Ombi kwa shirikisho la soka Tanzania (TFF)

vibertz

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
1,358
2,497
TFF tunaomba mfikirie umuhimu wa mashindano, ubora wa mashindano na vipaumbele vya mashindano. Kwasasa timu ya Simba na Yanga zina mechi muhimu sana ya klabu bingwa hatua ya robo fainali na inachezwa tarehe kati ya tarehe 29 na 30 mwezi huu. Lakini nimeshangazwa na kutaka kuwatumia wachezaji muhimu wa Simba na Yanga kwenye bonanza la FIFA series ambayo itachezwa tarehe 25 huko Azerbaijan.

Hivi kweli mmeshindwa kutafakari kuona umuhimu wa timu zetu za Tanzania kufanya vyema kwenye klabu bingwa kiasa kwamba hamkuona haya ya kuwaachia wachezaji wao waendelee na program za makocha wao kujiandaa na mechi ya klabu bingwa zilizopo mbele yao?

Yaani hili nalo ni mpaka mfundishwe? Au mnataka vilabu visiwe vinatoa ruhusa kwa wachezaji wao muhimu?

Kuna umuhimu wa viongozi wa Simba na Yanga kukaa chini na TFF kuomba kubakishiwa wachezaji wote waendelee na program za maandalizi ya mechi ya klabu bingwa na isitoshe katika wachezaji wataochukuliwa ni kutoka Tanzania pekee kwavile mataifa mengine yanatoka hawa wachezaji wa Simba na Yanga hayapo kwenye hili bonanza
 
Michuano hio itatumika kwa ajiili ya maandalizi ya team kwa ajiili ya michuano ya kufuzu Afcon, na most important kwa ajiili ya kutangaza wachezaji wetu nje
 
Acheni uzwazwa.....hzo ndo akili zenu haya matimu yenu yakiwaga na mechi za kimataifa yanasimamisha mechi za ligi kwa wiki 2 kabisaa eti yanajiandaaa......Kwani huko Azerbaijan wanaenda kufanya nini si kucheza mpira????
 
Wachezaji wanaocheza klabu bingwa wanayo platform ya kujitangaza tayari, kama lengo ni wachezaji kujitangaza basi waende wasiokuwa na mashindano ya kujitangaza
 
Wangetoa nafasi kwa wachezaji wapya waliokosa nafasi AFCON waone uwezo wao sasa unawapeleka Manula, Msuva, Zimbwe, Kennedy kutafta nini?
 
Wachezaji wanaocheza klabu bingwa wanayo platform ya kujitangaza tayari, kama lengo ni wachezaji kujitangaza basi waende wasiokuwa na mashindano ya kujitangaza
Hujitangazi sehemu moja, unajitangaza kila mahali,
Ndio mana unao makampuni yanajitangaza kila yanapopata nafasi, sio kukomaa na CL tu,
Halafu mzee hao wachezaji wakicheza stars watavunjika ? Acheni kudeka dadeq
 
afu Hajui kama FIFA inamtangaza mchezaji Globaly iyo CAF champions leauge asimilia kubwa watazamaji wake ni wa hapa hapa Africa na jicho la ma agent wengi huwalinatua kwenye Michuano ya FIFA na vijana sana
 
Unaongelea mambo ya kizamani siku hizi scouts wanafatilia mchezaji hata kwenye mechi za ligi yaani mchezaji amewika mechi moja ya timu ya taifa unabeba?
 
wew Nani alikwambia ili uone ubora wa mchezaji ni lazima acheze mechi 200 ndio utagundua ubora wake kuna wachezaji wengi tu Duniani apa wamesajiliwa kwa bonaza la siku moja mfano Antonio Valencia alisajiliwa kwa kucheza kwenye bonaza lilofanyika siku moja tu Na watu wakaona kipaji chake ,Yule Dogo Mohhamed Muntari alichezea timu ya Taifa ya Qatar kombe la 2022 alisajiliwa kwenye bonaza lilofanyika Ghana tena siku moja tu

Afu kwa kukongezea tu Hakuna agent mkubwa atachoma mafuta yake kutoka ulaya kuja kutazama kipaji kwenye ligi kama ligi kuu Tanzania Bara sababu huna Historia ya kuuza wachezaji moja kwa moja kutoka kwenye ligi yako kwenda Europe hasa ligi Bora kwahyo Timu ya Taifa inabaki kama moja kati ya njia nzuri kwa wachezaji wetu kujitangaza kimataifa
 
TFF inaongozwa na vilaza. Hii nchi inq wachezaji wengi sana ukiondoa hao wa simba na Yanga! Kwanini wasiwape na wenyewe nafasi kwenye mashindano kama hayo? Kila siku wanaitwa wachezaji wale wale!!
 
wew Nani alikwambia ili uone ubora wa mchezaji ni lazima acheze mechi 200 ndio utagundua ubora wake kuna wachezaji wengi tu Duniani apa wamesajiliwa kwa bonaza la siku moja mfano Antonio Valencia alisajiliwa kwa kucheza kwenye bonaza lilofanyika siku moja tu Na watu wakaona kipaji chake ,Yule Dogo Mohhamed Muntari alichezea timu ya Taifa ya Qatar kombe la 2022 alisajiliwa kwenye bonaza lilofanyika Ghana tena siku moja tu

Afu kwa kukongezea tu Hakuna agent mkubwa atachoma mafuta yake kutoka ulaya kuja kutazama kipaji kwenye ligi kama ligi kuu Tanzania Bara sababu huna Historia ya kuuza wachezaji moja kwa moja kutoka kwenye ligi yako kwenda Europe hasa ligi Bora kwahyo Timu ya Taifa inabaki kama moja kati ya njia nzuri kwa wachezaji wetu kujitangaza kimataifa
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana hao ulio watolea mfano walisajiriliwa katika umri gani sasa hao wazee kina Zimbwe , Msuva wanaenda kufanya nini huko? mbaya zaidi kuonyesha huna akili unasema agent kuchoma nauli wakati hio ndio kazi yake
 
TFF tunaomba mfikirie umuhimu wa mashindano, ubora wa mashindano na vipaumbele vya mashindano. Kwasasa timu ya Simba na Yanga zina mechi muhimu sana ya klabu bingwa hatua ya robo fainali na inachezwa tarehe kati ya tarehe 29 na 30 mwezi huu. Lakini nimeshangazwa na kutaka kuwatumia wachezaji muhimu wa Simba na Yanga kwenye bonanza la FIFA series ambayo itachezwa tarehe 25 huko Azerbaijan.

Hivi kweli mmeshindwa kutafakari kuona umuhimu wa timu zetu za Tanzania kufanya vyema kwenye klabu bingwa kiasa kwamba hamkuona haya ya kuwaachia wachezaji wao waendelee na program za makocha wao kujiandaa na mechi ya klabu bingwa zilizopo mbele yao?

Yaani hili nalo ni mpaka mfundishwe? Au mnataka vilabu visiwe vinatoa ruhusa kwa wachezaji wao muhimu?

Kuna umuhimu wa viongozi wa Simba na Yanga kukaa chini na TFF kuomba kubakishiwa wachezaji wote waendelee na program za maandalizi ya mechi ya klabu bingwa na isitoshe katika wachezaji wataochukuliwa ni kutoka Tanzania pekee kwavile mataifa mengine yanatoka hawa wachezaji wa Simba na Yanga hayapo kwenye hili bonanza
Hakuna kuahirisha mechi, sisi Yanga tunajiamini, hatudeki - Ally Kamwe
 
Back
Top Bottom