Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao.......

mimi John Kisekwa..."
Nazani (nadhani) mejitahidi Ila umezunguruka mpaka Kisumu ukarudia Kagera, umetumia muda mrefu kujieleza.
 
Chombo kimepinduka na hakijazama chote. Huenda kuna sehemu maji hayajafika kuleta madhara ya kifo. Baadhi ya watu wanaweza kuwa maeneo hayo.

Ingawa kadiri ya muda kwenda kiwango cha Oksijen kinapungua
kwaio unataka uniambie bd hio meli inaonekana kwa nje ya ziwa? M haya mambo sijui nilikua nimezimia tangu juz
 
Hivi daladala ikipata ajali kwa uzembe wa dereva mlevi balozi wa huo mtaa anapaswa ajiuzuru sababu ajali imetokea eneo lake? Wakati flani tuangalie maneno yetu hao uliowataja nahisi wengine umewarukia tu mkuu
 
Pia kuna matundu ya kutolea maji ndani ya kivuko kama yatakuwa upande huo uliopo nje ya maji kunauwezekano yakasaidia kuingiza hewa ndani japo ni kidogo.
Sie tunaona kwa nje kwa ndani sio padogo pale.

Pia, ukitaka kuelewa pindua bakuli/transparent kwenye beseni kabla haijazama yote kuna nafasi na hewa kidogo inakuwepo.
 
Engine room kuna watertight doors na bulkhead ambazo haziruhusu maji kuingia. Na kuwa na oil mwili mzima hii huenda imetokana na chombo kupinduka so oil imemwagika tu hovyo
we mwenyewe New member waweza ukawa ndo injinia mwenyewe, kua mkweli hapa n jf kwaio uliingia jana usiku kwenye meli Mheshmiwa?
 
Pia kuna matundu ya kutolea maji ndani ya kivuko kama yatakuwa upande huo uliopo nje ya maji kunauwezekano yakasaidia kuingiza hewa ndani japo ni kidogo.
Sie tunaona kwa nje kwa ndani sio padogo pale.

Pia, ukitaka kuelewa pindua bakuli/transparent kwenye beseni kabla haijazama yote kuna nafasi na hewa kidogo inakuwepo.
 
Mkuu nataka nikuambie watu wanaoishi na kufanyakazi ziwani ni very qualified kuliko hao wakusomea mimi nimefanyakazi za uvuvi ziwa victoria miaka ya nyuma huko Musoma tulikuwa tunafundishwa na mzee mmoja wa kikwaya alikuwa na ujuzi mkubwa sana ndani ya ziwa anatambua hali ya hewa ziwani kwa kuyaangalia maji tu. Nilivyoambiwa sababu kubwa ya ajali hii ni kuwa kwanza ilikuwa imejaza kupita uwezo wake pia abiria baada ya kuzogea kufika mwaroni walihama wote na kwenda mbele kujitayarisha kushuka hapo ndipo kosa likawa kubwa zaidi ndiyo maana ikapinduka
Nakubaliana Na wewe lakini swala la abiria kusogea sio sababu kabisa mara ngap abiria husogea kwenye vivuko visidondoke kama hiki ambavyo kimedondoka kingine mara nyingi abiria husogea mbele lakini haiwezekani abiria wote wasogee mbele wakati kunakuwa Na magari pale vilevile wafanyakazi wa vivuko hukaa pale mbele kabisa kuangalia usalama wa abiria, wajaribu fanyia uchunguzi kuna tatizo lingine hili la kusogea mbele waachane nalo mana linaonyesha jinsi Gani wanajaribu jitetea kwa wananchi
 
Zaidi ya wananchi 500 wamekwama katika eneo la Bugolora baada ya kukosa usafiri wa kuelekea kisiwa cha Ukara kulikotokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018.

Wananchi hao wanaoelekea kisiwani humo kutambua miili ya ndugu zao, wamekosa usafiri kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokwenda Ukara, wakiwemo viongozi mbalimbali wa Serikali.

Wakizungumza na MCL Digital leo Jumamosi Septemba 22, 2018 wameiomba Serikali kusaka njia mbadala ili kuwasaidia waweze kufika Ukara.

Lucas Makuna mkazi wa jijini Mwanza amesema huenda asiuone mwili wa kaka yake aliyefariki dunia katika ajali hiyo kwa kuwa muda umekwenda na inawekezana zoezi la utambuzi wa miili likawa na changamoto.

“Ninakumbuka mwaka 1996 ilipozama MV Bukoba baadhi ya watu walishindwa kuitambua miili ya jamaa zao hadi Serikali ikaamua kuwazika kwa pamoja,” amesema Makuna.

“Sikutaka hili litokee Serikali iangalie namna MV Nyehunge itafika hapa maana ipo kule Ukara pamoja na MV Clarias sasa sijajua kwanini.”

Christina Mwikwabe ambaye amekwama eneo hilo amesema aliwahi alfajiri katika eneo la Bogolora ili afike Ukara mapema kuutambua mwili wa mtoto wake lakini ameshindwa kufika.

Mariam Nguzu ambaye amekwama kuvuka amesema kivuko cha MV Nyehunge hakina mafuta tangu jana usiku.

Chanzo:Mwananchi
Hivi kwa nini katika majanga yanayowagusa wananchi moja kwa moja huwa mamlaka zinakuwa na kigugumizi cha kupata njia mbadala kwa wakati ma kwa haraka. Pangekuwa ni tukio la kusimamia hizi chaguzi za hovyo za marudio halafu siku ya kura patokee upungufu wa polisi wa kusimamia na kuongoza uchaguzi hakika hata kama ni zaidi ya 500 hiyo meli ingepatiwa mafuta kwa haraka kutoka popote ilimradi kuwahisha maaskari pamoja kwa lengo la makusudi ya matokeo kufikiwa.
Hapa ndo tunajiuliza, hawa "wanyonge" ni nani atakayewapigania kwa thati?....inanikumbusha muziki wa mwanamuziki Senzo wa "who gonna care for u"
 
Mkuu huyu ni shuhuda au manusura?

Lakini pia umejuaje kwamba huyu mwandishi alikuwemo kweli kwenye hio ferry? Maana sidhani kwa akili za kawaida mtu anusurike ajali kama ile ambapo hata simu yake iliharibika kwa kuingiliwa na maji, leo hii tayari kapata nyingine, (tena kule ukara hakuna duka la smartphone hadi avuke aende Ukerewe) na hapo hapo kapata ujasiri wa kuandika kwenye mitandao eti sijui ni shuhuda?

Nimeona hii post yake kwenye uzi flani nikaipuuza ila wewe naona umeibeba nzima nzima na kuifungulia uzi. Sasa tuthibitishie kuwa kweli yule alikuwemo kwenye ferry.
Mkuu hata mm nimejawa na wasiwasi huyu muhuni tu. Nimetoka kuangalia TBC wakihojiwa watu waloo nusurika wanasema kivuko kilikuwa na watu wengi na mizigo mingi hasa magunia ya mahindi wakasema wakitoka vyema ila tatizo ni kapteni alikuwa akiongea na simu gafla akakuta amepoteza uelekeo Wa lilipo gati ndipo akakunja kivuko gafla ndoo mizigo ikaanza kuanguka na watu kuamia sehemu mmoja hivyo kupelekea kivuko kuzama
 
Jina la kivuko kilichoza huko Ukara linatukumbusha muasisi wa Taifa letu ambaye alituunganisha kuwa Taifa moja la kusaidiana katika shida na Raha bila kubaguana kwa dini zetu Wala itikadi nyingine zozote zikiwemo za kisiasa.

Juzi tumepatwa na majonzi ya kuondokewa na ndugu zetu baada ya kivuko kuzama ambapo badala ya viongozi wetu kuwa kitu kimoja tulishuhudia kila mmoja kwa nafasi yake akiandika na kuongea anachojisikia katika media mbalimbali.

Tumeshuhudia Televisheni za nje zikirusha matangazo ya janga la ajali kwa muda mrefu kuliko hata Televisheni zetu ikiwemo Televisheni ya Taifa ambayo inaendeshwa kwa Kodi za wananchi. Labda niwakumbushe wamiliki wa vyombo vya habari kuwa watu hawakutaka warushe matangazo mubashara kwa lengo la kuona picha za ajali bali tulitegemea media zipaze sauti kuwaalika wadau mbalimbali wa uokozi walete ujuzi na vifaa katika kusaidia kuokoa ndugu zetu, ninyi mliona ni vyema mpige mziki na kuendelea na vipindi vyenu kwa manufaa mnayoona yanafaa.
Tumeshuhudia wanapotutoka wasannii wakubwa na viongozi wa mbalimbali mkisitisha matangazo mengine na kuomboleza kwa muda wa masaa au siku kadhaa bila hata kupewa maelekezo kutoka popote lakini kwa Mv Nyerere amkufanya hivyo....hii ni dalili ya mgawanyiko na ubaguzi ambao mwalimu aliupiga Vita.

Kilitolewa kigezo Cha Giza kusitisha uokoaji na sijaona media au KIONGOZI wa chama Tawala na serikali aliyejitokeza adharani kukemea tamko hilo lakini tumeshuhudia ajali za viongozi na wanasiasa namna zinavyoshughulikiwa..hiki kilichotokea kinatufumbua macho kuwa sisi siyo wamoja tena kwani hata viongozi wa vyama vya upinzani walikuwa na uwezo wa kwenda kuwahamasisha wananchi wakakesha wakifanya uokozi lakini nao wamebakia kwenye media kutoa matamko na kulialia bila kuchukua hatua...ubaguzi Ni dhambi kubwa.

Viongozi wa dina nao badala ya kukemea wamekuwa wanatoa kauli Tata mitandaoni bila kutoa dira na hivyo kuonyesha Kama vile wanaogopa Jambo flani japo na amini hakuna hofu kubwa kuliko hofu ya Mungu..mkiwaogopa binadamu kuliko Mungu mtaliteketeza Taifa, zungumzeni na kusimamia haki kwa Taifa Kama dini zinavyowaelekeza na siyo kuangalia binadamu anataka nini.

Ukiona Taifa limegawanyika kwenye mambo Kama haya tambua Taifa linafungua milango kwa maadui kuingia ndani kwa kupitia mianya na mgawanyiko tulioutengeneza.

Mwisho:Tunaweza kuwa na vyama vya siasa na asasi mbalimbali kwa wingi na mahitajio tunayotaka lakini hatuwezi kuwa na Tanzania zaidi ya hii tuliyonayo Sasa.

Unaweza kuhama vyama na dini utakavyo na ukaendelea kuishi huru Tanzania lakini usitegemee kuishi huru nje ya nchi yako.

Unaweza kutumia nguvu na jitihada nyingi kujenga taasisi au chombo chochote ndani ya Taifa lisilo na mgawanyiko lakini adui anaweza kubomoa taasisi na vyombo vyote pale mnaporuhusu mgawanyiko na maslahi binafsi kuwaendesha.

Pole kwa ndugu na jamaa mliofikwa na msiba.
Unadhani viongozi wa vyama vya upinzani wangeamasisha watu wakeshe kuokoa watu kwa madaraka gani waliyonayo ktk nchi wakati serikali ya mkoa ilisitisha zoezi sbb ya giza
 
Merchant shipping act na ferries act imeziondoa meli za jeshi na meli za serikali hazitumii hizi sheria. So afisa wa sumatra ambayo kwasasa inaitwa tasac upande wa majini hawezi kwenda kukagua meli za serikali pamoja na vivuko

Ukiondoa za Jeshi ambazo hazibebi abiria, Je ni haki hizi zilizo chini ya Temesa kutokaguliwa maana tayari zinabeba abiria na zinadili na maisha ya watu na tayari zimeonyesha udhaifu kuanzia MV bukoba na hii..

Hatuoni kwamba kuna haja nazo kukaguliwa maana tayari tumeona mapungufu baada ya hi kuzama na kuleta maafa.
 
Back
Top Bottom