Thadei Ole Mushi: Ukuta wa Mirerani unavyomkera jirani

Thadei Ole Mushi: Ukuta wa Mirerani unavyomkera jirani

UKUTA WA MERERANI UNAVYOMKERA JIRANI.

Na Thadei Ole Mushi.

Leo Saniniu Laizer anauza Tena Jiwe la Mabilioni ya shilingi, wakati haya yakiendelea hapa Simanjiro Kuna nchi nyingine zinanuna. Jiwe la leo lina uzito wa kilo 6.63

Twende sawa!!!

Mwaka 2014 Nchi za Kenya na India ziliipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.

Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo , Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa mwaka 2013, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kamishna Masanja alisema mwaka 2013 pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

"Katika kipindi hicho cha mwaka Cha mwaka 2013, India iliuza tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India," alisema Masanja.

Bila kumtaja jina, Kamishna huyo alisema mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka nchini Marekani aliwahi kumuuliza iwapo kuna migodi ya tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Mwaka 2016 Marc Nkwame, Mwandishi Tanzania Daily News aliripoti kuwa Kenya iliuza tena madini ya Tanzanite njee ya mipaka yake yenye Thamani ya Dola milioni Mia Moja huku India ikifikia dola milioni 300 na Tanzania ambaye ndiye mwenye machimbo akiuza madini ya Dola million thelathini na nane tu.

Ujenzi wa ukuta wa MERERANI umekuwa shubiri kwa Kenya na India Kwani sasa wamebaki wakitizama show ya uuzaji wa madini moja kwa moja pale Merereni na Tanzania Sasa ndio inayoongoza kwa uuazaji wa madini haya ndani na nje ya nchi fuatilia link ifuatayo kuona yaliyokuwa yakiendelee kwenye sector ya madini.

Efforts to curb tanzanite smuggling make Tanzania shine - ENACT Africa

Huenda yaliwahi kupatikana mawe Mengine Makubwa zaidi ya haya lakini yalikuwa hayaonekani na Wala yalikuwa hayaliingizii Taifa kipato. Mtaelewa tu kwa nini Kuna vuguvugu Kati yetu na Jirani.

Tanzania haiwezi kufanywa Kama Congo kamwe.

Ole Mushi
0712702602
FB_IMG_1596467668295.jpeg
 
Hapaa kweli inawezekanaa kabisaa aiseee...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Majamaa yamemind sanaa
 
Kitu cha kusikitisha jiulize nchi hii imeliwa kiasi gani kutokana na 1. Makanikia 2. Nyara za serikali Twiga, Pembe za Tembo, Kifaru, ngozi za Punda milia, Pembe za Nyati Ngozi, meno, kucha, vichwa vya Simba na Chui, Mikia ya Tembo, Ngozi za Mamba, meno ya Kiboko, mavi ya Tembo, Tausi na Kanga vitu vyote hivi vimeuzwa nje ya nchi miaka yote toka Tanganyika iumbwe bila kusahau Almasi, dhahabu na mawe mengine ndio maana Rais alisema nchi hii ni tajiri lakini watu hawamuelewi. Tumsaidie Rais kudhibiti hizi mali hakika fedha nyingi itapatikana na mishahara itapanda na ajira itaongezeka kwani fedha za kujenga viwanda hata vinu vya nyuklia zitakuwepo.
 
Siku Mjomba Magu akiondoka kwenye madaraka siku hiyo Kenya itasherekea.Nimesema hili kwa kuwa Magufuli anachukia kuibiwa raslimali za taifa.
Mungu akimjaalia umri mrefu hata akiwa nje ya system moja kwa moja usifikiri Magufuli atakubali aingie mtu pimbi baada yake,lazima ang'ang'ane apatikane mtu atakaeweza kuziishi falsafa zake na aende mbali zaidi aweze hata kuwa mshauri wake.

Ukiangalia jinsi alivyoweza kuwa-limit wanachama wa chama chake ni wazi itawezekana kuchaguliwa mtu kama rais ila ikawa imezingatiwa kukamilisha kile inachotaka katiba but nguvu bado ikawa inatoka kwa Mjomba mkubwa.

Na hii nchi yetu ilivyo kila mtu ana njaa mie natamani iwe hivyo tu,Magufuli ana kasoro zake kama kiongozi ila ukikaa chini hata kama ni mpinzani ukafikiria nje ya box...huyu mzee ni mfano wa kiongozi hilo siyo la kubeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu akimjaalia umri mrefu hata akiwa nje ya system moja kwa moja usifikiri Magufuli atakubali aingie mtu pimbi baada yake,lazima ang'ang'ane apatikane mtu atakaeweza kuziishi falsafa zake na aende mbali zaidi aweze hata kuwa mshauri wake.

Ukiangalia jinsi alivyoweza kuwa-limit wanachama wa chama chake ni wazi itawezekana kuchaguliwa mtu kama rais ila ikawa imezingatiwa kukamilisha kile inachotaka katiba but nguvu bado ikawa inatoka kwa Mjomba mkubwa.

Na hii nchi yetu ilivyo kila mtu ana njaa mie natamani iwe hivyo tu,Magufuli ana kasoro zake kama kiongozi ila ukikaa chini hata kama ni mpinzani ukafikiria nje ya box...huyu mzee ni mfano wa kiongozi hilo siyo la kubeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna kazi kubwa sana ya kumpata Raisi mfuatiliaji kama Mjomba Magu.Anayo mambo mengi kichwani sijui kama ataweza kumaliza hata robo yake.
 
Nashindwa kuelewa uwelewa wako kama hata umepitia darasa la kwanza!

Unafananisha Tanzanite na kilimo cha mahindi kweli?ile ni tunu ya Taifa duniani zaidi ya lile eneo pale Mirerani lisilozidi 8 kilometers hakuna pengine utakapokutana na hiki kitu hivyo lazima kiheshimike,fungua akili hiyo.nyang'au Wakenya wanatudharau Watanzania kwa sababu ya watu wenye akili kama zako,ufananishe mahindi na dhahabu halafu uonekane una akili si wendawazimu huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado swala la bidhaa za kilimo pia tunapigwa sana. Mfano ni parachichi linalochukuliwa hapa nchini na kuwa packed nchini Kenya. Yakifika London yanauzwa zaidi ya dola 2 kwa moja na inaaminika yanalimwa Kenya.
 
Madini hayanunuliwa tu kwa ukubwa bali pia kwa jinsi yalivyokatwa. Ndio maana ingawa almasi nyingi zinapatikana Botswana na Afrika Kusini, soko kubwa la almasi duniani liko Antwerp Ubelgiji. Huko ndiko wakataji wazuri wa almasi walipo na bila shaka wanauza na kusafirisha almasi zaidi ya Botswana na Afrika Kusini. Hivyo hivyo kwa Tanzanite. Kenya na hasa India wana uwezo mkubwa zaidi wa kukata na kupolish tanzanite na kuongeza value yake wakati sisi tumebaki kuuza kwa kilo.

Amandla....
 
Madini hayanunuliwa tu kwa ukubwa bali pia kwa jinsi yalivyokatwa. Ndio maana ingawa almasi nyingi zinapatikana Botswana na Afrika Kusini, soko kubwa la almasi duniani liko Antwerp Ubelgiji. Huko ndiko wakataji wazuri wa almasi walipo na bila shaka wanauza na kusafirisha almasi zaidi ya Botswana na Afrika Kusini. Hivyo hivyo kwa Tanzanite. Kenya na hasa India wana uwezo mkubwa zaidi wa kukata na kupolish tanzanite na kuongeza value yake wakati sisi tumebaki kuuza kwa kilo.

Amandla....

Nchi moja haiwezi kucontrol chain nzima ya biashara ya madini.

Wenye monopoly ya ukataji lazima watapata pesa nyingi zaidi kuliko nchi inayoproduce raw
 
Kuna mtu alikuwa Waziri wa madini, Waziri wa fedha, Waziri wa mambo ya nje miaka 10, Rais miaka 10. Lakini hakuona au hakujiuliza au haikumuumiza kichwa kwamba Tanzania sio nchi ya kwanza duniani kuuza Tanzanite wakati Tanzanite yote duniani inatoka Tanzania. Sijui leo hii anatapaje usingizi usiku.

Kuna wakati dhamira ya mtu ni muhimu kuliko experience kwenye ufanisi wa kazi.
 
Well said
Baba J anatuonyesha namna gani kiongozi wa nchi anatakiwa awe.

Msimamo l Weledi l Umakini

Go Baba J Go Bana we are all supporting you...

Jirani bado anaajira nyingi sana nchini term ya pili angalia namna gani tunavyoweza kuwaondoa;

1. Walimu wa hizi English Medium
2. Advertising Agencies
3. Managers wa Mahotel
4. CEO wa makampuni
5. Wawekezaji uchwara
 
Kwakwel Muheshimiwa Magufuli anaeleweka, Mungu amtunze akili yenye ubunifu na uchungu kwa Taifa letu iendelee kumkaa, kama awamu nyingine zimepita nyuma lkn hawakuyaona haya basi ni muda wa kumshukuru Mungu, majirani wabaya ni kuangalia mikakati mizuri tu ya namna ya kuzuia hujuma dhidi yao, yafaa tuwekeze vzuri katika intelijensia za aina zote.
 
JPM Ana akili kuubwa saana huyu mtu..Huwa ninajiuliza,hao watawLa wa awamu zilizotangulia ukimuondoa NYERERE,hawakupata akili hata chembe ya jinsi ya kuthibiti madini yetu yasitoroshwe ? JPM Amewaumbua.JPM Ana IQ Kuubwa Sana jamani.
Miaka mi-5 TU LAKINI ameperform wonders reli ya mwendo Kasi,umeme mkubwa Huko mto Rufiji,Ikulu na serikali yoote kahamishia Dodoma(KITU kilichowashinda watangulizi wake woote wa awamu 3 zilizomtangulia),Barabara za juu(Flyovers),Kathibiti Sana wizi wa madini yetu n.k.MAMBO NI MENGI MNO AMEFANYA kwa muda mfupi.MUNGU AMBARIKI Kwa kweli.
 
Back
Top Bottom