TFF uone umuhimu wa kusameheana na Michael Wambura kwa maendeleo ya soka

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
681
825
Miongoni mwa wadau wenye mchango mkubwa ktk kusukuma maendeleo ya soka hapa nchini ni pamoja na mwamba Michael Wambura.

Huyu amechangia Sana muda wake, uwezo wake wa mali na maarifa katika kulifanya soka la nchi hii kupiga hatua mbele akiwa ktk nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu, ngazi nyingine za juu za vyama vya mpira na FAT ambayo Ndiyo TFF ya sasa.

Ni kweli yawezekana kuwa aliwahi kuwa na mapungufu ya kibinadamu ktk mchakato wa kutafuta maendeleo ya soka kwa maana ya misigano na tofauti za namna ya kufikia malengo ya soka. Katika hili TFF waione kama sehemu ya nia njema kabisa kwa Wambura na kwetu sote watanzania tulikuwa na nia njema ya maendeleo ya soka, hivyo basi kwa muktadha huu TFF isamehe sasa na wamruhusu kushiriki mambo ya soka kwa maendeleo ya soka letu.

Watanzania bado tunaamini kuwa Michael Wambura bado anao mchango mkubwa wa mawazo chanya na jitihada thabiti za kuweza kushirikiana nasi ktk kipindi hiki.

TFF ni muda sasa wa kuachana na visasi bali tusameheane na sote tuunganishe nguvu na mawazo kuliendeleza soka.
 
Siku Wallace Karia akitoka tu kwenye nafasi ya urais wa TFF, basi siku inayofuata huyo Michael Wambura atakuwa huru.
 
Kilichomtuma aende mahakamani kwa masuala ya soka ndicho kilichomfuta,fifa wameshafanya atulie aendelee na michezo mingine,nashauri ahamie kwenye netball kutamfaa zaidi
 
Hivi kweli katika Tanzania ya watu mil 67 hakuna watu watakaoleta maendeleo ya soka mpaka na Wambura awepo,acha utani mwanzisha uzi
 
Back
Top Bottom