THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal

Sio haikufikirika..... sema sisi ndo tuna kawaida ya kutoamini from zero to hero...

Ila ye mwenyewe alijua atakuja kuwa nani....

Sema akifirisika akawa kam mim ndo atakuwa accidentally broke
Just imagine asingemeet with the girl, asingetengeneza facemash... inshort, inaweekana aliwaza ila the way it happened it was unexpectable
 
Vipi mkuu umeishiwa mb? Njoo umalizie ulichokianzisha... Interesting
 
Jarib kua na ufupisho mkuu
Kunywa pombe,kunyanyuka kusogelea
Story ndeeefu inachoshaaaaa siamin kama kuna pple zimeisoma yote kama ilivo
Mwisho
Kuwa mstaarabu kwa kuto-qoute uzi mrefu namna hii, jifunze kum-tag unayetaka aone comment yako. Ni kero na usumbufu kwa watumiaji wa simu.
 
Screenshot (126).png
Screenshot (86).png
Screenshot (92).png



Ilikuwa imekaribia miezi miwili kupita tangu Cameron na Tyler wamwambie Mark kuwatengenezea website yao, Mark amekuwa akiwaambia kuwa kila kitu kinaenda sawa kabisa, email hamsini na mbili pamoja na simu nyingi ambazo wamekuwa wakiwasiliana na Mark zote Mark alionesha kuwa na shauku na hamu ya kuitengeneza website hiyo kama ilivyokuwa hapo mwanzoni, Cameron na Tyler walimwambia Mark kuwa walifikiri ni kazi ya kutochukua muda sana lakini sasa wanaona inaenda taratibu sana kuliko walivyotegemea, Mark aliweza kuwajibu_ " Nimekaribia kumaliza coding, inaonesha kila kitu kinafanya kazi vizuri, nina kazi za darasa natakiwa nizifanye ntarudi baadae kuendelea"
Mpaka wiki ya saba walikuwa hawajapata email yoyote ile kutoka kwa Mark au chochote kile kuongezwa kwenye website yao, Tyler alianza kuingiwa na hofu aliona imechukuwa muda sana kwani yeye alifikiri kuwa mpaka ule muda walioenda likizo website yao ingekuwa imeshakamilika na kuanza kutumika hivyo alimwambia Cameron amtumie Mark email kumuuliza kama atamaliza hivi karibuni, Cameron alituma email, Mark alijibu "Samahanini inanichukua muda kuimaliza kazi yenu, nimejazwa na kazi nyingi sana wiki hii, nina project tatu za programming, nina mtihani wa semister ambao utakuwa ni jumatatu vilevile ninavitu vingi ambavyo natakiwa nivifanye siku ya ijumaa" ila aliendelea kuwaambia kuwa bado alikuwa anaendelea kuitengeneza website kwa kadri alivyoweza, alizidi kuwaambia kuwa "Nimeshafikia mbali, nimefanya baadhi ya mabadiliko japo sio yote na yameonekana kufanya kazi kwenye kompyuta yangu ingawa bado sijaweka katika website "
Mark pia aliongezea kitu ambacho kilimchanganya Tyler, alisema_ "Bado ninamashaka kama kuna ubora wa kutosha katika website wa kuweza kuvutia watu na kupata idadi ya watu kamili wanaohitajika ili website iweze kufanya kazi. Na kwa hali ilivyo sasa kama website itapata watu wengi kama ambavyo tunahitaji, sijui kama kuna uwezo wa kutosha kutoka kwenye internent provider mnayotumia wa kuweza kukabiliana na msongamano bila kuwa na shaka yoyote ile ambapo hii itachukua baadhi ya siku kuitengeneza"
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mark kueleza matatizo kama vile 'website inakosa ubora' lakini mpaka hapo bado alionesha kuwa na shauku ya kuendelea kuitengeneza website na alikuwa amekubali kuwa itakuwa na mafanikio makubwa
Baada ya email hiyo Tyler alimsisitiza Mark kuwa waonane, alikuwa ametumainia kuwa website yao ingekuwa tayari kwenda online mpaka muda huo,alihofia kuwa siku zinavyozidi kupotea bila kufanikisha huenda kutatokea watu wenye wazo kama lao na kuwawahi kutangaza website yao, kwa kuwa walikuwa mwaka wa mwisho walitaka hicho kitu kifanyike haraka kama iwezekanavyo lakini kila walipotaka kuonana na Mark, Mark alipeleka ratiba mbele akidai kuwa anakazi nyingi za shule kuweza kupanga ratiba yoyote ile ya kuonana nao.
Hatimaye, Divya, Cameron na Tyler walifanikiwa kuonana na Mark tena, kama ilivyokuwa mwanzo, Mark aliwapongeza na kuwasifia na kusema ni kwa jinsi gani ambavyo alifikiria kuwa wazo lao la Harvard connection litakuwa kubwa na lenye mafanikio lakini mara tena bila sababu akaanza kutoa udhuru akieleza kuwa hakuwa na muda mwingi wa kuweza kutengeneza sana katika website ile, kwamba anaproject nyingi ambazo zinachukua muda wake mwingi, Tyler alihashumu kuwa Mark alikuwa anaongelea project za darasani kwake sababu Mark hakuweka bayana kuwa zilikuwa ni project zipi, pia Mark alikuja na matatizo mengine ambayo hapo mwanzo hakuwahi kusema kuhusu website hiyo, alisema kuwa yeye sio mtaalamu wa kutengeneza/kudesign 'cover ya website' ambayo ilitakiwa kutengenezwa, Tyler alionekana kushangaa na kutoelewa kwa maana alichokisema Mark alimaanisha ni muonekano wa jumla wa kurasa ya juu ya website ambapo hapo nyuma ndo alionesha kuwa anakipaji na ni mtaalamu pale alipotengeneza websit yake ya Facemash
Mark alizidi kuchanganya baada ya kusema kuwa baadhi ya vitu ambavyo alihitaji kutengeneza ili website ianze kufanya kazi vilikuwa vinakera, alisema kuwa ni vitu ambavyo vilikuwa havimvutii kuvifanya, akasisitiza tena kuwa website ilikuwa haina ubora na kuwa watahitaji kuwa na uwezo mkubwa wa server.
Tyler akaanza kuwa na hisia kuwa labda huyo mtoto alikuwa anataka kuwapeperushia ndege wao, kwani mara ya kwanza alikuwa na shauku iweje sasa aanze kuwaambia kuwa alikuwa hana hamu ya kutengeneza website hiyo! Tyler alistaajabu kuwa huenda Mark alikuwa anachoshwa sana na kazi za darasani, huenda alikuwa anabidii sana darasani, kama alivyokuwa na uzoefu kutoka kwa raffiki yake mwingine kuwa engineers mara nyingi huchoka sana na wakati mwingine hukereka na baadhi ya vitu sababu aliona excuses za Mark zilikuwa hazina maana, tatizo la server? hivyo waongeze server! tatizo la front-end page? wakati mtu yeyote yule angeweza kutengenez front-end page! Tyler aliwaza na kuona labda Mark alihitaji muda wa kuwa peke yake ambao angeweza kuendelea na kazi hiyo na kurudiwa na shauku tena ya kuendelea kutengeneza website hiyo.
Tyler, Cameron na Divya waliondoka kiasi flani wakiwa na msongo wa mawazo kwani ilikuwa inachanganya sana, baada ya siku zote hizo Mark kuwaambia kuwa kila kitu kilikuwa kinaenda sawa sasa anawaambia tena hajakamilisha na hana shauku tena ya kutengeneza website hiyo bila kuwa na maelezo yanayoeleweka! Ilikuwa ni zaidi ya kuangushwa kwani alifikiri kuwa mtoto genius amewaelewa ni nini walitaka kukitengeneza na kwa kuzingatia kuwa aliona kilichokuwa tayari kimefanyika na kisha yeye mwenyewe kusema kuwa kazi iliyobaki ni rahisi sana kuimalizia kwa mtaalamu kama yeye ingemchukua masaa kumi au kumi na matano, lakini sasa alikuwa analeta huo uchafu mwingine wa server na front page, kwakweli haikuleta maana kichwani mwa Tyler, Tyler aliamua kuwa kitu kizuri cha kufanya ni kumwacha Mark kwa wiki kadhaa labda kuwa ataweza kurudiwana hali yake ya zamani
" Na kama asipoweza kumaliza ndani ya hizo wiki kadhaa?" aliuliza Divya
Tyler aliawaza kuwa labda Mark Zuckerberg hakuwa kama walivyomfikiria, labda alikuwa ni kompyuta genius asiye na njozi halisi
"Kama ikitokea, itabidi tutafute programmer mwingine, progrmmer ambae anaeelewa njozi kubwa" alijibu Tyler

Cameron na Tyler Winklevoss
Screenshot (99).png


***

Mark alifika bwenini kwake akikimbia huku akimpita Eduardo mlangoni ambae alikuwa akimsubiri kama walivyoahidiana kuonana, Eduardo alimwuliza Mark kwa nini amechelewa, Mark hakujibu chochote badala yake aliingia ndani haraka huku Eduardo akimfuata kwa nyuma, Eduardo alizidi kumwongelesha lakini Mark hakujibu chochote kile, Eduardo aliamua kumuacha akihisi huenda Mark alichoka ukizingatia ni wiki kadhaa amekuwa halali vizuri.
Mark alifika mezani kwenye laaptop yake na moja kwa moja kwenye project yake aliyokuwa akitengeneza 'thefacebook' ambayo sasa alikuwa akimalizia kuitengeneza, alikuwa anaongezea vitu vya mwishomwisho ili iweze kukamilika rasmi, vitu kama kudesign pamoja na coding vilikuwa vimekamilika na site ilionekana ni nzuri ya kuweza kuwavutia watu kuisogelea
"Inaonekana ni nzuri sana" Eduardo alisema, Mark alitikisa kichwa kukubali
"Nafikiri watu wataenda kuikubali" aliongeza Eduardo
Mark alipitia site nzima, alifungua kurasa ya ndani ambayo mtu angeona baada ya kujiasajili na angeweza kuweka maelezo yake binafsi, vitu vilivyokuwa katika website hii ni vitu ambavyo viliaksi maisha ya chuoni hivyo alijua lazima watu wangeeenda kuchizika nayo
Alifungua kurasa ya juu ambayo ingeonekana mara baada ya mtu kuingia kwenye website hiyo ambayo ilionekana na maandishi kama

(Welcome to thefacebook)
pamoja na maelezo mengine ikiwemo 'register' and log in'
Website ilihitaji uwe na email ya Harvard ili uweze kujiregister, hivyo ungeweza kujiunga na facebook iwapo ungekuwa mwanafunzi wa Harvard pekee. mwishoni mwa kila kurasa Mark altaka jina lake litokee hivyo aliandika 'A Mark Zuckerberg production' Eduardo hakuwa na shida yoyote ile kwa Mark kufanya vile, kwani yeye hakujali umaarufu akizingatia kuwa Mark ndie amekuwa akifanya kazi ile pasipo kulala na akikosa kwenda darasani karibia kila siku bila kujali kuwa mitihani ilikuwa imekaribia.

Mark Kuwa pale mbele ya website yake kulimpa ahueni, tayari alikuwa ameshaandikisha jina la website ile kama 'thefacebook.com' na tayari alikuwa amekodi servers ili kuweza kukabiliana vizuri na jam ya watu itakayotumia website yake na hivyo basi 'the facebook.com' ilikuwa tayari kwenda hewani

Screenshot (87).png

"tufanye hivi" Eduardo alimwambia Mark kisha akafungua email address yake na kwenda kwenye list ya contact email zake, "hawa watu ni wanaclub wenzangu wa phoenix kama tukiwatumia wao hii website basi itasambaa kwa haraka sana"
Mark alikubali wazo lile la kuwatumia wale walioitwa ' social stars' na ukizingatia ile ilikuwa ni social network hivyo kama wataipenda ni lazima itasambaa kwa haraka, kwani kama Mark angetuma kwenye list za email kwake, website ingekomea darasani kwake basi na kukwama hapo hapo

"Hayaaaa......." waliandika ujumbe mfupi wa kuitambulisha site ile na kisha
"Twendeeeee....." wakabofya sehemu ya kutuma ujumbe, ujumbe ukaenda na kwa mara ya kwanza thefacebook ikawa online ikiwa ni tarehe 4 february 2004

"Twende tukapate vinywaji ni muda wa kusheherekea" Eduardo alimwambia Mark
"Hapana ntakaa hapahapa" Mark alijibu
Eduardo alimuuliza kama anauhakika, Mark hakujibu chochote, Eduardo alimuuliza tena kama ataendelea kukaa hapo kushangaa screen ya laptop yake, Mark hakujibu chochote pia,alikuwa kimya mbele ya kompyuta yake akiitazama, Eduardo aliamua kumwacha rafiki yake ambae hakumwelewa maadam alikuwa amedhamiria kuketi pale na kompyuta yake hivyo hakuna shida kwake.

Eduardo Saverin
Screenshot (102).png


***

Tyler na Cameron walikuwa wakifanya mazoezi yao ya mtumbwi, Divya alifika akiwa na gazeti mkononi huku akionekana kuwa na hasira
"Tyler unatakiwa uone hili gazeti"
Tyler na Cameron walimsogelea na kumwambia awasome linasema nini kwa wao mikono yao ilikuwa imelowa maji hivyo wasingeweza kushika gazeti lile, Divya alianza kuwasomea gazeti lile ambalo lilikuwa na habari iliyomhusu Mark kuanzisha website iliyoitwa thefacebook
gazeti lilisema "ni baada ya Mark E.Zuckerberg kukosa uvumilivu wa kusubiri facebook ya ujumla kutoka chuoni na kuamua kuchukua maamuzi mkononi mwake__"
"Subiri kwanza" Cameron aliingilia " ni nini hicho"
Gazeti la leo" Divya alijibu "sikiliza" aaliendelea kusoma
" Baada ya wiki ya kutengeneza code, Zuckerberg ameweza kuiachia thefacebook.com jumatano mchana ya wiki iliyopita...."
Tyler alishangaa 'jumatano iliyopita?!' inamaanisha ni siku nne zilizopita!
"Hii haiwezekani! ameachia website?!" Tyler aliuliza kwa kutoamini
"Yeah" Divya laijibu." Sikiliza hapa alivyonukuliwa akisema"
Divya alisoma nukuu ya Mark gazetini
"Kila mtu amekuwa akiongelea kuhusu facebook ya chuo , ni kitu cha kijinga ambacho itaichukua chuo miaka kadhaa kutengeneza wakati mimi Naweza kutengeneza tena bora zaidi yao, tena naweza kutengeneza ndani ya wiki moja"
"Ndani ya wiki moja?!" Tyler alishangaa, wakati imewachukua miezi miwili bila kukamilisha website yao kumbe alikuwa bize akitengeneza website yake! Alidai hana muda kumbe alikuwa ana muda wa kutengeneza website yake mwenyewe na sio ya kwetu! Gazeti liliendelea kuelezaa kuwa zaidi ya watu mia sita wameshajiunga na thefacebook na watu mia tisa walitegemea kujiunga siku hiyo

Tyler hakuamini, alisema haiwezi kuwa kweli, watu mia tisa kujiunga na hiyo website ndani ya siku nne?! Hapana hiyo haiwezekani, Mark hakufahamu watu miatisa, Mark hakuwa na marafiki iweje leo tayari watu mia tisa wameshaifahamu website yake?!
Divya aliwaelezea thefacebook jinsi ilivyo ambapo tayari alikuwa ameingia kuitazama, Tyler aliona kuwa haifanani na waliyotaka kuitengeneza lakini kuna baadhi ya vitu vilifanana
Tyler aliona sio sahihi, aliona kuwa kwa vyovyote vile ule ulikuwa ni kama 'wizi'

Divya aliwaeleza kuwa Mark alipata msaada wa kifedha kutoka kwa rafiki yake aitwaye Eduardo ambae pia amekuwa kama sehemu ya mmiliki. "sababu kailipia?! " aliuliza Tyler
"nahisi hivyo" Divya alijibu
"Kwa nini Mark hakuja kwetu?!"
Walijiuliza, Mark alijua kuwa walikuwa wanapesa kwa nini hakuwaambia kama kulihitajika pesa kuanzisha site ile, vinginevyo basi alihitaji pesa ya kutengeneza kitu alichowaibia ambacho hakutaka wajue, Tyler alizidi kuchanganyikiwa baada pia ya kuona kuwa hawakuwa na mkataba wowote ule walioandikishana zaidi ya kushikana mikono tu nakupongezana.

Kulikuwa na nukuu kwenye gazeti pia kuwa Mark alisema "anatumaini website hiyo itamsafisha na tuhuma zake za mwanzo za kutengeneza Facemash.com" Tyler alizidi kuchukia kwani aliona kuwa Mark aliwaibia mpaka mneno waliyomwambia siku ya kwanza.

Waliulizana wafanye nini, kitu cha kwanza walichoamua kilikuwa ni kumpigia simu baba yao
Tyler alimweleza baba'ke kila kitu na kusisitiza kuwa kuna vitu vinafanana na idea yao, Tyler alitaka haki itendeke, haki ifuatwe kwani aliona Mark alichowatendea hakikuwa sawa kwenye ulimwengu wao wa haki na usawa, Tyler alisisitiza pia kuwa haikuwa kuhusu pesa maana hakuna ajuae kuwa website italeta pesa au la bali alidai kuwa anataka uhalali ufanyike ili kuleta heshima.
Baba yao aliwaambia kuwa atawapatia mwanasheria ili aweze kufuatilia suala hilo. Tyler alipata ahueni kidogo kwani ndicho alichotaka, kwenda mbele ya sheria ili kuona ni nini kitafanyika

***
the facebook ilizidi kukua, karibu asilimia 85 ya wanafunzi walikuwa wamejiunga na facebook. Kila sehemu aliyopita, Mark alinyooshewa vidole na wengine kunong'onezana kuwa huyo ndie Mark, ilionekana kuwa kuwa maarufu lilikuwa ni suala ambalo haliepukiki, gazeti la chuo lilimwandika karibia kila wiki sambamba na kuchapisha picha yake huku mara kwa mara wakimfanyia interview, ni Mark pekee ndie alijulikana na sie Eduardo, Eduardo yeye aliona ni sawa tu kwani yeye alichotaka ni faida ya kampuni na sio umaarufu, mara kwa mara alimwambia Mark kuwa waanze kutafuta wawekezaji na watangazaji ili waeweze kutangaza katika website yao lakini Mark alikataa, alisisitiza kuwa bado hajaamua kuifanya thefacebook kuwa ya biashhara, Eduardo alizidi kusisitiza kuwa website iliwagharimu pesa kuiendesha hivyo walitakiwa waanze kuitafutia pesa haraka, bado Mark alikataa akisema kufanya hivyo ni mapema sana kwani kunaweza kuipoteza website yake

Mark alikuwa amepokea barua kutoka kwa Divya, Cameron na Tyler ikiwa ni barua iliyomshtaki Mark kwa kwenda kinyume na makubaliano ya kutengeneza website yao ndani ya muda muafaka na kweza kuwachelewesha na tena badala yake yeye kufungua website yake kwa kutumia wazo lao, hivyo wakamwamrisha Mark kuwa aifunge hiyo website ya thefacebook.com isiendelee kutumika tena, awaandikie statement ya kukubali kuwa amefanya makosa, na mambo mengine mengi walimweleza Mark huku wakimwambia kuwa akishindwa kufanya hivyo sheria na maadili vitafuata mkondo wake.
Eduardo alisoma barua hiyo ambapo aliogopa kwani alihisi pia inamhusu mana yeye pia alikuwa ni mmiliki wa thefacebook.com, lakini Mark alimweleza kuwa tayari ameshaandika barua ya kuelezea kila kitu na kuipeleka kwenye ofisi ya chuo ambako kina Tyler walikuwa wamepeleka malalamiko yao, Mark alijibu kuwa website yake haihusiani kwa vyovyote vile na website ya kina Winklevoss na kuwa alikuwa hajawafanyia kazi yoyote ile hivyo hajatumia code zozote zile kutoka kwenye website yao kutengeneza website yake, na kuwa malengo ya ya yeyekutengeneza website ile ni kusaidia jamii ya Harvard na sio kama walivyoeleza hapo mwanzo.Mark alieleza melezo mengi akijaribu kuweka vitu sawa walivyokuwa wanashindwa kumwelewa
Eduardo alipata ahueni kwa jinsi Mark alivyojielezea,ilikuwa ni concept kama mfano kuwa 'fundi selemala ajaribu kumfunga fundi selemala alietengeneza kiti cha aina nyingine, kuna maelfu ya viti vya aina mbalimbali, na hivyo yeye kutengeneza kiti cha aina moja haimpi ruksa ya kumiliki viti vya aina zote'
Kulikuwa na social network mbalimbali, karibia kila mtu aliekuwa anasoma compyuta science alikuwa anajaribu kutengeneza social network hivyo haimaanishi waanze kushtakiana eti kisa wana idea zinazofanana, Mark yeye aliona hicho ni kama kijembe ambacho mtu yeyote yule akifanikiwa lazima apigwe na kutishiwa hivyo hakuwa na wasiwasi wowote ule, Eduardo pia alijaribu kuondoa wasiswasi

Mark alisema thefacebook ipanuliwe ifike mpaka vyuo vingine, na kwa kuwa watumiaji walikuwa wanaongezeka kila siku Mark aliona kuwa hataweza kuhimili kufanya kazi peke yake hivyo alihitaji mtu wa kumsaidia, alimteua roommate wake alieitwa Dustin Moskovitz kuwa msaidizi wake kwa masuala ya kompyuta , akamchagua pia roommate wake mwingine aitwaye Chris Hughes kushughulika na mambo ya kuitangaza kampuni kwa kuwa alikuwa ni muongeaji zaidi kuzidi wao. Eduardo alijua kuwa Mark alikuwa ameshapanga mpaka kufikia kutangaza hivyo na siku zote ambavyo huamua iwe ndivyo huwa na hivyo basi Eduardo hakuona haja ya kubisha bali alikubaliana na kila kitu. Mark aliongeza kuwa Dustin atamiliki kampuni kwa asilimia 5, Chris yeye wataamua mbeleni kutokana na kiwango cha kazi atakachokuwa akikifanya na Eduardo atabaki na asilimia 30 zake na huku yeye akipunguza kiwango chake kwenda asilimia 65.

Walikubaliana kuwa hiyo itakuwa ni team ya watu wanne ambayo wataipeleka thefacebook 'next level' na kuwapa vyeo kuwa Dustin atakuwa mkuu wa programming na vice president wa kampuni, Chris atakuwa ni msemaji wa kampuni, Eduardo ataendelea kuwa CFO na huku yeye akisema atakuwa ni 'mwanzilishi, mmiliki, commander na adui wa nchi (Mark alikuwa ni mtu mwenye maneno ya kufurahisha)'

Screenshot (94).png


***

Sean Parker aliamka asubuhi akiwa hana uhakika ni wapi alilala siku hiyo, aliangaza angaza macho ili kuwezaa kujua ni chumba gani alikuwa amelala usiku wa kuamkia asubuhi hiyo lakini hakuweza kugundua

Sean Parker alipokuwa highschool aliweza kuweka historia ya kutengeneza website ya kushare nyimbo iliyoitwa 'Napster' ambayo ilibadilisha kwa kiasi kikubwa rekodi ya kiwanda cha muziki na kumfanya Sean Parker kuwa maarufu, Napster ilitumika bure ambapo ilifanya Sean Parker asiingize pesa nyingi na hivyo kampuni yake kuweza kufa, Sean Parker alikaa na kuja na wazo lingine yeye na rafiki zake wawili ambapo waliweza kutengeneza website iliyoitwa Plaxo, website ambayo ilihusika na kushare e-mail pamoja na contact informations mbalimbali, website ilianza kidogo kidogo na kisha kuwa kubwa yenye kuingiza mamilioni ya pesa na baada ya pale Sean Parker aliweza kufukuzwa katika kampuni hiyo aliyoianzisha yeye mwenyewe huku akipewa kashfa mbalimbali kama ya kujihusisha na madawa ya kulevya, kulewa na pia kukesha club usiku kucha ambapo kiuhalisia wa maisha yake haikuwa namna hiyo.
Sean Parker alikuwa akiishi nyumba ambayo iliyokuwa maeneo ya chuo kikuu cha Stanford, nyumba ambayo ilikuwa ndani ya nyumba iliyokuwa ikikaliwa na watoto wengi wa chuo kiasi kwamba Sean Parker alikuwa maarufu sana,kila mwanafunzi alimfahamu Sean Parker ingawa alikuwa hasomi chuoni pale na wala alikuwa hasomi chuo chochote kile, Sean Parker alikuwa ni mtu wa kawaida asie na pesa pamoja nakuwa alifanya mambo makubwa yaliyomfanya kuwa mtu maarufu na kwa wakati huo wa sasa hakuwa na chochote kile wala kazi aliyokuwa akiifanya.

Sean Parker aliamka na kusogelea laptop iliyokuwa mezani akitaka kufungua na kusoma emails zake, laptop tayari ilikuwa wazi online na juu ilionesha website ambayo mtu alieiwasha alikuwa akiitumia. Sean aliitazama website ile, alionekana kuvutiwa nayo na kustaajabu jinsi ilivyokuwa ya kuvutia, aliendelea kuperuzi kwa shauku akitaka kuelewa zaidi, aliona profiles, picha, sehemu ya meseji na vingine vingi ambapo alitambua kuwa hajawahi kuviona katika social network yoyote ile,
alisoma chini ya kurasa maandishi 'a mark Zuckerberg production' moja kwa moja alijua aliyeandika jina lile lazima atakuwa ndie alietengeneza website ile

Sean aliingia google na kusearch ambapo matokeo yalikuja kutokea katika chanzo kimoja cha 'Harvard Crimson' ambalo lilikuwa ni gazeti la chuo cha Harvard
Alisoma kuwa website ile iliitwa thefacebook ambayo imetengenezwa na mwanafunzi wa mwaka wa pili ndani ya wiki sita zilizopita na ndani ya siku chache wanafunzi karibia wote waliweza kujiunga na thefacebook, na mpaka hapo ilikuwa na watumiaji karibia elftano katika vyuo vingine ambavyo ni Columbia, Stanford na yale

Sean alisoma na kujisemea mwenyewe "Thefacebook." kwa nini isiwe tu "Facebook?" Sean hakupenda hiyo the iliyotangulia mbele ya Facebook ambayo ilimpatia kero kila alipotaja 'thefacebook'

Vitu vya aina hii ndivyo Sean ambavyo alipenda kuvifanya, aliona hii ni project mpya ambayo anatakiwa kuifukuzia, aliona amtafte Mark ili aone huyo Mark yupo vizuri kiasi gani mpaka kutengeneza hiyo site, moyoni mwake alitumainia kuwa kama mambo yataenda sawa kama yanavyoonekana ataweza kumsaidia huyu mtoto kuibadilisha Facebook na kuwa kitu kikubwa, kitu alichoona ni cha mabillion ya dollar
Amekwisha jaribu sehemu mbiili ,Napster na Plaxo, je inawezekana Facebook kuwa sehemu yake ya tatu?

ITAENDELEA....
 
[eQUOTE="Kichpox, post: 20147074, member: 417104"]Jarib kua na ufupisho mkuu
Kunywa pombe,kunyanyuka kusogelea
Story ndeeefu inachoshaaaaa siamin kama kuna pple zimeisoma yote kama ilivo
Mwisho

We mtu gani unatusumbua afu kukwoti uzi mzima afu unaandika upuuuzi (magu wewe)[/QUOTE]
 
Story poa sana aisee uvumilivu,watu wanachangamkia fursa umenikumbusha Harvard napamiss sana mwe.
 
Back
Top Bottom