Tendwa sasa aiangukia Chadema

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Leo asubuhi ktk kipindi cha Nipashe cha Radio 1 Stereo Tendwa alionekana akiwabembeleza CDM wakutane naye, akitoa haja kwamba ule mkutano wa juzi kati yake na vyama hauhusiani kabisa na madai yao, hivyo anawashangaa kwa nini hawakuhudhuria mkutano, na hata vyama vingine vilivyohudhuria viliwashangaa CDM.

Kama kawaida mtangazaji aliyekuwa akimhoji alishindwa kumuuliza swali la msingi kabisa - kwa nini yeye Tendwa, baada ya tukio la kuuwawa kwa Mwangosi alikimbilia kwenda vyombo vya habari na kutoa kauli ya moja kwa moja kuilaumu CDM kuhusiana na tukio hilo na kutishia kukifuta CDM?

Yaani mtangazaji hakumuuliza kwa nini hata kabla ya tume ya uchunguzi kufanya kazi yake yeye aliishaamua kuwa CDM ndiyo wakosaji, hivyo kingefaa kufutwa. Pia mtangazaji hakumuuliza Tendwa kwa nini badala ya kwenda vyombo vya habari asiombe kwanza kukutana na CDM kabya ya kubwabwaja katika vyombo vya habari?

Kwa ujumla Tendwa alionekana kama vile anawabembeleza CDM wakutane.

Ushauri wangu: CDM wakutane na Tendwa lakini kwa sharti moja -- afute na aombe radhi kauli yake kwa vyombo vya habari kwamba CDM ndiyo mhusika wa tukio la mauaji ya Mwangosi hadi kufikia kutishia kukifuta chama.
 
Hongereni makamanda kwa kumkoma nyani usoni kwa kukataa ruzuku ya mafisadi kwani tutachanga senti tano tano kuikomboa nchi yetuanachaneni na ruzuku ya mafisadi! Big up kwa uamuzi huu!
 
imekuwaje mkuu,wamesusia? manake niliona kwenye gazeti jana huyu mwana ccm Tendwa akiwashauri kusuia ruzuku
 
Hongereni makamanda kwa kumkoma nyani usoni kwa kukataa ruzuku ya mafisadi kwani tutachanga senti tano tano kuikomboa nchi yetuanachaneni na ruzuku ya mafisadi! Big up kwa uamuzi huu!

Mkuu hebu eleza kitu cha kueleweka.
 
Thubutu!!! we-we-we CDM hawana ubavu wa kususia ruzuku. In fact Mbowe ataua mtu iwapo ruzuku itakatwa. Amekuwa akijenga CDM kwa lengo la kupata ruzuku zaidi, sasa iweje asuse? Ni sawa na kuwa na hisa kwenye kampuni halafu wakati wa kugawana gawiwo ususe kupokea.
 
haka kazeee nakachukia mpaka akasababishwa nikapigwa ban..ndo nimerudi juzi asije akanipandisha hasira nikapigwa ban tena...
 
Yule mzee nilishamweka kwenye kundi la wazee wanaozeeka vibaya.

Anazeeshwa vibaya na wanaomtumia. Na huyu sasa ndiyo atakuwa adui namba moja wa demokrasia, kutokana na kutumia dhamana aliyonayo kuikandamiza. Hata kama sisi tukimsamehe, HISTORIA haitamsamehe kamwe.
 
Hongereni makamanda kwa kumkoma nyani usoni kwa kukataa ruzuku ya mafisadi kwani tutachanga senti tano tano kuikomboa nchi yetuanachaneni na ruzuku ya mafisadi! Big up kwa uamuzi huu!

Walishindwa kususia shangingi la mbowe itakua ruzuku aaaaaaaaah
 
Mimi nadhani kwa busara za kawaida ili uweze kukabiliana na adui yao hautakiwi kumkimbia kwa kuwa atajua unamwogopa na atakufuata kwa njia zote ili akushinde, ni vyema wakaendelea kushiriki vikao vyote na matukio yote muhimu ili kuepusha kuacha mwanya wa kufanyika maamuzi mabaya bila wao kuelewa. Kumsusia Tendwa au chochote kinachofanywa na Tendwa ni makosa na itawagharim wao. Nawashauri waendelee kukabiliana ana kwa ana na siyo kumkimbia hiyo ni hatari kwa ustawi wao.
 
haka kazeee nakachukia mpaka akasababishwa nikapigwa ban..ndo nimerudi juzi asije akanipandisha hasira nikapigwa ban tena...
Chadema no kukutana na mwendawazimu tendwa maana yeye anajua ninyi mnajua na watu wanajua yupo pale kwa maslahi ya Ccm hivyo yeye ni moja agenda za mabadiliko tunayoyataka yaani ili tupate democrasia ya kweli kama wenzetu ni lazima wajinga kama Tendwa wasiwepo ktk nafasi kama hiyo maana anafikiria kwa kutumia tumbo na masaburi yake hivyo makamanda msikutane na huyo mpuuzi!!!!!Aendelee kukaa na hivyo vyama vibaraka vya Ccm sio chadema chama cha ukombozi!!!
 
Alikurupuka huyu mtumishi wa magamba sasa anaijutia kauli yake. Amejidhihirisha kama ni kibaraka anayetumiwa na magamba.

Hayo ndiyo matatizo ya mtu kukurupuka kuandika taarifa wakati kichwani bado ana hangover ya mikiki mikiki ya maisha ya jana yake!!! Kajipange vizuri ndipo uje uandike!!!
 
Tendwa acha unafiki Chadema sio APPT-Maendeleo kwanza kusema tu utaifuta ni kulitukana taifa la vijana na wapenda mabadiliko wa nchi hii kwa kubembeleza matapishi ya mafisadi ili ushibishe tumbo lako mzandiki tendwa kila mbaya lazima aadhibiwe awe hai au kafa na ndo unachokistahili wewe na Ccm yako
 
Back
Top Bottom