The case against MUSTAFA MKULLO

Huyu hatufai kabisa kama data zenyewe ziko hivi,tutaendelea kuendeshwa mpaka lini mimi nadhani Tanzania tunahitaji mapinduzi ili kurudisha adabu ama mnaonaje maana wote tunageuzwa wajinga na mazmbukuku
 
The man is placed at a strategic place ready for raising money for CCM, haendi kokote unless yatokee yalimtokea Chengele
 
The man is placed at a strategic place ready for raising money for CCM, haendi kokote unless yatokee yalimtokea Chengele

Atatoka tuu it is just a matter of tym,na siku zenyewe sii nyingi sana zilizobaki, ulitegemea Cents kuumbuka that soon????
 
That the Minister of Finance Mr. Mustafa Haidi Mkullo owe one of our premier Bank a loan of 30,000,000 plus accrued interest to the total of about 24,000,000 ( a debt of abt 54,000,000). It has been allegedly estabilished with documentary proof that Mr. Mkullo while he was a Deputy Minister of Finance alipatiwa mkopo huo ambao hadi hivi sasa hajalipa kitu chochote kinachoeleweka....

So, anapojiandaa kusimama kusoma bajeti vile vinzi vinavyozunguka vimeahidi kuonesha ushahidi wa deni hilo kubwa muda mfupi baada kabla ya yeye kusoma bajeti hiyo.. so, kama ninyi na miye nimekaa ku subiri kuona kama 'vyalika'?
 
Mkullo is another Chenge.

Hivi hao wadeni wake wasipolipa kodi na kuja kumuomba mwanya wa msamaha wa kodi ataweza kuwakatalia?
 
That the Minister of Finance Mr. Mustafa Haidi Mkullo owe one of our premier Bank a loan of 30,000,000 plus accrued interest to the total of about 24,000,000 ( a debt of abt 54,000,000). It has been allegedly estabilished with documentary proof that Mr. Mkullo while he was a Deputy Minister of Finance alipatiwa mkopo huo ambao hadi hivi sasa hajalipa kitu chochote kinachoeleweka....

So, anapojiandaa kusimama kusoma bajeti vile vinzi vinavyozunguka vimeahidi kuonesha ushahidi wa deni hilo kubwa muda mfupi baada kabla ya yeye kusoma bajeti hiyo.. so, kama ninyi na miye nimekaa ku subiri kuona kama 'vyalika'?

Hii inaonyesha jinsi JK na serikali yake ya CCM jinsi walivyo bega kwa bega kutafuna pesa ya walipa kodi kiroho mbaya, na jinsi wasivyo na nia ya kupiga vita UFISADI.
 
Mkullo is another Mbowe!!!!
I dont see why the name of the bank in this case is withheld, any reason MMK? Alichukua huu mkopo lini exactly?
 
Subiri vinzi vitakuletea habari. Hivi Mbowe ni waziri? Au basi imekuwa ni ushabiki?
 
Subiri vinzi vitakuletea habari. Hivi Mbowe ni waziri? Au basi imekuwa ni ushabiki?

Nazungumzia wanasiasa waliovuta mkwanja mnene na kukaidi kurudisha katika muda wa makubaliano kwa sababu zao binafsi, sio ushabiki mkuu. They all belong to the same group when it comes to their financial reputation, wangekuwa UK hawa wote wangekuwa na poor credit score!
 
Ushahidi unaonyesha Mbowe alirudisha pesa, Je, huyu waziri ambaye huna hata chembe ya data za hizo pesa alizokopa wakati tunategemea vinzi vitupe dataz utasema nini? Maana unaonekana kuanza kutetea wakati info... huna.

Hiyo bad credit unaipima vipi? Rejea kwenye thread ya pesa alizokopa Mbowe ujiridhishe.
 
Kana Ka Nsungu,

Nakubaliana na wewe kwamba kuna connection kati ya Mkulo na Mbowe kama hii habari inavyoonyesha. Na kwamba Mkullo angekuwa na credit score mbaya Viwanja.

Lakini kumtetea Mbowe, naweza kusema, hata nchi za nje mkubwa wa kampuni akikopa kwa niaba ya Kampuni, huwa sifa mbaya ya kutolipa deni haimwendei yeye bali kampuni yake. Ndio maana Marekani kampuni zina credit score pia. Hata majimbo nayo yana credit score.


Mbowe aifilisi NSSF

Rai
Thursday, 13 March 2008


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.

Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.

Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo kwa sasa ndiye Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.

Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.

Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.

Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.

Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.

Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.

Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.

Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.

Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.

Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.

NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.

Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.

“Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria,” alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.

Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.

Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.

Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katiak moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.

Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.

Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini.
 
Ushahidi unaonyesha Mbowe alirudisha pesa, Je, huyu waziri ambaye huna hata chembe ya data za hizo pesa alizokopa wakati tunategemea vinzi vitupe dataz utasema nini? Maana unaonekana kuanza kutetea wakati info... huna.

Hiyo bad credit unaipima vipi? Rejea kwenye thread ya pesa alizokopa Mbowe ujiridhishe.

Ukweli ni kwamba Mbowe hajamaliza kulipa deni, so far ameweza kulipa sehemu tu ya deni. Vigezo vya credit scoring unaweza kuvipata kwenye www.experian.co.uk au www.equifax.co.uk. So far sijaona kokote kwenye post zangu nilipomtetea mtu, read btn the lines.
 
Nilipo sikia Mkulo ni waziri wa fedha, Nepi yangu ilianguka chini kwa kutetemeka. Mkulo aliiba sana pale NSSF na alikuwa another Balali pale NSSF.
Alichofanya Balali ndicho Mkulo alifanya. Michango ya wavuja jasho ipo mikononi mwa wachache akiwa mmojawapo na haitarudi ng'ooooooooo.

Naye lazima aende chiniii

je Mwungana ananguvu hiyo?????????
 
Ukweli ni kwamba Mbowe hajamaliza kulipa deni, so far ameweza kulipa sehemu tu ya deni. Vigezo vya credit scoring unaweza kuvipata kwenye www.experian.co.uk au www.equifax.co.uk. So far sijaona kokote kwenye post zangu nilipomtetea mtu, read btn the lines.

Sasa mwaga data hapa zimebaki ngapi na huyo Mkullo karudisha ngapi? Ili tuweze kumkoma nyani hapa mchana kweupe maana ya Mbowe tunayajua na pumba zikija tunaziona. Haiwezekani kila hoja ahusishwe Mbowe wakati yeye sio waziri au amepewa dhamana yoyote ya kuliongoza taifa, wakati waliopewa hiyo dhamana wanakenua na kutapanya pesa ya walipa kodi.
 
Mkullo is another Mbowe!!!!
I dont see why the name of the bank in this case is withheld, any reason MMK? Alichukua huu mkopo lini exactly?


mwaka jana akiwa Naibu Waziri... mfano wako kuwa Mkullo is "another" Mbowe waweza kuwa na ukweli... lakini Mbowe siyo Waziri wa Fedha!
 
Sasa mwaga data hapa zimebaki ngapi na huyo Mkullo karudisha ngapi? Ili tuweze kumkoma nyani hapa mchana kweupe maana ya Mbowe tunayajua na pumba zikija tunaziona. Haiwezekani kila hoja ahusishwe Mbowe wakati yeye sio waziri au amepewa dhamana yoyote ya kuliongoza taifa, wakati waliopewa hiyo dhamana wanakenua na kutapanya pesa ya walipa kodi.

Dua unaeleweka vizuri ukisema hii mada haimuhusu Mbowe. Lakini ishia hapo. Ukianza kusema deni alishalipa unafungua milango ya arguments zinazosema deni hakulipa.

Hata mimi sipendi Mbowe anavyodhihakiwa kwa sababu nadhani ni mwanamapinduzi. Lakini tusimame kwenye ukweli. Kama kampuni yake haijalipa deni usiseme kalipa, halafu ukibanwa unasema, oooh, hii siyo mada ya Mbowe.

Ungeng'ang'ania hicho hicho, kwamba hii sio mada ya Mbowe. Nukta.
 
Sasa mwaga data hapa zimebaki ngapi na huyo Mkullo karudisha ngapi? Ili tuweze kumkoma nyani hapa mchana kweupe maana ya Mbowe tunayajua na pumba zikija tunaziona.

Rejea kwenye thread ya pesa alizokopa Mbowe ujiridhishe.
 
Back
Top Bottom