Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Tanzania itajengwa na watu wenye moyo. Elimu ni ufunguo wa Maisha. Akili ni nywele, kila mtu anazo. Elimu ni bahari, haina mwisho.
Tuna wasomi, lakini hawajaelimika- Ali Hassan Mwinyi 2008.
Kuna hali na hisia fulani iliyojengeka Tanzania hasa kutoka kundi la wasomi kuwa kutokana na usomi wao, basi wao wanapaswa kupewa kipaumbele na umuhimu hata kuhudumiwa kama mteja wa daraja la kwanza.
Dhana hii potofu haijaanza leo au jana, tumekuwa nyo tangu wakati tukiwa koloni la Muingereza mpaka leo hii.
The elite group of Tanzania carries itself as if they are entitled to special preference, special treatment and they are the only group that should be in power and enjoy the luxuries of the sweat and daily toil of everyone.
Kila mtu katika kundi hili, hujivunia unono wa Usomi na vyeti vyake mithili ya wanaotambiana ukubwa wa dhakari (ashakum si matusi) kuwa ni tija!
Najiuliza je tuwaenzi wasomi wetu kwa vyeti vyao na kuwapa vifuta jasho kwa kuhenyeka kwao walipokuwa wakisoma mpaka wakapata vyeti, au wapimwe matunda ya usomi wao kwa kuonyesha kuelimika na kufanya kazi ambazo zitang'ara na kuonekana bila kung'ang''ania kutambulikana kwa Usomi wao?
Miye Kihiyo, elimu yangu ni elimu dunia na si elimu cheti, je upeo wangu wa uelewa wa mambo ni batili mbele ya msomi mwenye cheti?
Je mpaka lini Tanzania iendelee kusubiri wasomi wake wageuze hivyo vyeti na majigambo yanayoambatana na kutaka kupata sifa na vyeo kutokana na usomi wao na si matunda ya kazi zao kutumia elimu walioipata/
Ukiangalia Serikali na hata Bunge letu, limejaa wasomi, watu wenye vyeti mpaka vya udakitari. Lakini ukiangalia ufanisi na hata uchapa kazi, ni heri wale waliosoma ngumbaru. Ukipima busara za maamuzi ya wasomi hawa, bora babu yako aliyeishia darasa la nne wakati wa mkoloni.
Hata katika mashirika, taasisi na hata vyuo, kudindiana kutokana na vyeti kunaonekana kuwa ni tija na sifa kubwa na si kugeuza kisomo hicho na kuelimika na kukifanyia kazi.
Mjoli wangu Zakumi kwenye ile hoja ya Nyerere, Ujamaa na Azimio anadai kuwa kila kitu kwenye maandishi kinaonekana bora, tatizo linakuja kwenye vitendo.
Je kaugonjwa haka nako kako katika tabaka la wasomi? Maana kila siku utasikia tunataka vyeo, tunataka mishahara mikubwa, mafao na masurufu kibao, kisa eti "tumesoma" na tuna vyeti kuthibitisha.
Ikiwa mpaka kesho tunachechemea kwa umasikini na hatuna hata uwezo wa kujenga vyoo, kuwa na akiba ya kutosha ya chakula au kutumia fedha zetu vizuri tunazopata kutokana na mapato finyu, kuna faida gani basi kuendelea kuwa na Wasomi au kuwatukuza?
Rais Lula da Silva wa Brazil, ni mtu wa kawaida, aliye na elimu sidhani hata kama imefikia chuo. Lakini pamoja na kutokuwa msomi, ni mtu aliyeelimika na mwenye hekima, busara na mchapa kazi.
Je ikiwa wasomi wetu wataacha kujitapatapa kuhusiana na Usomi wao na kuvua suti na tai na kuanza kuchapa kazi na kisha kubadilisha usomi wao na kuwa elimu bora inayolijenga Taifa, hatuoni kuwa tutaanza kupata maendeleo?
Je usomi au kuwa msomi kwa Tanzania ni chimbuko la kuwa na maarifa na kutumia juhudi katika kazi?
Tuna wasomi wengi sana, lakini bado hawajaelimika wala kuwa na uwezo wa kutumia Usomi wao kuelimika na kuongeza tija, ubunifu na ufanisi, vitu ambavyo ni muhimu ili kuongeza pato na kujenga msingi imara wa Taifa.
Kwa maoni yangu, ni mpaka pale tutakapoacha ile kitu wazungu wanasema "carrying ourselves with arrogance, pompousness and sense of entitlement" hatutakuwa na maendeleo na tutaendelea kugombea vyeo, madaraka na mishahara huku matunda ya usomi wetu na kazi zetu zikiwa ni sufuri.