'The Economist' Takes Gloves off on Kikwete...

Mkuu ni siku nyingi sijasoma makala yako iliyotulia kama hii! Sasa tujiulize baada ya hii analysis tuanzie wapi. Tujadili.

In all, big up and thanks for this splendid analysis!

Masanja,
Shukran mkuu,tatizo ni muda kusema ukweli,hata asubuhi kabla ya kukamata vitabu huwa nachungulia kwa muda wa at least nusu saa,ni muda mfupi sana wa kuweza kuchangia kutokana na ukweli mijadala huwa mara nyingi inafurika hapa ukumbini.
Hata hivyo kuna mijadala ambayo inakugusa na inakuwa vigumu kuacha kuongezea kamuda kidogo ka ku type something. Ili uweze kutype hoja nzuri ni lazima uwe na muda na uwe umetulia na kuweza kuisoma mada iliyoletwa hapa JF.
Mapumziko kidogo ya summer yanaanza baada ya wiki ijayo na God willing tutapa muda zaidi.
 
Mzee najua huwa atukubaliani kila kitu but most of the time huwa unatoa maoni very constructives, Goodluck with exams .......
 
FMES,
Mkuu wangu, hawa jamaa hawana mpya ambayo haijazungumziwa hapa JF..ni marudio tu ya kile tunachokifahamu siku zote. Hili gazeti toka zamani linajulikana kuwa ni gazeti la Ubepari...Na kazi zao sio gazetiu tu wame invest ktk Banks na railway wakiamini free trade, internationalism, wanapinga sana Government interference in the affairs of the market..na kikubwa kwao - Uchumi ni Politics!

Ni gazeti ambalo lilikuwa likiwatukana Wachina, Warusi bna hadi kesaho wataendelea kuweka mashaka ktk maendeleo ya nchi kama China. Walikuwa wakiunga mkono Makaburu south, Marekani ktk vita ya Vietnam na Iraq na mengineyo mengi tu ili mradi Kuukomaza Ubepari ktk fikra za watu.. Na wamefanikiwa sana kwani elimu yetu ni pamoja na kupigwa vumbi la macho..

Pamoja na yote haya kuna ukweli ktk maelezo yao megi pamoja na kwamba siku zote wamekataa kutaja waandishi wao au habari hizi wamezikusanya vipi au kupitia vyombo gani..Kuhusiana na Kikwete naamini kabisa wanayozungumza yana ukweli dndani yake lakini mara nyingi ktk Uandishi wao hutegemea relationship ya mhusika (rais) na business world ktk mtazamo wa KULIA zaidi hivyo ni mara chache sana kuona wakisifia mtu au nchi ilotawaliwa na Liberal ideas..

Kama umeona mara zote hawawezi kumsifia mtu kama Nyerere hata kidogo na failure yake ndio signature ya Ujamaa..lakini hawa hawa leo hii failure ya Ubepari nchi zote dunia ya kwanza hawamlaumu mtu isipokuwa biashara yenyewe na sisi wananchi tunao consume mali zao..Na haiwezekani kuuliza kwa nini rais wa lets say Iceland walio run Bankrupt kuzungumziwa kuwa wamefanya makosa kufuata mfumo huo wa Kiuchumi..Kinacholaumiwa ni mazingira ya biashara lakini hii hai apply kwa Wajamaa..

Sii kweli kabisa kuwa Kenya na Uganda wapo mbele yetu ktk elimu ya uzalishaji isipokuwa Tanzania hatuna vyanzo vya uzalishaji na Policies zetu bado haziko wazi kama tuu Mabepari au Wajamaa..Kila siku hofu ya wawekezaji toka nje ni ule uhakika wa Ubepari nchini kuweza kukomaa, vitu kama umilikaji wa ardhi, sheria za ajira pamoja control ya Commanding heights of the economy kuwa chini ya serikali hizi ni sababu kubwa ambayo zinawagusa sana Mabepari sio uwezo wa Wananchi ktk kuzalisha..Kuna nchi kama Vietnam walikuwa mwisho inapofikia maswala ya elimu lakini kwa sababu walifungua milango pamoja na madirisha wazi kabisa leo hii wanasifika sunia nzima lakini basi tazama maisha ya wananchi wenyewe.. very small percentage ya wananchi wananufaika na maendeleo yanayodaiwa. Kama Tanzania, Vietnam ni nchi inayosifiwa kwa maendeleo yatokanayo na michongo ya IMF..Lakini ni lazima nikubali kuwa wenzetu wanajitahidi.. Wanajenga miundombinu yao na wamewezesha nchi yao kufungua viwanda vya uzalishaji pamoja na kwamba pato la mfanyakazi wa kiwanda cha nguo anaweza kuvuta dollar 5kwa kazi ya siku nzima masaa 12 kazini... Yes ukitazama juu juu utaona wanamaendeleo makubwa ya viwanda kufunguliwa nchini mwao lakini tazama pato la mwananchi!..Sasa ukikuta watu kama Kikwete na Mkandara hapa wanaopinga malipo ya namna hii tunaitwa Wajamaa. Ukikuta watu kama Kiwete wanaopinga mgeni kumiliki ardhi kama mali yake wanatuita Wajamaa na kamwe gazeti kaa economist hawawezi kusifia..
Tofauti ya ngu na Mtazamo wa mengi mimi husema hivi..
Ujamaa kwangu ni sawa na ku share mapato iwe umaskini au Utajiri yaani wali uliopikwa unamwangwa ktk sinia kila mmoja wetu anakula kwa kituo..bila shaka kuna ubaya wake esp. ikiwa chakula hakitoshi..
Na ubepari ni Kugawana mapato iwe umaskini au utajiri yaani badala ya wali kumwagwa ktk sinmia moja kuna mtu anagawa wali huo ktk plate za watu.. kwa hiyo mgawaji ndiye anajua nani apate kiwango gani!.. Ukiwa Mkandara hapa usiye kuwa na jina wala address huwezi kupewa nyama ya nundu hata kidogo..
Hizi ndizo tofauti za Ubepari na Ujamaa ktk mtazamo wangu na sio Uzalishaji wa mapato..Kama mapishi ya wali kila mpikaji ana mbinu za mapishi yake with the same tools na kinachogomba kwetu hasa nchi za kiafrika Wapishi wetu (viongozi) wenyewe ni njaa tupu...Humaliza chakula wakiwa bado jikoni na kingine hujifundika ktk mifuko yao ili mradi tu hawana shukran..
Serikali ya Kikwete imekosa mwongozo, watu wanaiba na kuponda fedha kama hakuna kesho, toka ameingia madarakani - the first two yrs kumekuwa na matanuzi ya fedha za Umma kuliko wakati wote wa utawala wa Mkapa..
 
... even disturbing, is the fact that some prominent Wabunge are pushing ahead for remuneration hikes!!!

Kwani kosa ni la nani? Si kura tunawapa wenyewe? Mbunge anakaa miaka 20, hajaleta chochote jimboni kwakwe halafu anashinda tena, je utalaumu mbunge au utawacheka wanaompa kura???

Watanzania tatizo letu kubwa ni maneno maneno tu nothing more nothing less!, Wengi wetu tupo kama FISI, kelele nyingiiiii, ukitupiwa FUPA unakaa kimya! Je wabunge wangapi wanaishi majimboni mwao? si wote wanatesa na mashangingi yao Dar tu, na wakati huo huo wakipalilia watoto wao ili nao wewe kama wao, yaani waingie kwenye siasa na waendelee kula vya wadanganyika!

Ukisoma post nyingi unaona sote hapa tunapiga kelele hizo hizo, ila ndani kwa ndani tunapendelea baadhi ya mafisadi kwa sababu zetu binafsi, uwe ni ukabila, udini au umajimbo, alimradi tu tunaendelea kuupalilia huo ufisadi wao ingawa hatunufaiki kama taifa.
 
Choveki,
Maneno yako ni kweli na hakika kama tungeanza na kujitazama sisi wenyewe labda tunaweza kuelewa kuwa tofauti yetu na nchi nyinginezo zinatokana na watu wenyewe - sisi Wapiga kura..
 
Tusiwalaumu viongozi. Tujilaumu wenyewe kwa kuwarudisha madarakani kila chaguzi.....

Hata mimi nimekuwa nasema hivyo kila siku, wa kulaumu ni sisi wenyewe. Kila kukicha CCM hivi CCM vile, kiongozi fulani kafanya hivi na kafanya vile...kura ikipigwa anashinda tena sasa hapo nani alaumiwe?
Watanzania tuna kale ka katabia ka kutengeneza miungu watu, halafu tunaanza kuwaabudu, kuomba baraka zao,kuwaomba watupatie mkate wa siku na pia wabariki tufipatavyo. Tabia hii itakapoachwa na kukemewa hadharani ndipo maendeleo yatainyemelea Tz, otherwise siye tutaishia domo tu!
 
"Tanzania is not even spending all the aid it is given. Last year, $2.4 billion of pledged funds were not disbursed."

Budget ya Tanzania ni $6 billion per annum. 40%+ ya hii budget ni misaada kutoka nje. Kwa mujibu wa huyu mwandishi, mwaka uliopita Tanzania haikupokea msaada wowote. Hivyo, iliweza kujitegemea. If budget independence means anything (of which I doubt), then last year, Tanzania virtually achieved that target.
 
"Tanzania is not even spending all the aid it is given. Last year, $2.4 billion of pledged funds were not disbursed."

Budget ya Tanzania ni $6 billion per annum. 40%+ ya hii budget ni misaada kutoka nje. Kwa mujibu wa huyu mwandishi, mwaka uliopita Tanzania haikupokea msaada wowote. Hivyo, iliweza kujitegemea. If budget independence means anything (of which I doubt), then last year, Tanzania virtually achieved that target
.

Hapana, Zungu Pale, umeitengeneza hiyo tafsiri.

Kwa mujibu ya huyo mwandishi Tanzania haijatumia hela zote ilizopewa, akafafanua kwamba $2.4 bil za misaada hazikutumika. Hajasema lolote kuhusu msaada wote uliotolewa ulikuwa ni kiasi gani. Hatujui.

Bado hatujajitegemea.
 
Mkitaka kujua nini kimeidekeza na hatimaye kudumaza Tanzania tayari mnakijua. Foreign aid.. Mkitaka CCM wacharuke pigeni kelele wasitishe misaada ya kigeni. Kwa sababu ikisitishwa ndiyo kwa mara ya kwanza ile urgency ya kusimamia fedha zetu wenyewe vizuri itaonekana, ndipo wananchi wataanza kuona impact ya ufisadi (sasa hivi hakuna anayeiona kwani pale cha kitu kiliponyakuliwa wajomba wakajaza vya kwao)..

Naamini adui mkubwa wa uhuru wetu ni misaada ya kigeni!! Ni kama toto kubwa ambalo halitaki kuachia nyonyo!

I find this misleading! Tanzania ni mimi na wewe. Ukisema Tanzania imedekedekezwa, ina maana ni mimi na wewe na raia wote wa Tanzania wamedekezwa. Kwamba hakuna tunachokifanya kwa sababu tumedekezwa. At an individual level, what is the impact of foreign aid? Kwamba, mwananchi wa kawaida katika kijiji cha Kwa Mpiga Miti kule Liwale, hawahangaiki kuboresha maisha yao kwa sababu wanajua Marekani watatoa pesa kwa ajili ya chakula, mavazi, makazi, elimu, afya, barabara n.k. Is this what you mean?

I suspect hii misaada ikisitishwa, hakuna kitakachobadilika. Eti kwamba Serikali haitoi kipaumbele kwenye suala la kukusanya mapato kwa sababu ya misaada ya nje. Kwa ninavyofahamu, hata miradi ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hufadhiliwa na nchi wahisani [technical and financial aid]. So, kukusanya mapato tu lazima "tupigwe jeki" kutoka nje. Argument kwamba misaada ikisitishwa ndio tutakusanya mapato kwa nguvu "doesn't hold enough water". Pengine, hata mapato tunayokusanya sasa yakapungua. Again, aid is not to blame for our messy. Tatizo ni mimi na wewe na Kikwete na wote wenye nchi hii [rejea post ya Dilunga].
 
Last edited:
Hapana, Zungu Pale, umeitengeneza hiyo tafsiri.

Kwa mujibu ya huyo mwandishi Tanzania haijatumia hela zote ilizopewa, akafafanua kwamba $2.4 bil za misaada hazikutumika. Hajasema lolote kuhusu msaada wote uliotolewa ulikuwa ni kiasi gani. Hatujui.

Bado hatujajitegemea.

Dilunga,

Nilivyoelewa ni kwamba kati ya kiasi cha fedha tulichoahidiwa (pledged fund) na wafadhili, $2.4 billioni hazikutolewa kabisa. Hii ina maana hii pesa haikupokelewa na Serikali. Hivyo, ama miradi iliyopangwa kutekelezwa na fedha hizo haikutekelezwa au serikali ilibeba mzigo wote. Na kwa mujibu wa takwimu, utegemezi wetu kwa sasa ni 44% (of the annual budget) - if not mistaken. So, tunajua kiasi cha msaada kinachotolewa (at least estimates).

Hii yote inaonesha mapungufu ya hii article. Hutarajii msomaji wa article yoyote ya The Economist [kwa hadhi yao] kubaki na maswali kuliko majibu. Nafikiri walishapita hatua hiyo.
 
Dilunga,

Nilivyoelewa ni kwamba kati ya kiasi cha fedha tulichoahidiwa na wafadhili, $2.4 billioni hazikutolewa kabisa.

Zungu Pule, kama ulielewa hivyo, mbona ulidai kwamba mwandishi kasema Tanzania "haikupokea msaada wowote"? Ukatufinyangia hesabu moja ya uwiano hapo kana kwamba ndivyo ilivyo. Sivyo.

Tanzania inaishi na kufa kwa misaada. Sasa tusiliwazane upotofu. Makala iko hapa hapa tunataka kupotoshana?
 
Dilunga,

Nilivyoelewa ni kwamba kati ya kiasi cha fedha tulichoahidiwa (pledged fund) na wafadhili, $2.4 billioni hazikutolewa kabisa. Hii ina maana hii pesa haikupokelewa na Serikali. Hivyo, ama miradi iliyopangwa kutekelezwa na fedha hizo haikutekelezwa au serikali ilibeba mzigo wote. Na kwa mujibu wa takwimu, utegemezi wetu kwa sasa ni 44% (of the annual budget) - if not mistaken. So, tunajua kiasi cha msaada kinachotolewa (at least estimates).

Hii yote inaonesha mapungufu ya hii article. Hutarajii msomaji wa article yoyote ya The Economist [kwa hadhi yao] kubaki na maswali kuliko majibu. Nafikiri walishapita hatua hiyo
.

- Mkuu Zungu, heshima mbele sana ndugu yangu ndio maana JF ni mahali pakubwa sana kwa kuchota elimu ya bure, maana ni watu kama wewe mnaoweza kukata ishus kiroho mbaya bila kuogopa, saafi sana na ubarikiwe.

- Endelea kuweka vitu hapa wengine tunakusoma sana kwa pembeni.

Respect.

FMES!

Zungu Pule, kama ulielewa hivyo, mbona ulidai kwamba mwandishi kasema Tanzania "haikupokea msaada wowote"? Ukatufinyangia hesabu moja ya uwiano hapo kana kwamba ndivyo ilivyo. Sivyo.

Tanzania inaishi na kufa kwa misaada. Sasa tusiliwazane upotofu. Makala iko hapa hapa tunataka kupotoshana?

"Tanzania is not even spending all the aid it is given. Last year, $2.4 billion of pledged funds were not disbursed."

Hii sentensi (bolded) unaielewaje brother? $2.4 billions ya fedha zilizoahidiwa na wafadhili hazikutolewa, right? Na kiasi hichi cha fedha ni asilimia 40% ya bajeti ya Tanzania ya $6 billions. Kama utegemezi wa bajeti ni asilimia 40%-44% (kama takwimu zinavyoonesha), ina maana serikali ilijitegemea kwa kiasi kikubwa (almost 100%). I might be wrong, kama utegemezi kwa mwaka uliopita wa fedha ulikuwa zaidi ya asilimia 45%.

Pia kusema "Tanzania inaishi na kufa kwa misaada" ni upotoshaji. Chukulia utegemezi kwa mwaka uliopita wa fedha ulikuwa ni 60% (of $6 billions budget). Kama kiasi cha $2.4 billion hakikutolewa au hakikutumika (kama unavyotaka tuamini), ina maana Tanzania ili-survive bila 2/3 (almost 67%) ya misaada iliyoahidiwa.
 
Last edited:

"Tanzania is not even spending all the aid it is given. Last year, $2.4 billion of pledged funds were not disbursed."

Hii sentensi (bolded) unaielewaje brother? $2.4 billions ya fedha zilizoahidiwa na wafadhili hazikutolewa, right?
Maana sahihi zaidi ni hii hapa:

Nilivyoelewa ni kwamba kati ya kiasi cha fedha tulichoahidiwa na wafadhili, $2.4 billioni hazikutolewa kabisa.

Sawa, umeelewa? Au nisema, umejielewa?

Na kiasi hichi cha fedha ni asilimia 40% ya bajeti ya Tanzania ya $6 billions.
$2.4bil ni sawa na 40% ya $ 6 bil, ndio. Okay...

Kama utegemezi wa bajeti ni asilimia 40%-44% (kama takwimu zinavyoonesha), ina maana serikali ilijitegemea kwa kiasi kikubwa (almost 100%).
Whoa whoa whoa... hold it, stop stop!

Ilijitegemea kwa 100% vipi wakati umeshasema tegemezi la bajeti ni 40%-44% ? That's dopey. Takwimu zimekuonyesha kwamba tegemezi ni 44%, there is no need for conceptual heavy lifting here, tegemezi ni 44%, sasa imekuwaje tegemezi sifuri?

Pia kusema "Tanzania inaishi na kufa kwa misaada" ni upotoshaji. Chukulia utegemezi kwa mwaka uliopita wa fedha ulikuwa ni 60% (of $6 billions budget). Kama kiasi cha $2.4 billion hakikutolewa au hakikutumika (kama unavyotaka tuamini), ina maana Tanzania ili-survive bila 2/3 (almost 67%) ya misaada iliyoahidiwa.
Fuzzy math!

"Tanzania ili-survive bila 2/3 (almost 67%) ya misaada iliyoahidiwa," iliahidiwa kiasi gani? 100% ni ngapi hapo?

Na umejueaje? Huwezi fanya hisabati za asilimia kama hujui au huwezi kujua asilimia 100% ni nini. Tunaongelea sehemu, sehemu ya nini?
Tunachojua ni kwamba $ 2.4 bil kati ya zilizoahidiwa hakitolewa. Hatujui ngapi zilitolewa. Asilimia zako unaziunga unga zisipohusika.

Sisi ni tegemezi karibia nusu ya bajeti yetu, tunaishi na kufa na misaada, period.
 
Tanzania imekuwa haiwezi kutumia pesa zote ilizokuwa allocated kila mwaka kwa sababu kubwa zifutazo:-
  1. kuchelewa kukamilisha taratibu zinazotakiwa ili disbursement iweze kufanyika, hata pale ambapo recepient wake normally government agency and NGO wamekamilisha taratibu wanawekewa mizwengwe na watendaji wetu pale hazina mpaka pesa zinarudi zilikotoka nakumbuka 2005 capacity utilization ya miradi ya ukimwi ilikuwa kidogo sana kiasi cha kuwashangaza hata donors wakati watu wanakufa kwa ukimwi, pesa zilikaa hazina mpaka zikarudishwa geneva
  2. Watanzania tunaweza kuandika proposal lakini ukifika wakati wa kuandika action plan kwa ajiri ya kuchukua pesa tunachukua muda mrefu mrefu sana, ndio maana ukiangalia Waganda kwenye donor projects wanautilize sana kuliko sisi wanachngamka sana
nakubaliana na wanaosema misaada inatulemaza nafikiri umefika wakati sasa watunyime misaada ili wananchi wawe wakali na scarce resources tulizonazo ndio wataweza kubadilisha uongozi, mabadiliko hayatakuja bila watu kuumia kwanza kwa hali ngumu ya maisha.
 
I wish nisingefungua hii thread. I feel like exposed naked!! Gush what is going on..... Nilidhani wenzetu hawaoni kumbe wanaona na wanaelewa. griii....
 
Last edited:
Nafarijika kuona kuwa hata hawa wazungu wamegundua kuwa Jakaya anatumia muda mwingi kuzurula kuomba omba badala ya kutulia nyumbani na kutatua matatizo yanayoikabili nchi!! Nashuku kuwa hiyo misaada anayoomba huko ndio hiyo inayojenga mahekalu huko kijijini kwao Msoga; badala ya kujengea shule na zahanati!!
 
I wonder what the president reads, if he reads that is. Hints zote hizi hapati message, I expected him to do something after Bob Geldof "unceremoniously" gave him hints at the IMF meting earlier this year. Does ikulu subscribe to any intellectual publications?

As if you were reading my mind. True i remember that clip of Bob Geldof. He spit fire on him... but you know huwa hatuelewi.
 
Kwani kosa ni la nani? Si kura tunawapa wenyewe? Mbunge anakaa miaka 20, hajaleta chochote jimboni kwakwe halafu anashinda tena, je utalaumu mbunge au utawacheka wanaompa kura???

Watanzania tatizo letu kubwa ni maneno maneno tu nothing more nothing less!, Wengi wetu tupo kama FISI, kelele nyingiiiii, ukitupiwa FUPA unakaa kimya! Je wabunge wangapi wanaishi majimboni mwao? si wote wanatesa na mashangingi yao Dar tu, na wakati huo huo wakipalilia watoto wao ili nao wewe kama wao, yaani waingie kwenye siasa na waendelee kula vya wadanganyika!

Ukisoma post nyingi unaona sote hapa tunapiga kelele hizo hizo, ila ndani kwa ndani tunapendelea baadhi ya mafisadi kwa sababu zetu binafsi, uwe ni ukabila, udini au umajimbo, alimradi tu tunaendelea kuupalilia huo ufisadi wao ingawa hatunufaiki kama taifa.
Mkuu Choveki,

Hapo juu umepigilia msumari wa ukweli. Watu tumegeuka kuwa wapiga makofi wa teams zetu, hata zikichemsha, sisi tunashangilia tu.

Ndani ya CCM ufisadi au vita dhidi ya ufisadi umegeuka kuwa mtaji wa kisiasa. Ukweli ni kwamba wengi wao wote ni mafisadi tu ambao wakimpata nafasi ya kummeza mlalahoi wanafanya hivyo mara moja. Ukitaka kujua ufisadi wao, angalia uchaguzi wa 2005.

JF hatuna principles ambazo tumejitengenezea za kutusaidia ku assess hawa viongozi wetu. Tunachofanya ni kuangalia mhusika anatoka wapi, ana sura gani na anapingana na nani.

Hivi JK kule kwenye jimbo lake alifanya nini cha maana hadi sisi Wadanganyika tutegemee kwamba angelikuwa rais wa maana Tanzania? JK aliijua system ya CCM na kuitumia kupata urais hata kama hana uwezo wa kuleta change Tanzania.
 
Back
Top Bottom