TFF wazembe wanakubali CAF kupangia muda mbovu

NguoYaSikuKuu

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
595
712
TFF wamekua wazembe sana kwenye suala la muda wa mechi za TAIFA stars. Hii ni mechi ya pili wanapangiwa muda mbovu na CAF wanakubali bila hata kuhoji.

Mechi saa nne usiku ni rafiki kweli kwa nchi yetu na usafiri wa Dar Es Salam? Hawaoni kuwa sio rafiki kwa mashabiki na kwa ushangiliaji wa mechi husika,

Nimeishi South Africa na sijawahi kuona wanapangiwa muda mbovu. Mechi zao zote za timu yao ya Taifa zinapangwa muda rafiki na nchi yao. Je, Karia anaogopa watu wa CAF ?

TFF mbadilike katika hili.
 
Inawezekana ndiyo muda tuliotaka sisi ili wachezaji wapate muda zaidi wa kupumzika maana wametoka tu kucheza game na Niger. Nadhani ndiyo sababu kubwa. Sidhani kama kujaza uwanja ni kipaumbele sana kwetu.
 
Inawezekana ndiyo muda tuliotaka sisi ili wachezaji wapate muda zaidi wa kupumzika maana wametoka tu kucheza game na Niger. Nadhani ndiyo sababu kubwa. Sidhani kama kujaza uwanja ni kipaumbele sana kwetu.
Sio kweli , CAF ndo wamepanga.
 
Sio kweli , CAF ndo wamepanga.
Ninavyojua mimi CAF wanampa timu mwenyeji options za muda, unachofanya ni kuchagua muda huo na kuwataarifu. Kuchezwa masaa ya mbele kumewapa wachezaji wa TZ masaa kadhaa zaidi ya kupumzika ingawa nadhani kibaridi cha usiku wa saa 4 ni faida zaidi kwa Morocco.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom