vitu vizuri hali inayowaongezea hasiri wasionacho mpaka kudiriki kuwachukia walionacho, kwa kuwa hakuna anayepiga kelele kulaani pengo la walio nacho na wasionacho.

Safari bado ndefu: Mtikisiko wa Makundi ya Watoto wa Mbwa mwitu na Panya Road tuyatumie kama changamoto ya kupata ufumbuzi, kwa kuanza na kufanya mahojiabo ya kina na waliokamatwa kwenye Operesheni kamata Panya Road,
 
Thanks brother, you have explained it in a simple and straightfoward manner.
Kuna watu wanafikiri Panya Road is a criminal occurence, hawajui kuwa hilo ni tatizo la kijamii.
 
You are free to believe what you want but we had no freedom of thought under Nyerere. All the educational institutions were teaching his ideologies and socialism including UDSM. It is called indoctrination.

Again, what did your free education achieve? Nothing. Why? You had no right to think to improve production, innovate etc. Only follow Nyerere and achieve Utopia!
Who goes to school and learn about socialism if you know anything about economics.

In economics a choice of production derive as a result of answering how best to produce, if you learn the means of production you can shift easily to another mode based on government preference.

Sasa sijui Nyerere anahusika vipi na sera za sasa.
 
Kwa tuliopita Development Studies wakati wa kuchukua digree zetu za kwanza, kwa sasa tunaingia kipindi cha ubepari ambapo kuna a direct class struggle kati ya the haves and the have nots.

Kwa miaka sasa tumeona ubepari mzito mzito ukiingia, na sera nzuri nzuri za kuremba uwekezaji, ili mabepari waweze kufaidika maradufu na fedha zao nchini kwetu.
Na kweli uwekezaji umeingia kwa kasi, na tunaambiwa hata uchumi unakua kwa kasi ya 7%.
Kitu tunachokiona kwa macho ni majengo marefu yanayokua kama uyoga hasa jijini Dsm na miji mingine kama Mwanza.

Hata hivyo kwa upande wa pili, sera za kuwaendeleza wananchi (social participation policies) zimekuwa haziendani na kukua huko kwa uchumi.
Wananchi wa kawaida wanazidi kuachwa nyuma kimapato na haionekani kama wanafaidika sana na maendeleo wanayoyaona.

Kwa sasa ni dhahiri, ruling class imeji align na the bourgeoise(the wealthy class), wakati sera za kuzatiti kundi la wenyeji na wafanyakazi wa hali ya chini(proletariat) zinazidi kutopata kipaumbele kinachohitajika.

Dalili za kupinga mgawanyiko huu kati ya the haves na the have nots, ndo tunapata vijana walio katika extreme end ya the have nots: Panya Road.

Katika hii struggle nguvu ya polisi haitasaidia sana mpaka hapo the have nots nao watakaposhirikishwa katika kufaidika na maendeleo ya jamii.
Mahsusi hili ndio bomu lenyewe ambalo limekuwa likiongekewa kwa miaka sasa kutokana na kutoshughulikiwa na matatizo ya kushirikisha kwa makini matatizo ya wanyonge , hususan vijana katika mipango ya maendeleo.

Mimi sioni mwisho mwema katika hii struggle maana hata wakiwepo kina Kova kumi, vijana wale wasio na kazi wako pake pale.
Suluhisho ni kwa kuanzia tu, ipatikane miradi mikubwa ya maendeleo sehemu zote nchini, itakayo buniwa mahsusi ku ajiri hii idle resource kwa maana ya vijana, ili waweze kuchangia uchumi na vile vile wajipatie kazi, hivyo kutoka katika vikundi vya kihalifu kama Panya Road.

Mkuu Masopakyindi, haihitaji kusoma DS au falsafa za akina Carl Marx kujua athari za ubepari, au uongozi usioangalia mstakabali wa watu wake. Ni "Common sense tu" Ni suala la Mipango tu kama familia inaweza kujiwekea Mipango kwa ajili ya ustawi wake, nchi inashindwa vipi kwa ajili ya watu wake? Tunafanya sensa kwa ajili gani? Tunasomesha watu wetu ili baadaye wafanye nini? Tunao vijana takribani 70% ya wanaograduate wako mtaani hawana ajira (walisoma ili waajiriwe). Watoto wanaoitwa wa mtaani wanaishia wapi? Vijana wengine ambao hawakubahatika kupata elimu wana matumaini gani ya maisha? Haya ndo "Mabomu " tunasubiri yalipuke ndo tuseme kuna mtu nyuma yao?
 
Unachosema ni kweli kabisa mkuu!!
Lakini nani asiyejua kuwa pamaoja na kujua huko, sasa we have a social problem, the Panya Road problem.
Its easy to mis understand and think that this is a criminal problem.
Elimu ile ya social studies ilikuwa muhimu sana hasa kwa viongozi wetu wasije jisahau, na kuji align na the bourgeoise, the haves.
Sababu za the ruling class kuji align na hao bourgeoise ziko very clear, and its not in the interest of the proletariats(walalahoi).

Hivyo basi, ni muhimu sasa kujitathmini katika policies zetu ili kulitatua hili tatizo la Panya Road Phenomenon, ili lisije kuwa kweli bomu ambalo tayari limeanza kulipuka.
 
Nina uhakika kama tungekuwa na viongozi waadilifu,wazalendo na wanaomuogopa Mungu,UJAMAA na KUJITEGEMEA ungeweza kutufikisha mbali sana.

Leo hata wakulima wakitaka kununua yaliyokuwa MASHAMBA ya taasisi za umma wananyimwa kwa kisingizio cha UWEKEZAJI.Hivi hawa WAWEKEZAJI ni wajomba zetu?Hivi Watanzania wanaotaka kununua mashamba haya kwa nini wasiuziwe na kupewa mashamba hayo?

Leo tunaviwanda vilivyouzwa kwa wawekezaji vimekuwa magofu ya kupanga wavuta bangi na majambazi.

Kijana wa kawaida akitaka eneo la kulima hawezi ku-afford hana hata kianzio,tutamwitaje kijana huyu mvivu?Kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya vijijini ndiko kunakoleta vijana wengi kuhamia mijini.

Viongozi wetu wakiacha choyo na ubinafsi twaweza kuanza upya kuangalia wapi tulianguka na kujisahihisha,vinginevyo tusiwalaumu vijana waliojiundia kundi la ujambazi,tujilaumu ni namna gani tumeweza kuisaidia jamii maskini kuondokana na umaskini walionao.Wala tusiwalaumu wazazi maana hata sisi pia ni wazazi wao.
 
Mkuu kama unaamini kabisa kuwa Ubepari haukwepeki (sijui sababu), basi kuwa na hakika kabisa kuwa Uneven Distribution of Resources & wealth HAKUKWEPEKI
Hujapatia sana chanzo na hitimisho lako. Kwanza, ubepari haukwepeki kabisa bali unatakiwa kusimamiwa kwa vigezo vilivyo wazi na kukubalika kwa wote. Vigezo hivyo ni pamoja na vile vinavyotoa fursa na haki sawa kwa wote huku maadili na sheria vikisimamiwa kwa uwazi na bila kuyumbishwa na chochote kile (blind justice). Aidha, uchumi wa kibepari unaoendeshwa inavyostahili na kwa uwazi, huwatupi kabisa wasiojiweza; hujitahidi kuimarisha huduma za kijamii kama vile za afya na elimu ya msingi kiasi cha kuweza kuwafikia wote. Cha muhimu zaidi, wananchi wakiona mambo yanaeleweka; fursa zipo na zinatolewa kwa haki; matumizi ya rasilimali yako wazi na jitihada za kuhakikisha kuwa zinachangia vilivyo katika ustawi wao zinafanyika - hawapati taabu na tofauti zilizoko kati ya vipato na tofauti za madaraja ya utajiri binafsi.
'Uchumi wa Kibepari unaoendeshwa INAVYOSTAHILI' ni dhana MFU kwetu, kamwe haiwezi kuishi si Tz peke yake bali Afrika kwa ujumla wake! Nina maana kuwa, hivyo vigezo vya ubepari sahihi havisawili Mazingira na Nyakati zetu halisi!
Anaita sasa!
 
Back
Top Bottom