Thamani mojawapo kuu ya dini ni tumaini la faraja angalau baada ya maisha mateso ya hapa duniani

Thamani mojawapo kuu ya dini ni tumaini la faraja angalau baada ya maisha mateso ya hapa duniani

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,242
Reaction score
90,300
Kuna watu wanateseka sana kwenye hii dunia, wengine wanateseka tangu wanazaliwa mpaka wanakufa, wengine wanateseka nusu ya maisha yao yote n.k

Fikiria watu wanaugua kansa za kila aina, watu wanapata ajali wanabaki vilema wasiojiweza maisha yao yote, watu wanafungwa maisha au miaka mingi pasipo kuwa wametenda kosa lolote, watu masikini wanaoishi maisha yao yote wakiwa hawajui hata mlo unaofuata utatoka wapi n.k

Hawa na wengine wote wa aina hii uwaambie hakuna Mungu na dini ni kitu cha kutunga tu kisicho na uhalisia wowote watakuelewa kweli?

Yani baada ya haya mateso yao yote hata kama waliishi maisha mema kiasi gani wakifa ndio imeisha tu hivyo hakuna kitakachoendelea huko mbele, hakika sio rahisi kwa jambo hilo kueleweka au kukubalika. Linapoteza maana na matumaini ya kuishi kabisa.

Dini inawapa binadamu wengi tumaini kwamba mateso yao wanayopitoa angalau sio bure tu.
 
Back
Top Bottom