Babuwatanga
Member
- Oct 29, 2022
- 8
- 5
Teuzi za raisi samia zinavyoakisi dhamira njema aliyonayo kwa Watanzania.
Kassim mpingi
Rufiji -pwani
Duniani kote teuzi za kisiasa huwa na kazi kuu mbili, kazi ya kwanza ni shukran kwa kiongozi kwa waliomsaidia ushindi na kazi ya pili kudhibiti mamlaka ya uongozi hasa kwa kuweka watu makini wanoweza kufanya udhibiti huu.
Mwaka 1832 aliyekuwa seneta wa jiji la new york bw.William marcy alitoa kauli maarufu wakati anatetea teuzi zilizofanywa na raisi wa wakati huo wa marekani bw andrew jackson
Nina nukuu
“to the victor belong the spoil of the enemy “
Wakati huo neno “spoil “ likimaanisha teuzi za kisiasa kama vile ukuu wa mkoa, wilaya, balozi nk.
Hapa seneta wiliam alimaanisha mshindi (victor) ana haki ya kufanya teuzi atakazo kwa kuzingatia kazi zote mbili za teuzi ama shukran kwa kusaidia ushindi au kumsaidia usimamizi na kudhibiti dola
Mara nyingi kazi ya kwanza ya teuzi yenye lengo la shukran na pongezi kusaidia ushindi huwa haizingatii umahiri na uchapakazi wa mteuliwa,bali nafasi ya mteuliwa kwenye kufanikisha ushindi wa kiongozi anayeteua.
Mara nyingi kazi hii ya teuzi haituletei watu makini sana kwenye kuitumikia jamii na siku zote wateule huisi wao ni sehemu ya ushindi na ni ngumu kuwatenganisha wao na mamlaka iliyowateua.
Nadharia ya pili ya kazi ya teuzi ni hii ya kudhibiti mamlaka. Nadharia hii mara nyingi hupelekea teuzi zenye tija kwa jamii husika.
Katika nadharia hii ya pili wateule hupatikana kwa kuangali sifa zao na namna wanavyoweza kuleta mabadiliko yanayohitajika kwenye jamii husika, hapa kiongozi anayeteua hutazama nini jamii inataka na nani mteule yupi anaweza kufanikisha mahitajia hayo ya jamii.
Kiongozi anayeteua kwa kuzingatia kazi ya pili ya teuzi hana haja ya kutazama kama mteule alichangia ushindi wake au la.
Aina hii ya pili ya teuzi mara nyingi hafanikiwa kuleta mabadiliko yanayohitajika katika jamii husika.
Ukitazama teuzi anazofanya raisi samia toka aingie madarakani hatazami nafasi ya mteuliwa kwenye kufanikisha serikali anayoingoza kuingia madarakani,hatazami ni kwa vipi mteule husika alimsaidia yeye na raisi aliyegombea nae kama mgombea mwenza 2020.
Ndio maana huashangai kuona baadhi ya waliokuwa wagombea wa uraisi wa upinzani, watu waliokuwa sekta binafsi wenye uwezo mkubwa wa kutumikia jamii wamekuwa sehemu ya teuzi zake na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko yanayohitajika katika jamii.
Taasisi na bodi za mashirika mbalimbali nchini zinaongozwa na watu makini ambao pengine hawakuwa na mchango wa moja kwa moja wa ushindi wa chama chake bali ni watu wenye uwezo usio na shaka hata chembe, huku yeye akisisitiza atamteua yeyote mwenye sifa ili tusaidinae kwa pamoja kuijenga Tanzania tuitakayo.
Hakika teuzi za raisi samia zinaakisi dhamira njema aliyonayo kwa watanzania
Mungu ibariki afrika,mungu ibariki tanzania
#kaziiendelee