Tested HIV positive, looking for a soul mate

Tested HIV positive, looking for a soul mate

Nimeuliza ili awe specific,njia zipo nyingi sana nilizisoma kwenye biology mwaka 1997(Kuna sexual intercourse,blood transfusion,accident,sharing of sharps instruments with infected people etc)

Haitoshi kuwa specific kwa ninayemhitaji? Unaonaje hapo? Thanks.
 
Nilikuwa mahala nikimsubiri msichana kutengeneza hayo mahusiano. Pembeni kulifungwa hema na huduma flan ikiendelea. Katika kusubiri nikageukia kwenye hema nijue kinachojiri. Nikagundua ni huduma ya kupima VVU. Bila ya hofu nikaamua kuchek huku kwa mbaali yakiwa yanapita mawazo kichwani ya kuwashangaa watu kuogopa kupima au kupokea majibu. Hakukuwa na foleni, na hilo likaniondolea hofu ya usumbufu kwa yule binti ninayemsubiri. Nikaingia moja kwa moja. Baadhi ya maswali ya yule mhudumu sikuyapenda, na kuona sasa anaanza kunichelewesha jambo ambacho nalichukia. Kwa mfano aliniuliza ni kwa nn umeamua kuja kupima? kuna wakati baada ya kugundua sikupenda maswali akaniambia kwani ulitegemea utakuja kupima bila kuulizwa? Inawezekana nilimkwaza kias flan ila yote ni kwa sababu sikuwa na mpango wa kupima siku ile na pale nilikuwa napoteza/natumia muda ule mfupi nikimsubiri mtu.(Huwa ninaweza vizuri kujibu maswali na kujieleza waziwazi lakini ni kwa wakati na mtu husika - Pale sikuwa na swala la kupima lakini ndio nikawa nimepima na huku muda wa swala lililonileta maeneo yale unazidi kutumika tofauti na nlivyotarajia). Nilijibu maswali yote kwa haraka na pia nlimwambia wazi kuwa sikuwa na mpango wa kupima ila imetokea tu.
......... Alizingatia taratibu zake kikazi, na hatimaye akanipa jibu. Kumbe ilikuwa ni kuelekea kuadhimisha siku ya ukimwi duniani disemba mosi. Nikaondoka na kwenda kwenye ATM karibu nikavuta kiasi kama kwa kuchanganyikiwa vile ili kinisaidie na haukupita muda nikakutana na nlokuwa namsubiri. ...Vip unaumwa? Yap! Nina dozi ya malaria lakini naendlea fresh.... Loh! Uko kimya sana leo, unawaza nini? Usjali, am okay. Pia si unajua kawaida yangu kama sina issue? Unajua na hiki kifua naogopa kuongea sana nitakohoa. Nilimsindikiza mahala tukiongea , kisha tukaachana.

Nikasema labda vipimo vilidanganya maana nlikuwa na dozi ya malaria na antibiotic kwa ajili ya chest infection. Nikasema nikimaliza dozi nitapima tena. Aaaa wapi? Nani asubiri?! Niliongoza mpaka dispensary flan ambayo naendaga. Breki kwa daktari. Nikamueleza mwanzo mwisho, huku nikihoji inawezekana kweli? Maana tabia yangu naijua (clean)!
Akaniuliza kwani Ulishafanikiwa wahi pima kabla? Strongly nikamjibu yes! Nilipima mwezi wa 8 ikawa fresh. Na kabla ya hapo nilipima mwezi wa 4 pia ilikuwa poa. Na nyuma yake nilifanya mpaka full blood pic. Niko fresh doc. Nikamwambia nimekuja nawe uchek. Akaniambia bahati mbaya vipimo hivyo sina , lakini maliza dozi yako then ukapime kwengine.... Siku za usoni nikapata wazo yawezekana huyo docta wangu alitumia busara tu pale.

Nadhani inatosha.

Yule binti bado yupo, huwa anajali afya na katika mazungumzo alisema ikitokea ameathirika anaweza kujiua. Wapo kadhaa wenye mtazamo huo wa kujiua. Nadhani mimi na yeye kwa sasa tunaishi ulimwengu tufauti kindoa. Simfikirii tena na ndio sababu nimekuja hapa.
...

Hongera kwa ujasiri. walau ulipima japo haikuwa kwenye Plan. Hivi tunavyotembea na huwa hatupimi sijui jamii yetu ipoje. Unasema unajijua ulikuwa clean mkuu so baada ya mwezi wa 8 hukuwa na mahusiano na mtu kabisa au? sijaelewa kidogo ?

All in all , you are a hero and May God make you stronger and healthy.
 
Amiin! Kupima haikuwa kwenye plan siku ile lakini huwa sina tatizo katika kupima. Sikuwa na mahusiano kinyau. Kwaheri ee!
 
Hayo ni mawazo ya zamani, kwa sasa most of people are educated they know everything about HIV and AIDS.Which is necessary is particular individual peace of mind. Unapoweka wazi mambo haiwezi kuzuia marimbukeni wachache kukuteta, lakini haiwezi kukupeini kwa sababu umewaambia and you know they know it . It will pain you more unapoona watu wanateta kwa sauti za chini na hata kama hawakusemi utakoma amani , this is called stress , eventhough you don't suspect it but it eats alot of your calories, lower your immunite and make you loose eppitite.This is the most distressing action but vital.

Kwa sasa sina hofu ya kutetwa, labda natetwa kwa mazuri tu. Kwa hiyo nitakuwa makini katika maamuzi kwa kuzingatia mazingira yangu ili nisijisababishie tatizo. Nitapima faida na hasara ya maamuzi mbalimbali. Incharge yuko sahihi kwa maoni yake, nawe pia uko sahihi kama nlivyowahi kukwambia kuwa ujumbe wako ni muhimu; lakini ni kawaida wakati mwingine binadamu kutofautiana kimtazamo kama ilivyo kwenu. Kazi kwangu sasa kuyatafsiri mawazo yenu katika mazingira yangu. Nawashkuru sana mnavyozidi kunijenga
 
Mkuu Pave,kwanza nikupongeze kwa moyo wako unaounyesha ktk issue hii kwa kuwajali wenzanko kwenye wakati huu mgumu kwako,hakika Mungu ndiye anaejua atakulipa nini,ushauri wangu kwanza:-weka akilini mwako kwamba lazima ipo siku utawaambia ndugu zako,rafiki zako na wafanyakazi wenzako kuhusu afya yako,(2)omba Mungu akujaalie upate mke mwema kadiri ulivyoomba,pia akujaalie mpate mtoto/watoto kisha ndio ugeukie kuwaambia ukweli jamaa zako,naamini hapo...watashtuka ila watafarijika coz watakuona una mke wako,mna mtoto wenu na ana afya nzuri tu na utaonekana ambaye huna wasiwasi kwani wakati huo nadhan utakuwa na amani moyoni.wala usijilaum kwa lolote maana hakuna aijuaye kesho yake,hayo ni maradhi mtu yeyote anaweza kuyapata pasi'nakutegemea..nakutakia maisha marefu na Mungu akuzidishie moyo wa huruma wakati huu unapohitaji kumpata mwenza wakuifanya kazi yake aliyokutuma hapa duniani,amini Mungu hampi kisogo mja wake ni kiasi cha muda tu utatimiliziwa hitaji lako,kila la kheri kaka...Asante!
 
Last edited by a moderator:
For what? Utawakamata wengi kwenye story yako ya kufanya research.

Sio vizuri mkuu,muache tu mdau madhali hajaja kukuhoji hapo ulipo sidhani kama ni sahihi ku-judge alichokiandika hapa...unless uniambie kakushikia bakora kwamba usome bandiko lake na kukulazimisha ucomment,matatizo tumeumbiwa wanadamu ndugu yangu usim-beze mwenzako kesho yakakukuta na wewe ukakosa faraja...ni maoni tu mkuu.
 
Pave unaniconfuse na sorry kwa kuuliza uliza : Inawezekanaje umepima August huna na after sometime unao na unasema hukuwa na mahusiano. Au ulikuwepo haukuonekana kwa sababu ya window period? Am so sorry but please clarify
 
Ahsante na imebidi nifrahi kuona ni kama umeyasoma mawazo yangu. Kila kitu ni hivyo hivyo; yaani najua uwezekano wa kuwaambia baadhi ya ndugu upo, lakini ni pale ambapo wataona mke na mtoto au watoto na mambo mengine yakiwa kwenye mstari. Kwa sasa labda itokee dharura itayonilazimu kufanya hivyo, vinginevyo niko okay.
 
Last edited by a moderator:
Pave unaniconfuse na sorry kwa kuuliza uliza : Inawezekanaje umepima August huna na after sometime unao na unasema hukuwa na mahusiano. Au ulikuwepo haukuonekana kwa sababu ya window period? Am so sorry but please clarify

Kwa udadisi wako nilihofia kukukanganya, na sasa imetokea. Lakini tambua mambo yote yanamajibu na jibu lolote utakalojitwalia ni sawa tu kwangu- haitanisumbua. Tafadhali hapa zingatia zaidi hitaji langu. Nilitumia neno 'inawezekana' kwa kuwa sikutaka iwe ndio jibu la moja kwa moja. Na dhumuni la kutaja kile kipindi ni kutaka nitoe picha kuwa yawezekana sikuwa nao muda mrefu kwa hiyo mtu anaweza ku imagine afya yangu japo kwa sasa nimesikia kuwa wengine hupata athari kiafya muda mchache baada ya maambukizi. Ningeweza kusema hivi, "Huwezi gundua kuwa nimeathirika maana ndio kwanza nawaza nidhibiti mwili wangu kunenepa, uzito nlikuwa nachezea 65 sasa 70 + huku tatizo la kuvusha mida ya chakula ninalo sana ninapotingwa na kazi, na stress za kazi na maisha kwa sana, najiwazia mimi na nawaza kufanya mabadiliko makubwa kimaendeleo katika familia yangu kwa ujumla jambo lililosababisha nichelewe hata kuoa, muda wangu wa kupumzika ni mdogo na mihangaiko ni mingi....." Pamoja na hayo yote status ndo hiyo na wala sikubagua anayetumia dawa. Ukiniuliza mimi binafsi nimepataje nitakwamba bado sina jibu la uhakika. Je? nitumie muda mwingi kutafuta ilikuwaje au niwekeze kwenye suluhu?
Nilimaanisha kukwambia kwaheri Kinyau , lakini kwa kuwa umeomba nikaamua kujibu tena. Sasa malizia na uje na jingine.
 
Sio vizuri mkuu,muache tu mdau madhali hajaja kukuhoji hapo ulipo sidhani kama ni sahihi ku-judge alichokiandika hapa...unless uniambie kakushikia bakora kwamba usome bandiko lake na kukulazimisha ucomment,matatizo tumeumbiwa wanadamu ndugu yangu usim-beze mwenzako kesho yakakukuta na wewe ukakosa faraja...ni maoni tu mkuu.

Naomba ayaelewe vizuri maoni yako
 
Ahsante na imebidi nifrahi kuona ni kama umeyasoma mawazo yangu. Kila kitu ni hivyo hivyo; yaani najua uwezekano wa kuwaambia baadhi ya ndugu upo, lakini ni pale ambapo wataona mke na mtoto au watoto na mambo mengine yakiwa kwenye mstari. Kwa sasa labda itokee dharura itayonilazimu kufanya hivyo, vinginevyo niko okay.

Mungu ni mwema mkuu amini mambo yatakuwa kama ulivyopanga kwa uwezo wake..mtu anakatwa miguu yote na mkono mmoja na anaishi itakuwa mtu kuwa HIV-ve,nguvu unazo kazi unayo nenda taratibu kaka yani bila hofu yoyote utayafikia malengo yako bila wasiwasi wowote.
 
Hongera sana mkuu kwa ujasiri,iwe fundisho kwa waathirika wengine wanao nyong'onyea kwa mawazo na kukosa matumaini.Hope you get the right one.Blessed
 
Amina mkuu! Mungu akuongezee busara na hekima. Pamoja!
 
Hongera sana mkuu kwa ujasiri,iwe fundisho kwa waathirika wengine wanao nyong'onyea kwa mawazo na kukosa matumaini.Hope you get the right one.Blessed

Asante sana mkuu. Mungu atufanyie wepesi panapo uzito.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom