Tgif - end of the month -pay day | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tgif - end of the month -pay day

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Mar 26, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Wakuu

  Thanks God is Friday - I got my salary today.
  i) kwa hiyo nina uhakika wa kulipa madeni ya mwezi huu kwa mangi ili nianze kukopa tena ya mwezi ujao
  ii) Naweza kutoka kula kitimoto na washikaji jioni sababu uchakavu ninao mfukoni
  iii) Nina uhakika kwa kwenda kwenye Kihamba changu kesho nikaone nini naweza kukifanya kule - hata kama kununua mifuko miwili ya sementi kuvuta ujenzi wa kibanda
  iv) Nitaweza kumtumia mzazi wangu walau kiasi kidogo ajikimu kwa mwezi ujao
  v) Nimepanga kuitoa familia yangu sunday - walau mara moja kwa mwezi si mbaya - hata pale Rose garden tu waone bongo inaendaje endaje
  vi) Kodi ya nyumba ya Mwaka natakiwa niwe nimeilipa mwezi ujao - duh
  vii) Umeme & Maji vinanisubiria

  Wakuu, Kwa mgawanyo huu hapo juu basi mshahara wangu umeshaisha - by Jtatu i will be broke again - sasa sijui haya maisha mpaka lini? Nikiangalia pay slip yangu hii sehemu ya PAYE - inanichefua kabisa.

  Sipati picha nikizingatia PASAKA inawadia natakiwa walau kubadili menyu ya familia yangu siku hiyo walau wapate pilau na soda.- aisee hii kweli Bongo Dyaslamu --Bila kutumia ubongo wafwaaa.....
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  inabd ujiunge na wajasiriamali, mi nimepanga kujiunga mwezi ujao hapa ndo na pambanua mradi
   
 3. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nilisahau kuwa wewe umeanza kulima, ucjali kabisa maisha haya ya ukapa yana mwisho mavuno ya kija utasave nyingi kwa ajili ya mwaka wote unaokuja hakuna kukopa kwa mangi tena,
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako ELNINO,

  Vipi ule mradi wa kilimo hapa sijaona mahali umeutaja au umehairisha.
   
Loading...