masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,410
- 14,119
- Thread starter
- #41
Very true !!Mkuu Masopakyindi sijakataa jumla unachosema. Aidha, kwa kukosoa uongozi wa nchi naweza kuonekana kirahisi nimeingiza siasa za vyama; kama vile nakishambulia chama kilichoko madarakani. Sivyo kabisa. Wasiwasi wangu mkubwa sana kuhusu Tanzania leo hii ni ule utamaduni tulioujenga kwa miaka mingi wa kuchukulia madaraka kama njia ya kuinua uchumi binafsi wa mtu badala ya taifa. Sidhani kama unahitaji kuelezwa kuwa hata biashara kubwa Tanzania zinahusishwa na ukaribu na walioko madarakani. Kwamba usipokuwa na madaraka au kuwa karibu na wenye nayo si rahisi ukafika mbali kibiashara (nikiweka utani: utaishia kunadi juisi na matunda - tena mitaani!).
Mtazamo wangu wa dhati kabisa, si kwa chama kilichoko madarakani tu, hata vikija vingine naona uwezekano wa kujikuta tukiendelea na mfumo wa "kleptocracy" ni mkubwa sana. Leo hii nikiwatizama Watanzania wengi wanaowania nafasi za uongozi (wa vyama vyote) naona wanasukumwa zaidi na mtazamo wa "sasa ni zamu yetu kula". Wapo wanaonishawishi kuwa wanajitoa kwa taifa - kama alivyojanya JKN (pamoja na mapungufu yake ya kimkakati). Lakini ni wachache sana. Na naheshimu sana uwezo mkubwa wa binadamu kulaghai kikamilifu (ultimate deception capacity).
Kwa upande wetu kama jamii, SIJUI kama itakuwa rahisi kufuta mtazamo uliojengeka sana wa kuwaona viongozi kama miungu (wakiwa juu ya sheria na taratibu). Kunahitajika "mapinduzi" makubwa hasa kurejesha uwajibikaji kwa viongozi nchini ukichukulia kwamba kiwango cha unafiki na ubinafsi katika jamii ni kikubwa sana. Atakayefanikiwa kuchukua uongozi wa nchi (chama chochote) akiwa na ajenda ya dhati ya aina hiyo basi naona huyo awe tayari kupoteza umaarufu mapema sana, awe tayari kupoteza marafiki na hata ndugu na kutawala kipindi kimoja tu. Zaidi ya hapo, awe tayari kuwa mtu mpweke sana. Naomba sana niwe NIMEKOSEA katika mtazamo wa aina hii. I really wish to be completely wrong!
Kwa vyovyote vile, nisingependa sana kuchukulia mpambano unaosababishwa na tofauti za kiuchumi zinazotokana na mfumo wa wizi/rushwa katika tabaka la watawala (kleptocracy) kama kielelezo cha genuine class struggle. Kwangu mimi hizo ni vurugu zitokanazo na uongozi mbovu.
Mkuu mtazamo wako kwa yanayoonekana katika uwanda wa uongozi ncini ni huo ulioonyesha kinaga ubaga.
Na nakubaliana na maoni yako kuwa kwa kila atakayeingia madarakani(awe wa chama chochote kile) msukumo mkubwa ni primitive accumulation of wealth , na kama nilivosema huko nyuma hilo linafanyika kwa wizi, rushwa,na hata outright grand fraud.
Haya tunayaona sasa na sitegemei kuwa hata kikiingia chama kingine yatakwisha haya.
Mimi ninayo yaongelea ni matokeo ya kuupanga uchumi wetu kwa kuendekeza hizo sera zinazoendeleza tofauti kubwa za kipato, hivo kuendeleza classes hizo za the haves and the have nots.
Pengine tunapopishana ni position tunazoziona kwamba nini kinaanza na nini kinafuata.
Ni dhahiri kuwa uongozi mbovu, usiotilia maanani matakwa ya wananchi ndio unaolea sera za kupulanila(unchecked and conspicuous theft on a grand scale of resources).
Ni wazi kuwa matokeo ya sera kama hizo ndio zinazaa class struggle.
Najua kuwa kuna wasomi wazuri tu juu ya somo kama hili, lakini tatizo si tu la uongozi mbaya hadi tupate makundi kinzani kijamii, bali vile vile lazima tuwe na analysis nzuri tu ya ownership ya means of production.
Zamani hili lilikuwa rahisi kulicontrol maana serikali ilijizatiti na kuweka ownership ya means of production chini yake.
Mambo yamebadilika sasa maana with private ownership of means of production ndio nasema wanyonge sana sana wanakuwa a tool of production, yaani sana sana wanaweza kuuza nguvu ya(labour) inayoweza kuwa manipulated at will na owners of meands of production.
Na hapo ndio tunaziendeleza classes.