Tested HIV positive, looking for a soul mate

Tested HIV positive, looking for a soul mate

Nimekutwa na HIV mwezi wa 11, 2014. Yawezekana nimepata maambukizi katika kipindi kinachoanzia mwezi wa 8, 2014. Nimeogopa na kujitahidi kulinda afya yangu siku zote lakini imeshakuwa hivi.

Sijui imekuwaje nawaza sikustahili hali hii lakini ndio imekuwa. Sijafikiria kuwaambia ndugu au rafiki wa karibu kwa kuogopa kuwaumiza kimawazo zaidi yangu. Kwa sasa nahitaji kukamilisha sehemu ya maisha yangu, kwa kupata mwenza.

Mwenye sifa zifuatazo:

  1. Muislamu au awe tayari kuwa muislamu.
  2. Asiwe mtoto, na asiwe anakaribia miaka 40.
  3. Awe na afya njema , na haijalishi kama ameanza kutumia dawa.
  4. Awe tayari kuolewa (akinipenda) na kupata watoto.
  5. Awe anajituma na asiwe na tabia ya uvivu iliyokithiri.

Baadhi ya wasifu wangu:

  1. Sina mtoto na sijawahi kuoa.
  2. Ninakazi na elimu ni shahada.
  3. Ninajitegemea katika maisha ya kawaida, ni msaada kwa baadhi ya ndugu zangu na, ni mchapa kazi na mpenda maendeleo.
  4. Nina miaka 35, lakini watu huniona nina umri mdogo zaidi.
  5. Umbo la wastani, urefu ni kama sentimeta 165 (5'5"), rangi ni nyeusi kiasi.

Mkuu kwanza nakupongeza sana kwa ujasiri wako. Kwa kipindi hiki cha maendeleo ya tiba kupata HIV sio kufa you can live up to your maximum life span.Ninachokushauri ulichofanya hapa ukifanye kwa watu walio karibu nawe na pia ofisini kwako, hiyo itakujengea hali ya kujiamini hasa unaposikia watu wakinong'ona mambo yao na wewe ukadhani wanakuteta. Pia ofisni watakuelewa na kukupunguzia majukumu na mambo yanayoweza kukuletea stress. Pia kwa mjibu wa sheria ya HIV ya mwaka 2008 kuna malipo ambayo waathirika wote wa HIV hupewa ili kuwasaidia lishe.Nakutakia maisha marefu ya heri , uhuru na mafanikio.
 
Mbona sioni watu wakiomba PM jamani huu ni ugonjwa kama Malaria tuu,BTW bora amejitolea kuwalinda watu kuliko angeamua kuusambaza ovyo tu
 
Je ulikuwa kwenye mahusiano wakati unapima --just curious if you cared to hint your x? and kitu gani kilifanya upime , uliugua au routine checkup?

Mkuu siku hizi na madawa na vyakula unaweza kuishi miaka mingi sana 20+ so take it as a small challenge ila ukiwa mentally free u will win this battle. Hongera kwa uwazi.

Nilikuwa mahala nikimsubiri msichana kutengeneza hayo mahusiano. Pembeni kulifungwa hema na huduma flan ikiendelea. Katika kusubiri nikageukia kwenye hema nijue kinachojiri. Nikagundua ni huduma ya kupima VVU. Bila ya hofu nikaamua kuchek huku kwa mbaali yakiwa yanapita mawazo kichwani ya kuwashangaa watu kuogopa kupima au kupokea majibu. Hakukuwa na foleni, na hilo likaniondolea hofu ya usumbufu kwa yule binti ninayemsubiri. Nikaingia moja kwa moja. Baadhi ya maswali ya yule mhudumu sikuyapenda, na kuona sasa anaanza kunichelewesha jambo ambacho nalichukia. Kwa mfano aliniuliza ni kwa nn umeamua kuja kupima? kuna wakati baada ya kugundua sikupenda maswali akaniambia kwani ulitegemea utakuja kupima bila kuulizwa? Inawezekana nilimkwaza kias flan ila yote ni kwa sababu sikuwa na mpango wa kupima siku ile na pale nilikuwa napoteza/natumia muda ule mfupi nikimsubiri mtu.(Huwa ninaweza vizuri kujibu maswali na kujieleza waziwazi lakini ni kwa wakati na mtu husika - Pale sikuwa na swala la kupima lakini ndio nikawa nimepima na huku muda wa swala lililonileta maeneo yale unazidi kutumika tofauti na nlivyotarajia). Nilijibu maswali yote kwa haraka na pia nlimwambia wazi kuwa sikuwa na mpango wa kupima ila imetokea tu.
......... Alizingatia taratibu zake kikazi, na hatimaye akanipa jibu. Kumbe ilikuwa ni kuelekea kuadhimisha siku ya ukimwi duniani disemba mosi. Nikaondoka na kwenda kwenye ATM karibu nikavuta kiasi kama kwa kuchanganyikiwa vile ili kinisaidie na haukupita muda nikakutana na nlokuwa namsubiri. ...Vip unaumwa? Yap! Nina dozi ya malaria lakini naendlea fresh.... Loh! Uko kimya sana leo, unawaza nini? Usjali, am okay. Pia si unajua kawaida yangu kama sina issue? Unajua na hiki kifua naogopa kuongea sana nitakohoa. Nilimsindikiza mahala tukiongea , kisha tukaachana.

Nikasema labda vipimo vilidanganya maana nlikuwa na dozi ya malaria na antibiotic kwa ajili ya chest infection. Nikasema nikimaliza dozi nitapima tena. Aaaa wapi? Nani asubiri?! Niliongoza mpaka dispensary flan ambayo naendaga. Breki kwa daktari. Nikamueleza mwanzo mwisho, huku nikihoji inawezekana kweli? Maana tabia yangu naijua (clean)!
Akaniuliza kwani uliwahipima kabla? Strongly nikamjibu yes! Nilipima mwezi wa 8 ikawa fresh. Na kabla ya hapo nilipima mwezi wa 4 pia ilikuwa poa. Na nyuma yake nilifanya mpaka full blood pic. Niko fresh doc. Nikamwambia nimekuja nawe uchek. Akaniambia bahati mbaya vipimo hivyo sina , lakini maliza dozi yako then ukapime kwengine.... Siku za usoni nikapata wazo yawezekana yule docta wangu alitumia busara tu pale.

Nadhani inatosha.

Yule binti bado yupo, huwa anajali afya na katika mazungumzo alisema ikitokea ameathirika anaweza kujiua. Wapo kadhaa wenye mtazamo huo wa kujiua. Nadhani mimi na yeye kwa sasa tunaishi ulimwengu tufauti kindoa. Simfikirii tena na ndio sababu nimekuja hapa.
...
 
Usikate tamaa kijana ebu fikiria kuna watu wenye cancer wanatamani ata wangekuwa na HIV waondokane na maumivu makali yanayowapata.

Vile vile jitahidi najua ni ngumu lakini jitahidi usiwe na huzuni kila wakati kwasababu huzuni itakufanya macho na maskio na fikra kutafanya kazi kwa ufanishi.

Wishing you all the best
 
Mkuu kwanza nakupongeza sana kwa ujasiri wako. Kwa kipindi hiki cha maendeleo ya tiba kupata HIV sio kufa you can live up to your maximum life span.Ninachokushauri ulichofanya hapa ukifanye kwa watu walio karibu nawe na pia ofisini kwako, hiyo itakujengea hali ya kujiamini hasa unaposikia watu wakinong'ona mambo yao na wewe ukadhani wanakuteta. Pia ofisni watakuelewa na kukupunguzia majukumu na mambo yanayoweza kukuletea stress. Pia kwa mjibu wa sheria ya HIV ya mwaka 2008 kuna malipo ambayo waathirika wote wa HIV hupewa ili kuwasaidia lishe.Nakutakia maisha marefu ya heri , uhuru na mafanikio.

Asante sana kwa ushauri, maombi na vipengele ulonipa. Nitaufanyia kazi lakini kwanza nahitaji kuwa na amani ya kuwaeleza. Huwa ninafanya kazi long hours lakini kwa sasa nimeanza kupunguza. Hata baadhi ya hofu zangu za maisha naanza kuzidhibiti. Nimesema tu haya lakini comment yako yote imebeba ujumbe muhimu sana
 
Mbona sioni watu wakiomba PM jamani huu ni ugonjwa kama Malaria tuu,BTW bora amejitolea kuwalinda watu kuliko angeamua kuusambaza ovyo tu

Asante mkuu. Najua umetumia utani kidogo kuniwekea mambo sawa, lakini naamini watu wanaelewa kuwa malaria ni ugonjwa na hivi ni virusi vinavyoharibu kinga mwilini. Kwa hiyo hili ni tatizo la kipekee na kwangu mimi nafasi ya kumpata ambaye hajaathirika ni kama hakuna. Labda tuwashauri wengine wakapime haraka ili waamue vizuri ikitokea wako +ve au -ve.
Mkuu dhambi ya kuambukiza mtu siiwezi. Kwa bahati mbaya kuna mtu ameanza kuwa karibu yangu kwa kasi and she is okay, inanipa machungu maana najiuliza alikuwa wapi siku zote!!? Namtafutia dawa ya kumkimbia (wisely) awe salama hata kiakili. Nataka kunasihi kuwa tuwe na tahadhari sana, maana sio kila muathirika anaweza kuhurumia wasioathirika. Wengine huweza kutojali na kuambukiza wengine kutokana na maumivu alopata yeye, mwishowe utu wote unamuondoka na kuwa ni kawaida yake kueneza. Nahitaji kuishi maisha ya furaha na kutimiza ndoto zangu; hali hiyo haiwezi kufikiwa kwa kutojali wengine.
 
Usikate tamaa kijana ebu fikiria kuna watu wenye cancer wanatamani ata wangekuwa na HIV waondokane na maumivu makali yanayowapata.

Vile vile jitahidi najua ni ngumu lakini jitahidi usiwe na huzuni kila wakati kwasababu huzuni itakufanya macho na maskio na fikra kutafanya kazi kwa ufanishi.

Wishing you all the best

Asante sana mkuu. Nafarijika, na nitajitahidi kama ulivyonishauri. Again, Ahsante sana
 
Pole saana! Njoo kanisani hapa kuna watu wanapona HIV mkuu.

Unaweza kushinda hili. Trust me sir.

Regards,
Humble african.

Siyo kuona tu sijawahi hata kusikia kitu kama hicho acha kuleta habari za babu wa loliondo, kama mtu amewahi kuprove hili basi aweke ushuhuda hapa
 
Mkuu kwanza nakupongeza sana kwa ujasiri wako. Kwa kipindi hiki cha maendeleo ya tiba kupata HIV sio kufa you can live up to your maximum life span.Ninachokushauri ulichofanya hapa ukifanye kwa watu walio karibu nawe na pia ofisini kwako, hiyo itakujengea hali ya kujiamini hasa unaposikia watu wakinong'ona mambo yao na wewe ukadhani wanakuteta. Pia ofisni watakuelewa na kukupunguzia majukumu na mambo yanayoweza kukuletea stress. Pia kwa mjibu wa sheria ya HIV ya mwaka 2008 kuna malipo ambayo waathirika wote wa HIV hupewa ili kuwasaidia lishe.Nakutakia maisha marefu ya heri , uhuru na mafanikio.

Mimi naomba iwe siri yako jamii yetu wote tunaifahamu ukweli ndio huo, ukiwaambia watakusema tu na hata kukutenga kiaina bora iwe siri yako na close family members
 
Ahsante sana kwa uamuzi uliouchukua,hakika mungu tu ndiye atayekulipa kwani nilitembelea maeneo Fulani yanakaliwa na wanajeshi kwa wingi,loooh!!!dawa ipatikane tu vinginevyo miaka kumi ijayo tutakuwa tumejimaliza kabisa
Asante mkuu. Najua umetumia utani kidogo kuniwekea mambo sawa, lakini naamini watu wanaelewa kuwa malaria ni ugonjwa na hivi ni virusi vinavyoharibu kinga mwilini. Kwa hiyo hili ni tatizo la kipekee na kwangu mimi nafasi ya kumpata ambaye hajaathirika ni kama hakuna. Labda tuwashauri wengine wakapime haraka ili waamue vizuri ikitokea wako +ve au -ve.
Mkuu dhambi ya kuambukiza mtu siiwezi. Kwa bahati mbaya kuna mtu ameanza kuwa karibu yangu kwa kasi and she is okay, inanipa machungu maana najiuliza alikuwa wapi siku zote!!? Namtafutia dawa ya kumkimbia (wisely) awe salama hata kiakili. Nataka kunasihi kuwa tuwe na tahadhari sana, maana sio kila muathirika anaweza kuhurumia wasioathirika. Wengine huweza kutojali na kuambukiza wengine kutokana na maumivu alopata yeye, mwishowe utu wote unamuondoka na kuwa ni kawaida yake kueneza. Nahitaji kuishi maisha ya furaha na kutimiza ndoto zangu; hali hiyo haiwezi kufikiwa kwa kutojali wengine.
 
Mimi naomba iwe siri yako jamii yetu wote tunaifahamu ukweli ndio huo, ukiwaambia watakusema tu na hata kukutenga kiaina bora iwe siri yako na close family members

Hayo ni mawazo ya zamani, kwa sasa most of people are educated they know everything about HIV and AIDS.Which is necessary is particular individual peace of mind. Unapoweka wazi mambo haiwezi kuzuia marimbukeni wachache kukuteta, lakini haiwezi kukupeini kwa sababu umewaambia and you know they know it . It will pain you more unapoona watu wanateta kwa sauti za chini na hata kama hawakusemi utakoma amani , this is called stress , eventhough you don't suspect it but it eats alot of your calories, lower your immunite and make you loose eppitite.This is the most distressing action but vital.
 
Mkuu haujaeleza jinsi ulivyopata,maana umesema kati ya mwezi wa nane na wa 12,je ulitembea na mtu yeyote hapo kati ya mwezi wa nane na 12?
 
Nimekutwa na HIV mwezi wa 11, 2014. Yawezekana nimepata maambukizi katika kipindi kinachoanzia mwezi wa 8, 2014. Nimeogopa na kujitahidi kulinda afya yangu siku zote lakini imeshakuwa hivi.

Sijui imekuwaje nawaza sikustahili hali hii lakini ndio imekuwa. Sijafikiria kuwaambia ndugu au rafiki wa karibu kwa kuogopa kuwaumiza kimawazo zaidi yangu. Kwa sasa nahitaji kukamilisha sehemu ya maisha yangu, kwa kupata mwenza.

Mwenye sifa zifuatazo:

  1. Muislamu au awe tayari kuwa muislamu.
  2. Asiwe mtoto, na asiwe anakaribia miaka 40.
  3. Awe na afya njema , na haijalishi kama ameanza kutumia dawa.
  4. Awe tayari kuolewa (akinipenda) na kupata watoto.
  5. Awe anajituma na asiwe na tabia ya uvivu iliyokithiri.

Baadhi ya wasifu wangu:

  1. Sina mtoto na sijawahi kuoa.
  2. Ninakazi na elimu ni shahada.
  3. Ninajitegemea katika maisha ya kawaida, ni msaada kwa baadhi ya ndugu zangu na, ni mchapa kazi na mpenda maendeleo.
  4. Nina miaka 35, lakini watu huniona nina umri mdogo zaidi.
  5. Umbo la wastani, urefu ni kama sentimeta 165 (5’5”), rangi ni nyeusi kiasi.

Kwanza nakushukuru kwa kujikubali na kujiona ni mwenye afya zaidi ya mtu mwenye BP, Kusukari, Saratanu nk. Hope utafanikiwa 100%.

Ushauri, achana na watu wanaokupa matumaini ya kijinga km vile tutatibu HIV, tunaombea na kuponya HIV, hawa watakukatisha tamaa na kukufanya uwe mgonjwa zaidi hasa pale watakapofanya hivo na isiwe hivo.

Mtegemee Mungu, ishi maisha ya kawaida na endelea kuwa mtu wa watu

Hope utaishi zaidi ya ya sisi wazima.
 
Kwani njia za kujipatia ukimwi huzijui??

Nimeuliza ili awe specific,njia zipo nyingi sana nilizisoma kwenye biology mwaka 1997(Kuna sexual intercourse,blood transfusion,accident,sharing of sharps instruments with infected people etc)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom