Mkuu sana,
Tanzania imejengwa kwa msingi imara wa umoja na mshikamano kwa faida ya wananchi wote.
Hata hivyo, msingi huo unamomonyoka kidogo kidogo kwa wachache kutetea uovu, wizi, ubadhirifu kwa misingi ya urafiki, ukabila, ukanda, vyama n.k.
Maendeleo ya kweli yatapatikana pale tu wananchi kwa pamoja watakuwa wakweli na siyo kumtetea mtu au kumtuhumu mwingine bila kuthibitisha kwa vielelezo.
Hizi hadithi zinaweza kuzidi kuwagawa watanzania, vinginevyo ulete vielelezo kama ifuatavyo;
1. Kwamba GODFATHER ana nguvu kuliko serikali na ana uwezo wa kuiyumbisha anavyotaka.
2. Kwamba hao wote aliowashinda walikuwa wanatetea maslahi ya taifa na wala siyo maslahi binafsi au ya vikundi vinavyowanyonya wananchi.
3. Kwamba GODFATHER hana hoja za msingi ila hao walioshindwa ndio wenye hoja.
Kama unaweza pia naomba ujibu swali hili la kizushi;
Je kuna tofauti kati ya maslahi ya taifa na maslahi ya vyama? Kama jibu ni ndiyo, tunatofautishaje?