The Godfather

The Godfather

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
652
Reaction score
442
Mwanzoni mwa miaka ya 60 alikuwapo mwandishi mashuhuri aitwae MARIO PUZZO aliandika kitabu wakati huo kikiitwa THE GODFATHER..ndani yake kulikuwa na main character akiitwa VITO ANDOLIN CORLEONE.."THE GODFATHER"

Mwandishi huyo alijaribu kuandika mahusiano yaliyokuwepo baina ya Serikali na Organised Criminal Gangs "the family" na kuonyesha nguvu ambayo the family inayo katika maamuzi ya Serikali na Taasisi kubwa Duniani, kwa kutumia nguvu ya PESA ama kwa jina halisi RUSHWA, ambayo kwa rushwa waliwakamata wanasiasa, wanasheria na watendaji wakubwa katika Serikali.

Mwandishi akaonesha nguvu ya those powerful organised criminal gangs alipoodhihirisha walivyojipenyeza katika THE MOST POWERFUL AND SECURE INSTITUTION IN THE WORLD-the so called ROMAN CATHOLIC CHURCH kiasi cha kufanya ASSASSINATION ya POPE.

Hii ni nguvu ya Ajabu,.,kwa wale ambao wanaelewa nguvu ya Kanisa wanaelewa ninachokimaanisha.

Nirudi katika Uhalisia wa maisha yetu ya KBONGO.,nitaanza kwa mifano hai..

Katika Moja ya Vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM(kikao kikubwa cha maamuzi ndani ya chama kinachoongoza Serikali) Mjumbe mmoja aitwae KILUMBE NG'ENDA - Ambaye alikuwa ni Katibu wa Mkoa wa Dar es salam wa CCM.,aliwahi kutamka jina la GODFATHER kwenye kikao hicho., akimtuhumu kwa yafuatayo:-

@ Kuwa "GODFATHER" sio mwanaCCM kwa maana hana kadi ya Chama hicho.

b) Godfather anakihujumu Chama kupitia TV yake, Radio na Magazeti.

c) Akatoa nyaraka na meseji zenye kuthibitisha kuwa GODFATHER anafadhili CHASO na midahalo na makongamano ya CDM.

d) Ng'enda akataka Chama kimshughulikie GODFATHER kwani anakidhohofisha na kukipa taswira hasi kwa watanzania.

MATOKEO YAKE..,

Baada ya Mwaka mmoja, Kilumbe Ng'enda alivuliwa GAMBA, akanyang'anywa nafasi yake ya Ukatibu wa Mkoa na kushushwa Cheo, mpaka hivi tunavyojadiliana KILUMBE na miongoni mwa watumishi wa CCM wasiojulikana ofisi yao, hadhi yao, cheo chao wala idara (yupo yupo tu)
Na leo MKOA wa Dar ndio ngome ya Upinzani., Kila uchao nguvu ya CCM inapwaya na Upinzani unapata nguvu ktk Jiji hili, lakini CCM ilikubali ifikwe na hayo kuliko kushughulika na THE GODFATHER.

NAIZUNGUZA CCM AMBACHO NDICHO CHAMA TAWALA TANGU UHURU - THE MOST POWERFUL INSTITUTION HAPA NCHINI...wanaoijua nafasi ya CCM katika maisha ya Watanzania nadhan wananielewa.

Lakini kama Kumbukumbu zetu ziko sahihi kidogo, mtakumbuka kila WAZIRI wa Serikali hii ambae kwa namna yeyote alijaribu kugusa interest ya Godfather aliishia pabaya hasa kwa kuipoteza nafasi yake na kusahaulika kabisa katika siasa za nchi hii.

NDUGU ZANGU..,tunaiishi Tanzania ambayo Criminals wananguvu isiyomithilika na isiyozuilika.

Miaka kadhaa nyuma tulimsikia mmoja ya WAZALENDO HALISI wa nchi hii akitamka kwa ujasiri kuwa atashughulika na wauza dawa za kulevya, mtakuwa mashahidi kuwa HAKUDUMU na hatunae tena..

Miezi michache tu alitokea kidume mwingine aliyekuwa akikamata Nyara za Serikali kila asubuhi na jioni..,MAJANGILI wakakosa kupumua na wakahisi kubughudhiwa..kama hamjasahu Huyo KIDUME sasa hivi sio Waziri tena na taarifa nilizonazo ni kuwa hivi sasa MAJANGILI HAWAUI WANYAMA bali wanawasafirisha wazima wazima tena kwa kutumia NDEGE za SERIKALI.

MUHONGO nae alifikiri kwa kuwa amefika nafasi ya uwaziri bila kupiga magoti ya kuomba hela ya kampen kwa MAGODFATHER wala hawategemei kwa lolote akadhani anaweza kufanya jambo la sawasawa..,Nadhan mnashuhudia kinachomkuta.

HII NDIO TISA (TANZANIA ILIVYO SASA)

Wanyonge, masikini wa nchi hii wanayashuhudia haya kuwa kila anayejitahidi kuwahurumia na kujaribu kuwapunguzia maumivu yao na hadha za maisha magumu anaishia kupotea..

Masikini hawa ni wanyonge, ni masikini hawana nguvu wanaishia kulalamika (tena kimya kimya) lakini nafikiri wanakoelekea sasa wataanza kupaza sauti zao..MIMI NITAUNGANA NAO siku wakipata UJASIRI HUO.

BY ALLEX KOWE.
 
hivi kuna Godfather zaidi ya Seth au Rugemarila??

rugemalirila kagawa pesa mpaka kanisani.
 
Hakuna cha Mengi wala Godfather, viongozi mafisadi ni vizuri washughulikiwe...
 
Hizi story zinatusaidia nini tinaochangia ujenzi wa maabara huku wengine wakipeana mabilioni kama pipi?
 
THE GODFATHER:

Ingelikua CCM kuna msafi hata mmoja basi GODFATHER a.k.a Baba wawili angekua amesha shugulikiwa siku nyingi.Tatizo dili nyingi wanapiga wote so ni ngumu kumdhibiti.
 
Kuweweseka (hallucinations)
Tulia ndugu yangu le profeseri muhongo, ulipokuwa na madaraka vita ilikushinda sembuse leo huna kacheo kokote!!!!!!!!

Kubali yaishe sisi wananchi tunakusubiri mahakamani utajuta kumfahamu jk.
 
Wanasiasa ni watu wanafiki sana na ndio wanaosababisha nchi zetu za kiafrika zinaendelea kuwa masikini licha ya kuwa na rasilimali nyingi za kutosha.Wanasiasa wakati mwingine wanashindwa kufanya maamuzi sahihi kwa kuangalia upepo wa kisiasa.Kujiuzulu kwa Prof. Muhongo kumedhihirisha jinsi gani baadhi ya wanasiasa wetu wasivyo na nia njema na nchi yetu.Tumepoteza mtendaji anaejiamini sana, mtendaji ambaye alikuwa anakijua anachokifanya, Mtu ambae naamini kupitia kwake nadhani mafuta na gesi yangetunufaisha zaidi.Namuona Prof. Muhongo anaenda kutumiwa na nchi zingine licha ya kwamba alikuwa na uzalendo.

Unaweza kujiuliza kwa nini Jiji la Dar es salaambado lina shida kubwa ya maji wakati sehemu kubwa ya Temeke ina maji mengi yaliyo aridhini, tatizo ni wanasiasa kutowaruhusu wataalamu kufanya kazi kwa masilahi yao binafsi.Mikataba mingi ya madini Tanzania iliyosainiwa hapo kabla haitunufaishi, Hebu jiulize leo kapatikana mtaalaam wa kutunufaisha kwa kuziba mianya ya wazawa feki basi anaonekana hafai.

Jiulize: Huyo mzawa Mengi ulishawahi kusikia akitoa misaada sumbawanga, kigoma, lindi, makete, etc. Yeye anatoa misaada kwa wachaga wenzake.

Mzawa mwingine Bakhresa ulishawahi kusikia akitoa misaada kwa wakiristo zaidi mara nyingi ni kwa waislamu, tena na ajira anatoa kwa upendeleo kwa waislamu wenzake, ukiwa mkiristo kama unataka kazi nzuri basi ukubali kuslimu.Hii ni mifano ya baadhi ya wazawa ambao unadhani watatunufaisha kumbe watajinufaisha wenyewe na kikundi kidogo tu.
 
Taja direct uwoga sio wa maana sijaelewa maelezo marefu fupisha kwa kifupi tuelewa
 
Ni nani huyo?

Mkuu, unauliza tena? Nani mwenye vyombo vya habari nchini vinavyodeal na Serikali,nani akipenda Muhongo afukuzwe uwaziri leo na anafukuzwa? Haya mambo hayakuaza leo na hayakuanzia Tanzania, watu walishafanya tafiti zao siku nyingi.
 
Wanasiasa ni watu wanafiki sana na ndio wanaosababisha nchi zetu za kiafrika zinaendelea kuwa masikini licha ya kuwa na rasilimali nyingi za kutosha.Wanasiasa wakati mwingine wanashindwa kufanya maamuzi sahihi kwa kuangalia upepo wa kisiasa.Kujiuzulu kwa Prof. Muhongo kumedhihirisha jinsi gani baadhi ya wanasiasa wetu wasivyo na nia njema na nchi yetu.Tumepoteza mtendaji anaejiamini sana, mtendaji ambaye alikuwa anakijua anachokifanya, Mtu ambae naamini kupitia kwake nadhani mafuta na gesi yangetunufaisha zaidi.Namuona Prof. Muhongo anaenda kutumiwa na nchi zingine licha ya kwanza alikuwa na uzalendo.

Unaweza kujiuliza kwa nini Jiji la Dar es salaambado lina shida kubwa ya maji wakati sehemu kubwa ya Temeke ina maji mengi yaliyo aridhini, tatizo ni wanasiasa kutowaruhusu wataalamu kufanya kazi kwa masilahi yao binafsi.

Eti tunataka mabadiliko, kijinga hivi kweli? Nchi za wengine Hawa na akina Mengi walikuwa ni wa kula risasi tu ili nchi isonge mbele.
 
Ukijaribu kuangalia umeongea kwa point sana, lakini kwa maelezo hayo mengi hukujua hata kiabaiologia kila kitu kina mwanzo na mwisho. Nikiangalia hapa unataka kusema kwamba kitu fulani kikifanyika yaani kuwashughulikia huyo au magodfather basi chama chako kitadumu milele!!

Siamini kama kwa maelezo marefu ya namna hiyo huna uwezo wa kutambua kwamba chochote kwenye dunia hii kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho. Sikushauri kushindwa kulala na huku ukikosa amani kujaribu kuangalia kwanini sasa ccm haikubaliki na inapunguza mvuto. Ni kwamba sababu zitakuwa nyingi, lakini ni ili tu kukamilisha biolojia kwamba kila chenye mwanzo kina mwisho.

Kwa kukusaidia wewe na wenzako ambao mmeishi kwa muda mrefu kwenye blanket la propaganda za kwamba ccm itatawala milele, ni bora muanze kuandaa mazingira rafiki ya kuruhusu mabadiliko kwa njia ya amani na itakayolipeleka taifa letu mbele. Kinyume na hapo mabadiliko ni lazima na ccm lazima itoke na hata ikibidi kufa na msipoangalia itaondoka na kufa baada ya machafuko makubwa kulikumba taifa hili.

Ni bora mkaongea na akina Warioba kwani ni wanaccm wenzenu na wao wameamua kusimamia kwenye ukweli,na wameshatoka kwenye usingizi wa ccm kutawala milele bali waanaamini mabadiliko hayaepukiki. Cha muhimu ni mabadiliko ya amani. Ila ukijidanganya sijui Kilume N'genda na hadithi ndefu na mifano mingi ni kujidanganya. Jitambue, mabadiliko hayaepukiki na kila chenye mwanzo .......
 
This thread, I HUMBLY GIVE IT A THUMB UP...!!!

👉 Mengi wasipomdhibiti ATAIHARIBU CCM sana..!!!

☝ I swear to GOD....akija RAIS mwenye ujasiri kidogo tu atleast NUSU YA UJASIRI WA EL....Mengi atajutia...!!!

👉 CCM lazima iwe makini sana na watu wa aina hii with unknown identity within a party, yuko CCM kwa ID tu, but kimatendo na media zake zote ZINAIUA CCM....huu ni UHAINI..!!

💻📺📻✂🔨 CCM najua this time hawana la kumfanya...but NGOJA AJE LAIGWANAN....u will see MOTO...hakuna uselessness...!!!
 
Tujiulize:

Pamoja na yoote hayo, vyombo vya habari vya huyu Godfather unayemsema vinajitahidi walau kutuonyesha sura ya upande wa pili wa hao waliopewa dhamana ya uongozi kupitia chama tawala.

Wewe ulitaka vifanye kazi ya kuwasifia na kuwapamba watu wanaohujumu na kulidhoofisha taifa hili? Kama ilivyo TBC ambayo haionyeshi uhalisia wa masuala ya nchini mwetu?

Back
Top Bottom