Thamani ya mke

Thamani ya mke

Asikuambie mtu kazi za nyumbani baada ya kutoka job yataka moyo. Hao wanaolalamika hautawakuta hata siku moja wakisaidia watoto na homework.

Kwa wiki mbili sasa msadizi kaenda likizo, nina watoto watatu chini ya miaka kumi na ajira juu. Hakuna rangi sioni nasubiri kwa hamu arudi nipumzike kidogo.
Ninakuelewa mama, ni shughuli asikuambie mtu.
 
Wee acha tu wanawake hua tunajiongeza sana
Otherwise siku nyingine inakua balaa
Halafu cha kushangaza hapo mchepuko anaeza letewa kila kitu
Wewe wifey unaambiwa siko vizuri ndo tunaamua kutumia akili ya ziada
Ni shetani tu.
 
jamaa nae kadata kipuuzi... angewabeba watoto wote kwenda kwa bibi yao halaf akaanza kuwatafutia maswala ya shule.. mbona tatizo dogo tu hilo..!!!
 
Hapo hapo kuna watoto wawili wa wifi umeambiwa watakaa mpaka wamalize shule, unaona kabisa mkate hautoshi asubuhi, inabidi ukirudi kazini uumue unga wa maandazi na hulali mpaka uyakaange ili watoto wanywe chai.
Umeongea/umeandika kwa hisia sana.
 
Wanawake tuna roho ya kipekee sana
Hawa viumbe hawa wanahitaji uvumilivu wa hali ya juu
Kuna vitu vingine vidogo tu mwanaume hawezi kufanya mpaka akuite wewe mwanamke ambae umetingwa na majukumu uje ukifanye
Mungu awabariki wanaume wanaojali wake na familia zao kwakweli
Amen.....

asiione Shunie
 
Back
Top Bottom