The DaVinc code by Dan brown; Part 1

DAN LOKOMOTIVE

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
1,503
1,906
Salamu wana jamvi, leo nimeona niwaletee chapisho linaloelezea kitabu maarufu sana cha hadithi kinachojulikana kama’’The DaVinci Code”. Kitabu hiki nimekisoma hivi karibuni nikaona si vibaya kuleta hapa ili kujifunza. Kitabu hiki kilmeandikwa na mwandishi Dan Brown na kutolewa mwaka 2003. Sitaandika kitabu chote ila nitaandika ujumbe uliokusudiwa kufikishwa na mwandishi kwa wahusika. Katika chapisho hili nitatumia maneno baadhi ya kiingereza kwa sababu sifahamu maneno ya Kiswahili yatakayotoa maana sahihi na ujumbe uliotakiwa kuwafikia wasomaji. Kwa mujibu wa mwandishi wa hii hadithi ukiachilia mbali wahusika ambao ni wakutengeneza(fiction) viliyobaki vina ukweli 99%.

Tuanze kwa kuelewa kwanini mwandishi alikkipa jina hili “The DaVinci code”.Mwandishi alitaka kuonesha uwezo wa Leonardo DaVinci ambaye aliweza kutumia codes na alama mbalimbali katika michoro yake ili kuwasilisha ujumbe Fulani kwa watu watakaoweza kuzing’amua codes hizo. Kwa wale wasiomfahamu Leonard DaVinci huyu alikua moja kati ya wachoraji maarufu walioishi miaka hiyo pia utakua umeziona kazi zake kwa mfano mchoro maarufu wa mwanamke anaetabasamu unaoitwa “Monalisa” au mchoro wa maarufu wa karamu ya mwisho ya bwana Yesu akiwa na mitume wake “The last supper”.Pia “vitruvian man” na mingine mingi ilikua kazi ya bwana Leonardo DaVinci.

Simulizi inaanza kwa kumuelezea mhusika Robert Langdon ambaye alikua ni professor katika chuo cha Havard Marekani aliekua amejikita zaidi kaitka masuala ya Historia ya alama za kale zilizotumiwa kuwasilisha ujumbe fulani. Huyu Langdon alikua amealikwa kwenda mjini Paris (ufaransa) kufundisha masuala yayaohusiana na taaluma yake. Lakini kabla ya kwenda kufundisha anapokea ujumbe kwamba anahitajika kufika katika Louvre Museum. Basi Langdon ilibidi aahirishe kutoa lecture na kuelekea huko Louvre. Baada ya kufika hapa Langdon anapokelewa na askari wa uchunguzi anayeitwa Bezu Fache.

Askari huyu anamuongoza Langdon mpaka katika ofisi ya bwana Jacques Saunière. Huyu Jacques ni mhusika mwingine amabaye alikua ameuawa katika geti la Louvre lakini aliweza kujikokota hadi ofisini mwake amabako alipoteza maisha. Sasa Langdon akamuuliza afande Bezu nia na sababu ya yeye kumuita katika crime scene. Afande Bezu akaeleza kwamba kwa vile Langdon ni mtaalamu wa masuala ya alama labda anaweza kuelewa kilichotokea kwa sababu Jaques kabla ya kufariki alijichora mistari mitano ambayo inaonesha nyota katika mwili wake kwa kutumia damu yake lakini si hivyo tuu bwana Jacques alilala kifudifudi na kuchanua miguu yake na miguu akionesha moja kati ya alama za michoro ya Leonardo DaVinci.

Hapo mwanzo Afande Bezu alidhani Jacquese alikua mfuasi wa masuala ya kishetani ndio maana alijichora na kujitandaza namna ile. Ndipo bwana Langdon alipo muelezea maana ya hizi alama. Langdon akaeleza ile alama ilitumika miaka ya zamani 4000BC. Lakini afande Bezu akasema itakua ni alama ya kipagani. Langdon akamwambia alama pamoja na maneno yana maana nyingi mfano Klux Klax Klan ni kundi la wazungu liliokuwa la kueneza racism Marekani walikua wanavaa kama kanzu na hoods. Lakini katika Uhispania namna hii ya uvaaji lilikua kundi la kidini .Pia akamwelewesha Bezu hata neno “Pagan” linatokana na neno la kilatin “Paganus” likimaansha watu wa vijijini wasiofuata imani za mjini.

Langdon akaendelea hii alama inaitwa Pentacle hii ilikuwa ni nusu ya alama kwani watu wa zamani waliakua wakiamini katika masculine (gods) na feminine (goddess) maana waliamini katika miungu hii ambayo ilileta usawa kama ilivo Ying na yang. Sasa nyota waliamini ni nusu ya ukamilifu huu na ni kutokana na uonekanaji wa nyota ya Venus ambayo ni sayari hii ya Venus na wagiriki waliweza kuisoma na kugundua kila baada ya miaka mine inaonekana vizuri zaidi. Langodn akasema pia wagrirki walitengeneza ratiba yao ya michezo ijulikanayo kama “Olympaids” na hadi leo hii ni watu wachache wanafahamu kwamba ratiba ya Olympics inafuata mwendelezo wa hii Venus(goddess). Pia akaongeza kwamba ile alama ya michezo Olympics ambayo kwa sasa ni miduara mitano ilitokea huku kwenye hii idea. Lakini baadae ilibadilishwa

Langdon akamuambia hizi alama zilikatazwa na Kanisa pamoja Vatican baada ya ukristo kuingia duniani wakitaka kueneza ziaidi ukristo akamuambia pia alama hizi ndio utaziona kwenye mabegani mwa sare za maaskari mahali pengi duniani wakizitumia kama vyeo lakini maana yake ni “feminine goddess of love sexuality and protection” ya Venus. Bezu akazidi kushangaa akamuuliza tena kwanini huyu Jacques aliamua kuvua nguo na kujichanua namna hii kama Eagle. Langdon akamuambia hii alitaka kuonesha moja kati ya kazi ya Leonardo DaVinc ijulikanayo kama “Vitruvian man”. Hii ni alama ikimuonsha mwanaume asiyekua na nguo kachanua mikono na miguu. Afande Bezu akasema huyu Jacquese atakua na mambo ya kishetani kama aliokua Leonardo DaVinci.

Langdon akamulezea DaVinci kwamba ukiachilia mbali kuwa na kipaji na akili nyingi alikuwa na tabia za tofauti Mfano DaVinc alikuwa ana fukua miili ya maiti zilizozikwa ili ajifunze anatomy. Pia huyu DaVinci alikua anaandika mambo mengi amabayo watu walishindwa kuyaelewa mpaka akuelezee pia DaVinci alikuwa mtu anaeabudu Nature na alikuwa Homosexual. Ukiachilia mbali DaVinci alipewa madeal mengi ya kuchora na Kanisa lakini yeye alitumia hii nafasi kuchora alama na michoro inayoendana na imani ya kikriso japokua alikuwa anamaanisha vitu vingine tofauti na alichombiwa achore. Pia alijiaminisha anauwezo kugeuza madini ya Lead kuwa dhahabu.

Langdon anaendelea kusema DaVinci alivumbua mashine nyingi za kutesea na silaha ambazo zinge weza kuua watu wengi kwa wakati mmoja.Kwa mfano picha ya mwanamke inayojulikana sana kama “Monalisa” siyo ya mwanamke wala mwanaume ila ni muungano wao. Na pia DaVinci alitumia kufikisha ujumbe wa imani zake kupitia huu mchoro. Anaendelea kusema huu mchoro ulikua muungano wa moja feminine god wa misri ulioitwa AMON ambaye alimaanisha “"masculinitiy sexuality god” ambaye sanamu lake ilikua na kichwa cha mbuzi chenye mapembe marefu (horns)yaliyojikunja. Na ndio sababu ya kuzuka kwa msemo wa “HORN-Y” ikimaanisha ashki ya mapenzi.

Pia kwa upande wa pili DaVinci alitumia miungu kike goddesss alietiwa ISIS kama nusu ya pili ya imani yake ya ukamilifu wa goddess kwahiyo ukijumlisha haya maneno AMON na ISIS unapata.

AMONL'ISA

Ndio likapatikana jina la “‘monalisa”.Kwa hiyo hata haya majina ya monalisa origin yake ni hii miungu.goddess and gods. Analezea kwamba mchoro original haukuwa unaeleweka kama ni mwanamke au mwanaume ila DaVinci alimuwekea tabasamu kama dhihaka kwa wale ambao hawkuweza kuutambua,.
Itaendelea
 
Uwe unaandika kitu Kwanza kikishakamilika ndio upost, hii mambo itaendelea ndio nini sasa?
 
Back
Top Bottom