Bunge siyo serikali kuu, haliko chini ya rais; uzembe wa Bunge usichukuliwe kuwa ni Uzembe wa serikali kuu. Nnimeandika huko nyuma kidogo kuhusu uzembe wa Bunge katika kutunga sheria za nchi.
Bajeti za serikali huwa hazitayarishwi na wanasiasa, kuna jopo kubwa la wataalamu wa uchumi na uhasibu ndio hutayarisha bajeti zile kwa kushirikiana na wataalamu wa field nyingine mbalimbali kutoka mawizarani na tena baada ya kukusanya data za nchi nzima. Waziri anaisoma tu, halafu wabunge wetu wanasikiliza tu.
Kuhusu kumuamini Zitto hiyo ni haki ya kila raia kuamua wa kumuamini mtu wake. Najua Marekani kuna watu wanamuamini Trump hata kama anapoongopa waziwazi. Nimeshafuatilia sana malalamaiko ya Zitto na kuconclude kuwa mengi ni baseless. Anaposema kuwa pesa zimechotwa kinyemela wakati kweli bajeti inaonyesha kuwa zilipitishwa na bunge ni wazi kuwa kajitungia, na iwapo wewe hutapenda kusoma bajeti hiyo basi pia utakuwa ni victim wake na hiyo ni haki yako. Nimeonyesha huko nyuma kuwa manunuzi yote ya ndege yalikuwa kwenye bajeti lakini Zitto aliwahi kuibuka akidai kuwa Serikali ilichota hela hazina kwenda kununua ndege bila kupitishwa na Bunge. Kuna siku alidai kuwa ile Dreamliner ni terrible teen, nikamletea idadi ya ndege zote za Terrible teens na waliozinunua. Kuna mambo mengi yameibuliwa na Zitto na kuonekana kuwa siyo kweli; amekuwa conspiracy theorist mkubwa sana siku hizi. Inahitaji open mind kubwa kutafuta ukweli kamili uko wapi katika kila madai yake, ila ukisoma na confirmation bias in mind, basi utakuwa ni victim wake siku zote.
Kuhusu data mbalimbali za serikali zipo na ni accessible sana, ni kwa vile watu wengi hawataki kuzitafuta wanasubiri kuambiwa na wanasiasa kama Zitto na kumkubalia moja kwa moja hata kama anapotosha. Mimi niliweza kupata data za wizara ya Ujenzi Uchukuzi na mawasiliano (
http://mwtc.go.tz/), Wizara ya fedha (
http://www.mof.go.tz/), benki kuu (
Bank of Tanzania), national Bureau of Statistics (
https://www.nbs.go.tz); nina imani unaweza kupata data za Wizara nyingine kwa njia hiyo hiyo kwani website za serikali ziko current sana sasa hivi kuliko zamani. Hata World Bank na IMF wanatumia data hizo hizo, hawana kitengo chao binafsi cha kukusanya data za nchi. Data za Uchumi kutoka World Bank ni hizi hapa kwenye excel file, na report ya NBS iko kwenye hilo faili la pdf. Zaidi zaidi ninataka uangalie hii page ya World bank ambayo ina visual aids nzuri kuliko kupitia namba za kwenye hilo excel file.
Tanzania from The World Bank: Data
Weka mkazo kwenye hiyo Graph ya kwanza ya GDP uweke mouse yako mwisho kabisa itakuonyesha kuwa GDP ya mwaka 2018 ilikuwa ni
$57.437b kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini
Halafu ukirudisha mouse nyuma kidogo, itakuonyesha kuwa GDP ya mwaka 2017 ilikuwa ni
$53.321b kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini
Sasa wewe piga mahesabu ya growth rate kutoka 57.437 mwaka 2017 hadi 53.321 mwaka 2018 kama hutapa
{(57.437-53.321)/53.321}x100=7.72% tena ambayo ni zaidi ya ile iliyoko kwenye ripoti ya NBS na Benki kuu; inawezekana NBS wanatumia moving average method kuliko hiyo instantaneous value.
Hata hivyo, unaona kuwa hiyo ripoti ya 5.5% ni namba za kupikwa tu. Hata kama ingekuwa ni moving average ya miaka kumi kumi bado isingefika namba hiyo ya 5.5% ya IMF. Sijui motive ya IMF kupika namba hizo lakini data zinaonyesha kuwa utegemezi wa Tanzania kwa IMF umepungua sana kwa miaka ya hivi karibuni. Unlike World bank, hawana data za kina kuhusu Uchumi wa Tanzania; angalia hapa
Utasemaje kuwa data zao ndizo za kuaminika kuliko za Serikali na za World bank wakati wao wenyewe hawana database yoyote?
Lakini pia utaajiri Watanzania wapi katika kazi zinazohitaji teknolojia na elimu?
Wakorea wanajenga daraja, wana tenda na wanataka faida. Utaajiri watanzania wapi zaidi ya wafunga nondo? Na huyo mfunga nondo unataka alipwe milioni 6! Please
Reli inajengwa na Waturuki,sababu ni moja sisi hatuna uwezo wa ufundi
Hii haina maana ni mazezeta, hapana, ni kwasababu ulaji umetangulia na kazi haitafanyika
Unaweza kushangaa mataruma ya mbao! ilimradi watu wote kuanzia juu wanapiga
Sasa sijui ni miradi gani ikiwa kule Songea daraja la miti limejengwa kwa milioni 7
Pitia kumbukumbu za JF utaona hilo, na huo ni mfano mzuri kwamba sisi bado. Matumbo tu
Si kweli na nina mifano ya kutosha. Si kweli kabisa
Inawezekana wewe hujafanya kazi za kwenye construction projects; sehemu kubwa ya kazi hizo hufanywa na watu wasiokuwa na elimu ya juu kama unavyodhani. Kinachohitajia ni wataalamu wa kuwasimamia kuhakikisha kuwa kazi inafanyika vizuri. Project kubwa inaweza kuwa na mainjinia wawili tu pamoja na superintendents labda 10 tu kati ya wafanyakazi 300 wa project ile.
Mimi nilianza kufanya kazi kwenye ile miradi ya wakati wa Nyerere mara tu nilipotoka JKT; nilifanya kwa miaka miwiwli (tulikuwa na kitu kinaitwa Azimio la Musoma wakati huo). Nilianza kwenye mradi wa kujenga barabara kutoka Mororgoro hadi Dodoma iliyokuwa inafanywa na kampuni ya Kibrazili, baada ya hapo nikahama kutoka Dumila na kwenda Mororgoro Mjini na kujiunga na kampuni nyingine ya Kibrazili kujenga karakana ya reli, muda mfupi tu nikahamia mradi wa kampuni ya wakanada ya iliyokuwa inajenga Bwawa la Mindu kwa kuwa ilikuwa ikilipa zaid ya wabrazili, na mwishowe nikahamia kampuni ya Magunia kule Industrial Park kwa kupewa cheo cha Supervisor; dakika za mwishoni nikahamia kiwanda cha Canvass (kwa sababu za ujana tu kwa vile kiwanda kile kilikuwa na wasichana wengi wakati huo) kabla sijasepa kwenda Chuo Kikuu. Katika kampuni zote nilizokutajia, kasoro Canvass, wazungu au wabrazili walikuwa ni wale mabosi wa juu tu: Project Manager, Mainjinia, na Superintendents basi. Maofisa utawala wote, accounting, machine operators, madereva, mafundi, maforeman, vibarua, mesenja, wapika chai na kahawa, wafagiaji, walinzi na kila mtu wa chini walikuwa ni watanzania tu.
Siku hizi unaona kampuni ya nje inaleta hata vibarua kutoka kwao! Wachina walileta vibarua kibao kujenga uwanja wa taifa na baada ya project wakakwepa kurudi kwao, lao hii tunasuguana nao mitaani!
Unfortunately Jamiifurms hairuhus attachement za excel; hata hivyo unaweza kulipta kwenye hiyo website ya world bank niliyoweka link yake hapo juu