The fact that we are still arguing about food, health and education is mind boggling

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,818
11,542
Howzit! Sawubona!

Kipindi nakua, kidato cha pili, nakumbuka siku moja tumetoka shule nilikuwa nikimsikiliza rafiki angu wa kishua njiani analalamika kuwa kwao huwa wanabishana kuhusu hospitali waliyompeleka mzee wao mgonjwa wa kisukari. Kama ni nzuri au wamhamishe.

Alikuwa TMJ walitaka wampeleke Agha khan....Nikawaza: "mimi nikiugua nyumbani tunabishana nipelekwe zahanati au mganga wa kienyeji kusave cost, au nisikilizie tuone kama nitapona mwenyewe, au tumtafute mamdogo jeni yule nesi tumuelezee dalili atuambie dawa tukanunue dukani? Tatizo mamdogo nayeye sikuizi anaringa.

Yani sisi tubabishana kuhusu kupata au kukosa, lakini rafiki angu wanabishana kuhusu quality ya hicho kitu wanachokitaka. Ina maana sisi ni binadamu tusio na thaman yani grade II?"

Hayo mawazo yalinifanya niuchukie sana umasikini, kwasababu niliamini kama nguvu na akili nasisi tumepewa na Mungu, tunaweza kuvitumia kufanikiwa kuyakaba maisha.

Fast forward miaka 10 mbele nimesoma nimetusua dream job na vibisashara vya hapa na pale nikakumbuka story ya rafiki angu kipindi kile.

Nikajaribu kuiunganisha na situation ya hii nchi ilivyo sasa.

Sisi bado tunabishana juu ya wanafunzi kupata madawati? Wamama kujifungua wodini? Wakulima kupata pembejeo? Matundu ya vyoo vijijini? Umeme kukatika? Umeme kwa kila mtu? Dawa mahospitalini? Mabarabara mtaani? Upatikanaji wa chakula? Boom chuoni na mishahara kuingia kwa wakati?

Wazungu walishatoka huko kitambo, saivi wananchi wa kizungu wanabishana kuhusu quality ya chakula wanachokula kama ni healthy au la, Quality ya education wanayosoma watoto wao kama ni bora au la, Quality ya huduma za afya mahospitalini, Quality ya sanaa kama muziki wanazosikiliza, Quality ya sera za chama wanazoshabikia, Quality democracy (How media inaingilia uhuru na maoni & democracy yao).

CCM bado wanatuita vikao na kutuahidi kujenga madarasa na kuleta barabara, halafu sisi tunawapigia makofi kwa! kwa! kwa!

Kuna kale kautetezi (amebana pua)"Ooh hii nchi ni changa, wazungu wameanza kujijenga kiuchumi miaka 400 iliyopita, sisi tumeanza mwaka 61, lets trust the process."

Mimi nawauliza China wameanza lini? India wameanza lini? Qatar wameanza lini?

Fun fact: Dubai wameanza kuuza mafuta nwaka 1969(Tz tulikuwa tumeshapata uhuru) lakini yakaendelea kuwafaidisha waingereza na UAE mpaka walipopata uhuru 1971, but from 1971 mpaka leo miaka 50 tu wameshatupiga gep la maana. Kuna watu watakuja kusema "Ooh kule kuna Mafuta ni utajiri mkubwa, zile ni pesa za mafuta."

Mimi ntawajibu kwa swsli, Hapa Tz Hatuna nini? Maana hiDhahabu kila siku inagundulika maeneo tofauti huko bara, Madini yapo ya kutosha, Gesi ipo, Maeneo ya kulima ndiyo ya kumwaga, Mbuga za wanyama na vivutio vingi vya kumwaga, Inshort vyanzo vya mapato vipo vingi sawa na, au zaidi ya UAE.

Lakini sisi tulivyo wajinga, tumekubali kuwasikiliza wanaCCM wanapotuambia kuhusu matundu ya vyoo na huduma ya maji kufika vijijini.

Tanzania is not poor, Tanzanians have to first enrich their mental wealth, because mental poverty is the cause of our actual poverty... Everyone shouldnt be discussing about Sex, Football and alcohol all the time instead of the fate of our nation that affects us all.

When citizens become mentally rich, it would be easier for them to recognize the traps and potholes set by our weak leaders and thirsty thief gangs that don't want to allow change, because they fear if change happens maybe the beam balance of power might betray them.

Maybe more of other normal citizens might gain power and wealth and take over the precious control over us that they deem so important for them to have, as if it is their right.

I'm not saying I have a solution, Im either not saying Chadema or other parties are the solution(hell, They might even be the worse option for all I know!!). Im not saying CCM has to fall for actual development to take place in this country either.

But I'm just saying ''It is Absolutely mindboggling to me, that after 60 years of independence, we are still arguing about our children just acquiring food, health and education."
 
Africa huenda asilimia kubwa ya watu wake wengi wana udumavu wa akili.
 
Africa huenda asilimia kubwa ya watu wake wengi wana udumavu wa akili.
Sijui tatizo ni nini aise! Mbona zamani kabla ya industrialization waafrika walijitambua.
Mali empire,Songhai empire enzi za akina Mansa Musa tulikuwa fresh??
What happened hapa katikati??
 
Back
Top Bottom