Terios-ina uwezo kusafiri mwendo mrefu mtwara-- musoma?

Terios-ina uwezo kusafiri mwendo mrefu mtwara-- musoma?

BUNUNGULI

Senior Member
Joined
Apr 4, 2013
Posts
192
Reaction score
37
Nimepata gari aina ya terios jamaa ananiuzia,ina mwaka mmoja tangu ainunue na ameniuzia kwa milioni 6,napenda kuuliza kwa wafahamuo ubora wa gari hizi,binafsi ninategemea kuwa naitumia kwenda likizo nyumbani musoma kutoka hapa mtwara--naomba mnishauri
 
Gari zote zinasafiri umbali wowote ule kwa safari moja lakini kuna mambo ya kuzingatia kama ifuatavyo: kabla ya safari gari inafanyiwa service - oil change na parts zilizochoka kama air cleaner, fuel filter, brake pads and shoes, battery, matairi, na ujazo wa upepo kwenye matairi - unapunguza recommended amount, wheel alignment lazima ifanyike na mengine mengi.

Muda wa kuendesha sasa katika safari zako hakikisha unakuwa na vituo vya kusimama kwa muda wa nusu saa mpaka dakika 45 kwa wewe kupumzika na gari pia kupumzika na kuangalia kama kuna dalili zozote za kuleta shida kama leaks n.k. Pia muda wote uwe unaangalia dash board kuona kama kuna any warnings. Beba spareparts muhimu na coolant, oil ya gear box (kama ni automatic), engine oil at least one litre. Waweza pia kusafisha air cleaner kila baada ya 500km kama kuna sehemu ndefu utatembea kwenye vumbi. kumbuka kufanya service just engine oil change kabla ya kurejea Mtwara.

Ukizingatia vigezo hivyo utakwenda Musoma na kurudi Mtwara kila mwaka na watu watashangaa ni kwa sababu hawana info tips nilizokupa hapo juu.

Pia kumbuka au hakikisha mafuta hayashuki zaidi ya nusu tank ili kuongeza uhai wa fuel pump kwani uwa inachemka na kipozeo chake ni fuel kwenye tank hivyo yanabidi yawe mengi.
 
Hakuna tatizo lolote kwa kusafiri nayo endapo tu utaweka utaratibu wa kupumzika (kupooza engine) say kila baada ya masaa manne hivi kwa kuizima kabisa. Huwa si vizuri kusafiri mwendo mrefu non stop kwa gari yenye engine ndogo Terios ikiwa ni mojawapo.
 
Vipi CAMI kuna jamaa kanunua inasumbua sana. Je ni bahati mbaya ama ndo zake magari ya aina hiyo??
 
... JF iko Juu!
Hakuna sababu ya kuangaika huku na huku kutafuta USHARI! "JF YATOSHA"

... BigUp! Mkuu 'Mwanamayu' na 'Whisper' kwa ushauri wenu...
Bilashaka 'BUNUNGULI' & 'Nyati' mmegonga "Likes" zenu...

...mimi mwenye ninakwenda kukaweka vizuri ka-VITS kangu, ili nikapigishe safari ya kwenda BK na kurudi Dar.
 
Jamii forum imekuwa msaada mkubwa sana,ngoja nijiandae kulipia hii terios niwe natinga nayo mpaka kijijini kwetu
 
Gari yenyewe ni kama hii hapa..........ni 660cc engined(nadhani ndio wasiwasi wake)

19545tan4d.jpg

Cc ya hii gari n 660, uwezo wa engine n mdogo sana kwa hiyo safari non-stop, inaweza enda nayo na kurudi, just remember full throttle itaharibu kila kitu, kutembea usiku itasaidia engine kuwa cool vile vile . Good lucky
 
Haiwezi, acha kuanganyika, kitapasuka unakiona hivi hivi.

Ni sawasawa na kuku aolewe na punda, watazaa nini?

Hahahaha, mbavu zangu,
Kama ni kuzaa basi atazaliwa Alien type, tatizo hiyo mimba itapatikanaje? Kongosho unatisha
 
Hapo aisee balaaa Cc 660 uende musoma na kurudi ? Itakubidi upumzike sana njiana. Panga siku nne au tano nenda rudi.
 
Hapo aisee balaaa Cc 660 uende musoma na kurudi ? Itakubidi upumzike sana njiana. Panga siku nne au tano nenda rudi.
Mmh, hivi piki piki ina CC ngapi? Mbona huwa inapiga Dar hadi Iringa siku moja? Anyway, terious ya kawaida huwa ina cc 1300, na hiyo yenye cc 660 ni terious kid.
 
Haiwezi, acha kuanganyika, kitapasuka unakiona hivi hivi.

Ni sawasawa na kuku aolewe na punda, watazaa nini?

......................... vipi wakiamua kutozaa:love:
 
Back
Top Bottom