Ni kweli kabisa unayosema mkuu, mafundi wengi wa kibongo hawapo updated na teknolojia mpya. Mimi natumia Toyota Opa yenye engine ya D4 mwaka wa tatu sasa haijaniletea matatizo yeyote. Tatizo kubwa tu nililowahi kulipata ni kuwa gari ilikuwa inakataa kukaa sailensi kama kwenye foleni hivi ilikuwa ikizima, muda wote ilikuwa inataka lazima niwe ninakanyaga accelerator hivyo nikiwa kwenye foleni ilikuwa ikinilazimu niweke neutral ili niwe ninakanyaga accelerator.
Nikahangaika sana kwa mafundi wa mtaa wa lindi, mikocheni, maomeni na kwingineko, walikuwa wakibahatisha mara waninunulishe plug, nosel, fuel pump na vitu vingine bila mafanikio. Lakini baada ya kusearch kwenye mitandao yenye forums mbalimbali za magari nikaja kukuta kumbe watu wengi walipata tatizo kama hilo kwa engine ya aina hiyo na solution kumbe ni kubadilisha air cleaner. Fasta nikaenda pale msimbazi kituo cha bahresa nikanunua air cleaner... baada ya kuifunga mpaka leo tatizo lile likawa limetokomea.
Sasahivi gari yangu inakaribia km 100,000 za milage, nilishakuwa na corolla yenye engine ya 5A ambayo imeandikwa wazi kabisa kuwa ibadilishwe timing belt kila baada ya km 100,000. Sasa kwenye Opa yangu yenye D4 sijaona hayo maandishi wala sehemu yenye hiyo timing belt, sasa nauliza je hilo ya kubadilisha timing belt pia linaaply kwenye engine ya D4? pia naomba hapo kwa mafundi wako wanaofanya mainternance hizi kisomi hasa isiwe wale wa DT DOBIE na Toyota Tanzania ambao bei zao wanaoweza kuzimudu ni ma STK, SU na DFP