Terios-ina uwezo kusafiri mwendo mrefu mtwara-- musoma?

Terios-ina uwezo kusafiri mwendo mrefu mtwara-- musoma?

Excellent tech info!


Gari zote zinasafiri umbali wowote ule kwa safari moja lakini kuna mambo ya kuzingatia kama ifuatavyo: kabla ya safari gari inafanyiwa service - oil change na parts zilizochoka kama air cleaner, fuel filter, brake pads and shoes, battery, matairi, na ujazo wa upepo kwenye matairi - unapunguza recommended amount, wheel alignment lazima ifanyike na mengine mengi.

Muda wa kuendesha sasa katika safari zako hakikisha unakuwa na vituo vya kusimama kwa muda wa nusu saa mpaka dakika 45 kwa wewe kupumzika na gari pia kupumzika na kuangalia kama kuna dalili zozote za kuleta shida kama leaks n.k. Pia muda wote uwe unaangalia dash board kuona kama kuna any warnings. Beba spareparts muhimu na coolant, oil ya gear box (kama ni automatic), engine oil at least one litre. Waweza pia kusafisha air cleaner kila baada ya 500km kama kuna sehemu ndefu utatembea kwenye vumbi. kumbuka kufanya service just engine oil change kabla ya kurejea Mtwara.

Ukizingatia vigezo hivyo utakwenda Musoma na kurudi Mtwara kila mwaka na watu watashangaa ni kwa sababu hawana info tips nilizokupa hapo juu.

Pia kumbuka au hakikisha mafuta hayashuki zaidi ya nusu tank ili kuongeza uhai wa fuel pump kwani uwa inachemka na kipozeo chake ni fuel kwenye tank hivyo yanabidi yawe mengi.
 
Haiwezi, acha kuanganyika, kitapasuka unakiona hivi hivi.

Ni sawasawa na kuku aolewe na punda, watazaa nini?

acha kumtisha mmbona hizi gari za IT zinapita makambako daily to zambia na malawi sembuse musoma
 
Mmh, hivi piki piki ina CC ngapi? Mbona huwa inapiga Dar hadi Iringa siku moja? Anyway, terious ya kawaida huwa ina cc 1300, na hiyo yenye cc 660 ni terious kid.


Mkuu Lukolo, Mechanism ya gari ni tofauti na pikipiki kaka. Kwa hiyo trip ya jamaa kama ni pikipiki inabidi ziwe zile heavy duty kama HONDA,KAWASAKI,YAMAHA or BMW all sports,Hizi zina power kama ya toyota 110 zina cooling system kama ya gari. lakini na sio hizi MADE IN GUANGZHOU.


Hiyo KID inaweza fika Musoma lakini kwa siku kadhaa za kuwa barabarani kwa kupumzika.
 
Cami ya 1300cc inatiga mzigo bila shida ila terios 660cc sijui hiyo mambo
 
Kuna vitu wanasemaga don't try it at home. Hii ni moja wapo. Kama unataka kuweka kituo kila baada ya 200km si mbaya waweza enda nayo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Vipi CAMI kuna jamaa kanunua inasumbua sana. Je ni bahati mbaya ama ndo zake magari ya aina hiyo??
Hata viumbe wapo wanozaliwa vilema. Cami ni gari nzuri, tatizo linaweza kuja nalo tokea upya wake au mismanagement ya gari.
 
Labda mleta uzi atuambie terios yake ni ile ya cc 1300 au ile terios kid ya 660? Kama ni ya 1300 anaweza akatumia kama wiki moja hivi from Mtwara - Musoma lakini kama ni ile terios kid hapo si chini ya wiki 2 ajiandae maana hizo terios bana zinasumbua sana kwa safari ndefu.
 
Kwani terios kid inatofauti na suzuki kei, na terios 1.3L inatofauti na suzuki swift in terms of ufanisi?
 
Back
Top Bottom