KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Mkuu,
Kuna vitu viwili nataka tutafakari:
1. Kama hawa minorities wanaweza ku-overcome hizi changamoto zilizopo nchini kwetu, hata sisi weusi tunaweza. Admittedly, sio weusi wote hawajafanikiwa kibiashara. Pia sio minorities wote ni wahalifu.
2. Tuwe watengenezaji wa vitu (makers of things). Hatuwezi kutegemea tu primary products za kilimo, utalii na madini. We need to add value to our resources, export finished goods and earn foreign exchange. Tanzania tunatengeneza kitu gani ambacho wakenya, wamarekani, waingereza, wajapani, wachina watataka kununua kutoka kwetu kwa wingi?
1. Na admitedly vile vile sio minorities wote wamefanikiwa vile vile.
2. Kuhusu kutotegemea primary product na kuwa watengenezaji wa vitu (makers of things). Kinachozungumziwa wa hapa na subject matter ya hii article ni how do you achieve the status of maker of things. Inabidi vile vidogo ulivyonavyo kwanza uviendeshe efficiently ili vingine vifuate. Tunashindwa kuendesha bandari efficiently si kwa sababu we are not makers of things. Bandari ni product tena product kubwa. Tunashindwa kuendesha reli iliyopo. Reli ni product tena product kubwa.
3. Tunazungumzia innefficiency katika mfumo wa utawala unaofanya kusukuma hivi vitu iwe impossible. Sasa unazungumzia manufacturing wakati hakuna umeme. Na Tanzania usitarajie umeme ikiwa TANESCO haiendeshwi efficiently. Hakuna muwekezaji kutoka nje atakayekuja kufanya kazi inayofanywa na TANESCO. Lazima tuwe very dilligent katika kuendesha mashirika kama hili.
4. Maendeleo hayaji kama mvua kwamba mtaanza siku moja muanze kufanya industrial revolution. Labda historia tukisoma yaliyoandikwa tunaamini kuwa yalifanyika overnight. Ilikuwa ni process. Na process inaanzia na vitu vidogo vidogo.
5. Large enterprise, zilianza kama biashara au mashamba madogo madogo. Efficiency katika production ndio inafanya biashara ndogo ziwe competitive na kukua kufikia kuwa biashara kubwa. Inaelekea wengi sasa mnaamini katika injection ya large capital na overnight ku-overturn economy, hiyo haitatokea.
Sasa ninachosema ni nini?
Serikali ni instrument. Ni vehicle ya watu. Serikali inachukua kodi kwa watu. Inao wajibu wa kujenga mfumo utakaofanya uzalishaji katika nchi uwe rahisi na bidhaa za nchi ziwe competitive.
Serikali yetu badala ya kuwa vehicle ya development inakuwa vihicle ya kuwafanya watu wawe maskini. Inneficiency ndani ya serikali maana yake ni kuwa biashara ndogo haziwezi kukua kwani zinabeba mzigo mzito (Kodi ya kijiji, kodi ya wilaya, kodi ya serikali kuu). Ukitaka kuformalize biashara yako inabidi upitie ofisi tano tofauti zenye maofisa ambao umuhimu wao unatiliwa shaka. Ukitaka kusafirisha mzigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine unakuntana na vikwazo kibao (vizuizi barabarani, barabara mbovu, n.k.).
Mapato yanayotokana na kodi badala ya kurudishwa kwenye Elimu, Afya na miundo mbinu yanaongeza ugumu wa maisha kwa walipa kodi kwani yanatumiwa kununua vitu vya starehe kwa warasimu walio ndani ya mfumo wa utawala.
Innefficiency ya serikali ni balaa kwa wafanyabiashara wadogo na ni liability kubwa. Hii liability bila kutoka, hizo tunazoita industrialization inakuwa ndoto.
The economist wanazungumzia jinsi serikali ilivyozama na kutopea kutika uzembe, ufisadi, n.k. Watu wanasema hizi ni siasa. Sawa lakini hizi ndizo zinazoendesha nchi.
Hasara wanayopata entrepreneurs wadogo kutokana na kugharimia serikali kubwa, dhaifu na isiyo na ufanisi ni kubwa. Hii hasara inawafanya wenye biashara ndogo washindwe kuendeleea.
Wanaozungumzia kilimo hamjaenda huko mkafungua mashamba hata madogo muone jinsi kilimo kisivyolipa. Kulima kungekuwa na faida wakulima wasingekimbilia mijini. Ambao hamjakaa vijijini mnadhani watu wanakimbilia mijini kwa sababu hawataki kulima. What a shame?
Si mbali. Nenda hapo mkoa wa pwani tu anzisha mradi mdogo wa kilimo uone. Hautarudi, mizigo ni mingi na inasababishwa na serikali isiyo na ufanisi. Lazima hii serikali irekebishwe ili iwe pro-development kwa watu wake.
Last edited: