Thadei Kweka aachiwa huru

Thadei Kweka aachiwa huru

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,656
Taarifa ya hivi punde...

Mmarekani mwenye asili ya Tanzania ambaye alikamatwa huko Kilimanjaro kwa ‘maagizo toka juu’, ameachiwa huru jioni ya leo.

Screenshot_20260103_173104_WhatsApp.jpg


KWA KINA:

Thadei Kweka ameachiwa huru leo January 3, 2026 baada ya kushikiliwa Polisi kwa siku 6 kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kupitia group la "What sup".

Thadei ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Tanzania alikamatwa December 28, 2025 usiku na kushikiliwa kituo kikuu cha Polisi (Central) Moshi. December 31, 2025 alipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kupewa AMRI ya kutoa password ya simu yake ili polisi waweze kupekua hilo group la "What sup" alikokuwa akifanya uchochezi.

Hata hivyo Thadei alisema hatambui "What sup" ni kitu gani na hana application ya aina hiyo kwenye simu yake. Pia alisema kutokana na unyanyasaji aliofanyiwa na polisi, alipoteza kumbukumbu ya mambo yake mengi ikiwemo password ya simu yake.

Ubalozi wa Marekani ulituma fomu maalumu (Consular Notification and Access Form) ambayo Thadei alitakiwa kusaini ili Serikali ya Marekani iweze kuwa "involved" kwenye kesi yake. Ni kawaida Marekani kufuatilia kesi yoyote inayohusu raia wake. Lakini polisi walikataa asisaini.

Jana Mawakili wa Thadei wali-file "Habeas corpus" ili kuwalazimisha Polisi wamfikishe mahakamani. Pia Ubalozi wa Marekani ukataka kujua kwanini Thadei hajasaini "Consular Notification and Access Form" ili waweze kufuatilia kesi yake. Haraka sana Tahdei akapewa fomu ya ubalozi akasaini jana, na leo ameachiwa huru
 
Taarifa ya hivi punde...

Mmarekani mwenye asili ya Tanzania ambaye alikamatwa huko Kilimanjaro kwa maagizo ya Samia, ameachiwa huru jioni ya leo.

Taarifa zaidi zitawajia kuhusu details za kuachiwa kwake huru
View attachment 3524678
Kiukweli kuwa raia wa nchi zinazojitambua, it's a very big deal,
US passport imemuokoa, bila hivyo, saa hizi...zamaani!.
Bwana asifiwe

P
 
Kiukweli kuwa raia wa nchi zinazojitambua, it's a very big deal,
US passport imemuokoa, bila hivyo, saa hizi...zamaani!.
Bwana asifiwe

P
Kaka yangu Paskali.
Je unaichukuliaje taarifa hii?

Kwa nini passport ya Marekani imsaidie Kweka ilihali tuna Katiba bora yenye Bill of Right?
Tutafakari pamoja
 
Taarifa ya hivi punde...

Mmarekani mwenye asili ya Tanzania ambaye alikamatwa huko Kilimanjaro kwa maagizo ya Samia, ameachiwa huru jioni ya leo.

Taarifa zaidi zitawajia kuhusu details za kuachiwa kwake huru
View attachment 3524678
Bila kuwa Mmarekani angepotezwa tu kama Polepole, Mdude, nk. Samuya na genge lake wameona huo mfupa hata Fisi hauwezi, itawatokea puani
 
Back
Top Bottom