Tested HIV positive, looking for a soul mate

Tested HIV positive, looking for a soul mate

Pave

Member
Joined
Jan 24, 2015
Posts
57
Reaction score
30
Nimekutwa na HIV mwezi wa 11, 2014. Yawezekana nimepata maambukizi katika kipindi kinachoanzia mwezi wa 8, 2014. Nimeogopa na kujitahidi kulinda afya yangu siku zote lakini imeshakuwa hivi.

Sijui imekuwaje nawaza sikustahili hali hii lakini ndio imekuwa. Sijafikiria kuwaambia ndugu au rafiki wa karibu kwa kuogopa kuwaumiza kimawazo zaidi yangu. Kwa sasa nahitaji kukamilisha sehemu ya maisha yangu, kwa kupata mwenza.

Mwenye sifa zifuatazo:

  1. Muelewa na anayejiheshim
  2. Awe na afya njema , na haijalishi kama ameanza kutumia dawa.
  3. Awe anajituma na asiwe na tabia ya uvivu iliyokithiri.

Baadhi ya wasifu wangu:

  1. Sina mtoto na sijawahi kuoa.
  2. Nimeajiriwa na nimejiajiri pia.
  3. Nina miaka 35, lakini watu huniona nina umri mdogo zaidi.
  4. Umbo la wastani, urefu ni kama sentimeta 165 (5'5"), rangi ni nyeusi kiasi.
 
Pole sana Mkuu. Kila la heri katika kutafuta kile ukitakacho.
 
Kubali alilokukadiria muumba na usiwaze sana wote tu wapita njia tu na jitahidi kutengeneza upande huo.
 
Nakutakia mafanikio mema, umefanya vyema kucheck afya na kuamua kuwa muwazi, I salute you for that. Mungu akusaidie upate mke.
 
Pole sana Mkuu. Kila la heri katika kutafuta kile ukitakacho.

Kubali alilokukadiria muumba na usiwaze sana wote tu wapita njia tu na jitahidi kutengeneza upande huo.

Pole sana


Nakutakia mafanikio mema, umefanya vyema kucheck afya na kuamua kuwa muwazi, I salute you for that. Mungu akusaidie upate mke.


Regards,
Humble african.[/QUOTE]

Najaribu kujiweka kwenye viatu vyako, kwa kweli wewe ni jasiri. Kila kitu hutokea kwa makusudi maalum. Mungu aendelee kukuimarisha na akupatie haja ya moyo wako. Pole sn

Okay, thanks! mbarikiwe!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nimekutwa na HIV mwezi wa 11, 2014. Yawezekana nimepata maambukizi katika kipindi kinachoanzia mwezi wa 8, 2014. Nimeogopa na kujitahidi kulinda afya yangu siku zote lakini imeshakuwa hivi. Sijui imekuwaje…! (nawaza sikustahili hali hii) lakini ndio imekuwa. Sijafikiria kuwaambia ndugu au rafiki wa karibu kwa kuogopa kuwaumiza kimawazo zaidi yangu. Kwa sasa nahitaji kukamilisha sehemu ya maisha yangu, kwa kupata mwenza mwenye sifa zifuatazo:

  1. Muislamu au awe tayari kuwa muislamu
  2. Asiwe mtoto, na asiwe anakaribia miaka 40
  3. Awe na afya njema , na haijalishi kama ameanza kutumia dawa
  4. Awe tayari kuolewa (akinipenda) na kupata watoto
  5. Awe anajituma na asiwe na tabia ya uvivu iliyokithiri.
  6. ………
Baadhi ya wasifu wangu:

  1. Sina mtoto na sijawahi kuoa
  2. Ninakazi na elimu ni shahada
  3. Ninajitegemea katika maisha ya kawaida, ni msaada kwa baadhi ya ndugu zangu na, ni mchapa kazi na mpenda maendeleo
  4. Nina miaka 35, lakini watu huniona nina umri mdogo zaidi.
  5. Umbo la wastani, urefu ni kama sentimeta 165 (5’5”), rangi ni nyeusi kiasi
  6. ………

Unahitaji pongezi, wote wanamudu ujasiri wa namna hii. Hongera mkuu umekuwa wa kipekee katika hili.

Mungu akusaidie upate hitaji lako na zaidi akupe ujasiri zaidi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom