Thadei Ole Mushi: Ukuta wa Mirerani unavyomkera jirani

Thadei Ole Mushi: Ukuta wa Mirerani unavyomkera jirani

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
710
Reaction score
1,365
UKUTA WA MERERANI UNAVYOMKERA JIRANI.

Leo Saniniu Laizer anauza Tena Jiwe la Mabilioni ya shilingi, wakati haya yakiendelea hapa Simanjiro Kuna nchi nyingine zinanuna. Jiwe la leo lina uzito wa kilo 6.63

Twende sawa!

Mwaka 2014 Nchi za Kenya na India ziliipita kwa mbali Tanzania kwa kusafirisha na kuuza katika soko la dunia, madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana hapa nchini pekee.

Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini kwa wakati huo , Mhandisi Paul Masanja aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa mwaka 2013, Tanzania haikufikia hata nusu ya Kenya kwa mauzo ya madini hayo ya vito.

Kamishna Masanja alisema mwaka 2013 pekee, Kenya ilisafirisha na kuuza nje ya nchi tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Dola 100 milioni za Marekani (Sh173 bilioni) dhidi ya Dola 38 milioni (Sh45.5 bilioni) zilizouzwa na Tanzania.

"Katika kipindi hicho cha mwaka Cha mwaka 2013, India iliuza Tanzanite zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani 300 milioni (Sh509 bilioni) kiasi cha baadhi ya wanunuzi wakubwa, hasa kutoka Marekani kujiuliza iwapo madini hayo yanachimbwa India," alisema Masanja.

Bila kumtaja jina, Kamishna huyo alisema mmoja wa wanunuzi wakubwa wa madini ya vito kutoka nchini Marekani aliwahi kumuuliza iwapo kuna migodi ya tanzanite India kwa sababu akifika huko hupata tanzanite bora na zenye ukubwa kuliko anayopata Tanzania.

Mwaka 2016 Marc Nkwame, Mwandishi Tanzania Daily News aliripoti kuwa Kenya iliuza tena madini ya Tanzanite njee ya mipaka yake yenye Thamani ya Dola milioni Mia Moja huku India ikifikia dola milioni 300 na Tanzania ambaye ndiye mwenye machimbo akiuza madini ya Dola million thelathini na nane tu.

Ujenzi wa ukuta wa MERERANI umekuwa shubiri kwa Kenya na India Kwani sasa wamebaki wakitizama show ya uuzaji wa madini moja kwa moja pale Merereni na Tanzania Sasa ndio inayoongoza kwa uuazaji wa madini haya ndani na nje ya nchi fuatilia link ifuatayo kuona yaliyokuwa yakiendelee kwenye sector ya madini.

Efforts to curb tanzanite smuggling make Tanzania shine - ENACT Africa

Huenda yaliwahi kupatikana mawe Mengine Makubwa zaidi ya haya lakini yalikuwa hayaonekani na Wala yalikuwa hayaliingizii Taifa kipato. Mtaelewa tu kwa nini Kuna vuguvugu Kati yetu na Jirani.

Tanzania haiwezi kufanywa Kama Congo kamwe.

Ole Mushi
0712702602
 
Kati ya mambo ya msingi yanayompa Rais Magufuli kongole nyingi, ni hili la usimamizi bora kabisa wa sekta ya madini, na hata ufanisi ktk mafanikio yake yanaonekana wazi kabisa. Katika hili anastahili sifa za pekee.
 
Hii ya madini imekaa kizalendo sana, JPM ni bonge la kiongozi, ni hivi tu vijimambo mambo vyake vya chuki na udikteta vinavyowakera wengi. Haya yote anaweza kuyafanya bila kuminya haki za wengine
No chochote unachokiona kinafanyika ujue hakifanyiki kwa bahati mbaya. Yawezekana mfano hiyo taarifa hapo ulikuwa huijui na uliona watu walivyobeza ujenzi wa ukuta..ila serikali ilijua na inawafahamu waliokuwa wanafanya ujinga ambao leo usipokuwa mbabe na katili watakushinda. Maana kumbuka kuna nchi zilikuwa zinawaback up.
 
Kati ya mambo ya msingi yanayompa Rais Magufuli kongole nyingi, ni hili la usimamizi bora kabisa wa sekta ya madini, na hata ufanisi ktk mafanikio yake yanaonekana wazi kabisa. Katika hili anastahili sifa za pekee.
Siku Mjomba Magu akiondoka kwenye madaraka siku hiyo Kenya itasherekea.Nimesema hili kwa kuwa Magufuli anachukia kuibiwa raslimali za taifa.
 
Baba J anatuonyesha namna gani kiongozi wa nchi anatakiwa awe.

Msimamo l Weledi l Umakini

Go Baba J Go Bana we are all supporting you...

Jirani bado anaajira nyingi sana nchini term ya pili angalia namna gani tunavyoweza kuwaondoa;

1. Walimu wa hizi English Medium
2. Advertising Agencies
3. Managers wa Mahotel
4. CEO wa makampuni
5. Wawekezaji uchwara
 
Baba J anatuonyesha namna gani kiongozi wa nchi anatakiwa awe.

Msimamo l Weledi l Umakini

Go Baba J Go Bana we are all supporting you...

Jirani bado anaajira nyingi sana nchini term ya pili angalia namna gani tunavyoweza kuwaondoa;

1. Walimu wa hizi English Medium
2. Advertising Agencies
3. Managers wa Mahotel
4. CEO wa makampuni
5. Wawekezaji uchwara
Walimu na Afya sio kwa sekta binafsi, wapo serikalini pia yaani wana cheki namba kabisa na wanaongoza kwa kutukana watanzania kuwa ni wajinga!
 
Hili pia linanifanya mimi binafsi nimrafutie JPM kura milioni 3 bila kujali Wazalendo wengine watamtafutia ngapi
We mwenyewe huwezi kujitafutia hata kura 3 katikati ya wajumbe wa ccm kwenye kura za maoni za ubunge, unategemea mbeleko ya viti maalumu, halafu uwe na uwezo wa kumtafutia JPM kura millioni 3?

Sifa za kijinga a.k.a kujipendekeza ili akuone tena akuteuwe!
 
Juzi alipokuwa akihutubia wananchi Morogoro kwenye hafla ya uwekaji mawe ya msingi mahandaki ya sgr alichomekea kauli kwamba light ule ukuta ungejengwa tangu mwaka 1965 tngekua tumefikia wapi saivi,mi tangu siku ile ndo nimemuelewa mazima
 
Kwa hayo Hongera Rais wetu. La pili ukifanikiwa kufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa huru na wa haki bila vyama kuibiana kura utapata bonge ya sifa. Ninakutakia kila heri kwa kipindi chako cha pili na kuna uwezekano pia kama kijani wakiwa wengi wakakuomba kuendelea na ngwe nyingine.
 
juzi alipojkua akihutubia wananchi morogorokwenye hafla ya uwekaji mawe ya msingi mahandaki ya sgr alichomekea kauli kwamba light ule ukuta ungejengwa tangu mwaka 1965 tngekua tumefikia wapi saivi,mi tangu siku ile ndo nimemuelewa mazima
Wengi Wana muelewa Ila wanajitoa fahamu
 
Back
Top Bottom