The 10 poorest countries in the World


Ni kweli kuna mianya mingi ya ukwepaji kodi, pia kuna maeneo mengi yanayopaswa kutozwa kodi na pia kuna haja ya kupunguza misamaha ya kodi, serikali yetu kupitia TRA ikifanikiwa kuyadhibiti yote haya niliyoorodhesha, Tanzania itakuwa Dubai ya Afrika.

Lakini watanzania tuwe wawazi, Mhe. Kikwete alipoulizwa ni kwa nini watanzania ni maskini! akasema hajui sababu, kwa mwenye akili atajua maana ya Mhe. rais.

Mhe. rais alikuwa na maana ya kwamba, katika nchi ambayo kuna mianya mipana ya kutolipa kodi, kwanini wananchi hawatumi hii fursa katika soko lisilo rasmi ili kuzalisha mali? hiki ndicho kilimfanya Mhe. rais akose jibu.

TUZITAMBUE FURSA NA TUZITUMIE NDUGU ZANGU
 
Kweli mkuu,maisha ya mtanzania wa kawaida ni magumu sana,kuna tofauti kubwa kati ya Economic growth ana Economic development.
 

Una hakika?
 
Halafu kuna wapuuzi hapa Jukwaani hawaoni jitihada zinazofanywa na serikali ya CCM.

Kama jitihada gani? Hizi figurez zinasaidia nini ukiangalia na hali halisi ya mwananchi wa kawaida?
 
mkuu ungeweka sisi tupo wa wangapi ndio tungesema tunapiga hatua ila kwa hizo data hata mimi nimeangalia kwa nchi 195 zilizofanyiwa utafiti huo sisi tanzania tupo 170 kati ya 195 unataka kuniambia tupo katika hali nzuri tujisifie? so tukae kwenye viti virefu tusiongee siyo? maana tukiongea mnasema wanapiga tu kelele hawaoni hata maendeleo, kila kitu tunakiweka kwenye siasa, hata hivyo GDP ni kigezo kimojawapo tu cha kupima maendeleo na hatuwezi kugeneralize kuwa tuna maendeleo ya kutosha bila kuangalia sector mbali mbali za maendeleo, tupigeni kazi jamani
 
Tanzania ni tajiri tatizo ni ufisadi
 
Kwa hizo nchi ulizozitaja kwakweli hatustahili kuwepo!nadhani kwa GDP hata katika j
nchi 20 hatupo.Ingawa kipiko hiki kipo bias sana.
 
Per Capital Income ya TZ hadi last year ilikuwa around 500K usd how comes hatumo? Sikubaliani na hizo data
 

unategemea bajeti ya kilimo iwe kubwa kwa faida ya nani, kama wakulima wameacha kulima wamebakia kupiga porojo za CDM kama makasuku, mapori yanaongezeka, mjini wasanii nao wameongezeka, siku mkiamka na kuachana na siasa za DJ na kibabu, bajeti nayo itaongezeka
 
Per Capital Income ya TZ hadi last year ilikuwa around 500K usd how comes hatumo? Sikubaliani na hizo data

500K USD ndo maana yake nini?

500,000 USD Per Capita?
 
link naonyesha Tanzania ni ya 25 kwa umasikini duniani. kuna wakati tulikuwa kwenye 10 maskini. tumepga hatua. tuko kwenye mbio lakini kasi ni ndogo sana hata Zambia wako juu yetu, Kenya juu zaidi...
 
link naonyesha Tanzania ni ya 25 kwa umasikini duniani. kuna wakati tulikuwa kwenye 10 maskini. tumepga hatua. tuko kwenye mbio lakini kasi ni ndogo sana hata Zambia wako juu yetu, Kenya juu zaidi...

Huwezi kusema tumepiga hatua eti kwa sababu tulikuwa kwenye nchi 10 masikini kabisa na sasa tupo kwenye nchi 25 masikini kabisa.

Kwa sababu inawezekana tunazidi kuwa masikini (badala ya kutajirika) ila kuna wengine wanaozidi kuwa masikini kwa kasi kuliko sisi.

Chaguo kipimo kingine sio hiki cha kulinganisha na wengine bila kujua kiwango chetu wenyewe.
 
Dah,,,na mie nimeicheki kumbe Tz ni ya 26th from the poorest...

Source: The World

Mkuu kwa rasilimali ilizo nazo Tanzania ingeweza kuwa hata ya kwanza Afrika lakini tatizo ni kukosa uongozi bora!Hivi kenya wana rasilimali gani ya kutuzidi kiuchumi? Hii GDP ambayo baadhi yetu wanajivunia ni upuuzi tu maana katika hiyo asilimia kubwa ni mali za mafisadi maana ndiyo waliochukua lion share kwenye pato la taifa. It is 20/80 rule here yaani mafisadi wachache yaani only 20% wanachukua 80% ya pato la taifa na kuwaachia wananchi wengi yaani 80% wakigombania kile kiduchu kilichobaki yaani 20%. Kwa hiyo mtu akikokotoa GDP ya TAnzania itakuwa juu kiasi lakini nenda huko kijijini utakutana na wazee wamejaa vilaka kwenye matakoni mapaka vinaulizana wewe ulikuja lini bwana! Nchi njaa karibia maeneo yote kila mwaka! Kwa hiyo karibia asilimia kubwa ya watanzania hawana hata uwezo wakujilisha kwa mwaka halafu mtu anasema kila mtazania anaishi juu ya dola moja kwa siku! Shame on all of us especially our leaders! Tusipokuwa wazalendo na kukubali kuwa viongozi waliopo madarakani wametosha wawape na wengine wajaribu kuleta mawazo mapya basi tutabaki hapahapa mpaka Yesu anarudi! Tunahitaji mabadiliko makubwa hatakama kuna baadhi yetu tuliokuwatuna neemeka kwa njia za kifisadi tutapoteza lakini baadaye tutapata tena kwa njia ya haki na ndipo utajiri wa mtu utakuwa na maana!
 

Umepata stroke kichwani bila shaka...a normal human being cant contribute this way!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…