Tenda ya Bomba la gesi ya Mtwara

Tenda ya Bomba la gesi ya Mtwara

LEX STEELE

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2011
Posts
224
Reaction score
110
1. Ilitangazwa lini

2. Consultant alikuwa nani?

3. Estimates zake zinasemaje?

4. Tenda ilitangazwa na idara zipi za serikali?

5. Kampuni ngapi ziliomba hiyo tenda?

6. Majina ha hizo kampuni zilizoomba yako wapi?

7. Evaluation team ya hiyo tender ilihusisha akina nani?

8. Pre qualification stage zilipita kampuni ngapi?

9. Zilizoshindwa zilitolea kwa vigezo vipi?

10. Technical specs za huu mradi ni zipi?

11. Financial specs za huu mradi mbona siri kubwa?

12. Je kampuni ngapi za wana Mtwara zilihusishwa hata kwenye sub contracting?

13. Je, Mtwara Development Agency WALIHUSISHWAJE KWENYE HUU MPANGO?

14. Hizi TUHUMA za watu kula pesa China ni kweli?
 
Utasubiri hii kitu hata kwa miaka 100 hutaambulia chochote. Mafisadi wameshasema details za mikataba ya Serikali kuhusiana na rasilimali mbali mbali nchini ni siri kubwa.
 
Nadhani mkataba ulisainiwa chumbani somewhere huko China kwenye lijihoteli.
Sasa sijui wanaume wazima wasaini mikataba kwa usiri vyumbani huko ugenini!
Makalio yao yalisalimika kweli????
 
Mkuu sisi ndio tulikwenda wenyewe kuomba msaada CHINA tukawalilia hali, wakakubali kutoa mkopo kwa riba nafuu na grace periond nzuri - vile vile wenyewe ndio watafanya kila kitu sisi tunakabidhiwa mradi uliyo kamilika - Serikali ya Uchina haiwezi kuleta watu wababaishaji kwenye miradi inayo husu Serikali kwa Serikali, wanajuwa vizuri Kampuni zipi huko Uchina za kutekeleza mradi kama huu wa kutandaza bomba na pump za kusukuma gesi.

Mbona watu wanawasakama Wachina sana, mbona tumewahi kushuhudia miradi ya ujenzi wa barabara unofadhiliwa na Wajapani lakini Wajapani wanaleta makampuni yao kujenga barabara mfano: Kajima na Konoike bila ya kutangaza tenda, si hilo tu hapo zamani Wajapani waliwahi kutoa fedha za kununulia mchele kwa mashariti kwamba ununuliwe Ujapan kwenyewe hili ni jambo la kawaida tu - why pick on CHINESE!!

Haya tuje kwa mradi wa kujenga Hydro Electric mto Rufiji/Stigler Gorge - Wabrazil watatoa pesa zao, Macontractors wao katika utekelezaji wa mradi huo, Brazil haiwezi kukubali kutoa fedha alafu sisi tujifanye kutafuta Ma-contractos kutoka nchi nyingine, mambo mengine hatuna jinsi mkuu.

Mwisho labda niseme kwamba kuna mradi wa kutandaza mabomba ya gesi huko Pakstani kama sikosei, wahusika wa mradi huu ni Wachina nafikili urefu wake hauna tofauti na huu wa kwetu, gharama za ujenzi na kila kitu hazizidiani na mradi wa hapa kwetu na kumbuka Pakstani hiko karibu na Uchina kijografia kuliko sisi - kuna baadhi ya watu wanafikili Wachina wamejipanga kutuibia?
 
fanya utafiti uje na majibu. Sasa hapa unamuuliza nani?
ast

Kamwulize FastJet na mwanae Riz1. Hivi kwa nini mnapoteza muda wenu kuuliza maswali kama haya? Lini mikataba ya ufisadi ikawekwa wazi? Unakumbuka Karamagi alisema mikataba yake aliweka kidole hotelini nchini Uingereza kwa nini kwa sababu yule mama wa madili Maajar alikuwa balozi wetu hapo UK. Angalia jinsi alivyopata kesi zote za nchi na sasa ameona zitamtokea puani ameamua kuachia ubalozi. Usishangae rais maisha yake yakawa ya mashaka baada ya kuachia ngazi 2015. Yangu macho
 
Majibu yaleelezwa zamaaani sana humu na mchambuzi wetu bwana PASCO

wenye kudharau wakaudharau ule uzi na kilichofanyika ukahamishwa kwani haukuwa na mvuto kama threads za CHADEMA na CCM

sasa kiko wapi?
 
Majibu yako ni yafuatayo:

Tenda ya consultant haikutangazwa

Rizwani na shemeji yake Habat Marwa ndio wenye hati miliki zote za mikataba yote kati ya serikali ya Tanzania na China. Imeefikia mahala wachina wanatamka wazi kwa maafisa wa wizara ya fedha kuwa wao wanawatambua Riz na Habat.

Huko China hasikilizwi mtu na watu washakula kamisheni zao. Ila sina hakika kama wa Jerumani walitoa chochote kwani wao wako pamoja na wachina kwenye huu mradi.

Mengine wewe mezea tuu maana watu washakula.
 
Naomba kutumia model ya ile Tenda ya Bandari

1. Ilitangazwa lini-Hikutangazwa

2. Consultant alikuwa nani?-CCCC

3. Estimates zake zinasemaje? zilianza Dola milioni 360 cha juu cha nanii na nanii ikafika 460-560 hadi 660

4. Tenda ilitangazwa na idara zipi za serikali?-Haikutangazwa

5. Kampuni ngapi ziliomba hiyo tenda?-moja CCCC

6. Majina ha hizo kampuni zilizoomba yako wapi?-CCCC

7. Evaluation team ya hiyo tender ilihusisha akina nani? -Wataalamu walipekwa China na CCCC

8. Pre qualification stage zilipita kampuni ngapi?-1 CCCC

9. Zilizoshindwa zilitolea kwa vigezo vipi? Hazikuwepo

10 .Technical specs za huu mradi ni zipi?-ziliandaliwa na CCCC

11. Financial specs za huu mradi mbona siri kubwa?-Ziliandaliwa na CCCC

12. Je kampuni ngapi za wana Mtwara zilihusishwa hata kwenye sub contracting?

13. jE mtwara development agency WALIHUSISHWAJE KWENYE HUU MPANGO?

14. hIZI TUHUMA ZA WATU KULA PESA cHINA NI KWELI? - ni uwongo!.

Hili la bandari CCCC ndio waliofanya feasibility study kwa ghara yao wenyewe!
CCCC wakatafuta funder Exim Bank
CCCC wakawa ndio wajenzi
CCCC wakaomba goverment guarantee wakapata!.
CCCC ndio wangerun mpaka utakapolipwa!.

Waziri Nundu akasmell a fish, akasimamisha kila kitu, wakamruka waziri, wakamtumia naibu waziri, government guarantee ikatoka bila kuombwa na waziri husika!. Waziri Nundu akamwaga ugali, JK akawatema wote, Mwakiembe ndie akamalizia kusafisha bandari.

Sasa ni zamu ya TPDC.
Pasco.
 
Mkuu sisi ndio tulikwenda wenyewe kuomba msaada CHINA tukawalilia hali, wakakubali kutoa mkopo kwa riba nafuu na grace periond nzuri - vile vile wenyewe ndio watafanya kila kitu sisi tunakabidhiwa mradi uliyo kamilika - Serikali ya Uchina haiwezi kuleta watu wababaishaji kwenye miradi inayo husu Serikali kwa Serikali, wanajuwa vizuri Kampuni zipi huko Uchina za kutekeleza mradi kama huu wa kutandaza bomba na pump za kusukuma gesi.

Mbona watu wanawasakama Wachina sana, mbona tumewahi kushuhudia miradi ya ujenzi wa barabara unofadhiliwa na Wajapani lakini Wajapani wanaleta makampuni yao kujenga barabara mfano: Kajima na Konoike bila ya kutangaza tenda, si hilo tu hapo zamani Wajapani waliwahi kutoa fedha za kununulia mchele kwa mashariti kwamba ununuliwe Ujapan kwenyewe hili ni jambo la kawaida tu - why pick on CHINESE!!

Haya tuje kwa mradi wa kujenga Hydro Electric mto Rufiji/Stigler Gorge - Wabrazil watatoa pesa zao, Macontractors wao katika utekelezaji wa mradi huo, Brazil haiwezi kukubali kutoa fedha alafu sisi tujifanye kutafuta Ma-contractos kutoka nchi nyingine, mambo mengine hatuna jinsi mkuu.

Mwisho labda niseme kwamba kuna mradi wa kutandaza mabomba ya gesi huko Pakstani kama sikosei, wahusika wa mradi huu ni Wachina nafikili urefu wake hauna tofauti na huu wa kwetu, gharama za ujenzi na kila kitu hazizidiani na mradi wa hapa kwetu na kumbuka Pakstani hiko karibu na Uchina kijografia kuliko sisi - kuna baadhi ya watu wanafikili Wachina wamejipanga kutuibia?

1. Acha upotoshaji kwa hoja zako , kuhusu mkopo wa Exim Bank of China, tuliuchukua kwa kudanganywa kuwa kutakuwa na grace period katika ulipaji wake baada ya mradi kukamilika na hivyo katika kufanya appraisal ya financing ya mradi wa bomba la gesi watawala wakakakimbilia China kukopa, lakini kwa namna mradi ulivyo tungeweza kupata pesa za mkopo kutoka benki nyinginezo duniani tena kwa riba ndogo isipokuwa kwa kuwa wakubwa walijua exim bank of china ni kichochoro cha rushwa walikimbia kukopa pale, kumbuka hawa exim china kwenye kukopesha serikali hawafanyi kitu kinaitwa credit rating na hawafanyi tathmini ya kuona mradi wao wanajali kampuni za China zifanye kazi basi provided ninyi mnacommitment ya kulipa. Kwa taarifa yako hata wahisani wetu wa maendeleo wenye kuchangia bajeti hawajaridhika na haraka tuliotumia kufanya maamuzi ya kukopa China bila kuangalia hali halisi ya mradi.

2. Gharama za ujenzi unazoongelea PAKISTAN zipo chini kulinganisha na za kwetu kwa maana kwanza umbali wa bomba lao ni mrefu kuliko wetu, pia eneo la ujenzi ni gumu kijiografia na mwisho kipenyo cha bomba lao ni kubwa kuliko letu. Hoja ya ulinganifu wa bomba hilo na letu ipo humu JF itafute . Acha kuupotosha umma kuhusu mradi huu ambao umefunikwa na wapiga dili na maprofesa kama muhongo wameingia kichwa kichwa bila kujua waliowateua ni watu wa aina gani.
 
Upo sahihi Pasco Exim Bank of China wanajua rushwa ya kimataifa wanajua bei ya watawala wa kiafrika, watawala wetuwamepiga dili hapa,kwenye ishu ya bandari gati namba 13 na 14 ngawira zilitembezwa Wizarani ,TPA,TISS, kwa wabunge na washauri wa RAIS.

Mzee Nundu alitolewa sadaka kwa uaminifu na uadilifu wake.

Leo hatujifunzi tunafurahia mkopo wa aina ile ile wenye masharti ya mzabuni, mhandisi, mhandisi mshauri, msimamizi mmoja, wapi na wapi mwalimu wewe, mwanafunzi wewe, na bado unajisahihishia.
 
Last edited by a moderator:
Sasa ni zamu ya TPDC.Pasco. Upo sahihi PASCO Exim Bank of China wanajua rushwa ya kimataifa wanajua bei ya watawala wa kiafrika, watawala wetuwamepiga dili hapa,kwenye ishu ya bandari gati namba 13 na 14 ngawira zilitembezwa Wizarani ,TPA,TISS, kwa wabunge na washauri wa RAIS. Mzee Nundu alitolewa sadaka kwa uaminifu na uadilifu wake.Leo hatujifunzi tunafurahia mkopo wa aina ile ile wenye masharti ya mzabuni, mhandisi, mhandisi mshauri, msimamizi mmoja, wapi na wapi mwalimu wewe, mwanafunzi wewe, na bado unajisahihishia.

Mkuu nafikili unaelewa kinacho endelea kati ya mataifa ya Magharibi na Uchina - vita hii ndio inaendelea katika mradi huu, wanaweza kusema chochote cha kuwazulia Wachina as if na wenyewe hawahusiki na vices wanazo watuhumu Wachina!! Ingechukuwa muda gani kupata mkopo kutoka nchi za magharibi ambazo hali yao ya kifedha si nzuri, wangetoa mashariti gani; je kampuni ya magharibi inayohusika kusafirisha GESI kwa njia ya bomba kutoka Kilwa unataka kunieleza hiko clean sio kwamba ilikuwa inachezea TAIFA letu kwa kubadilisha badilisha tariff za GESI wakati mwingine kuifunga kabisa kwa visingizio vya kila aina, Je TANESCO ilikuwa inalipa kiasi gani cha fedha kwa mwezi kwa kampuni hii ya kinyonyaji ambayo ilikuwa imepania kuzima ushindani wa kibiashara katika usafirishaji wa gesi nchini, walikuwa wanataka wabaki wao tu! - hilo mbona amlisemi, mnawashambulia Wachina tu.

We unafikili kwa nini Serikali iliwashtukia kampuni hii kutokana na umangameza wao, Serikali ilikata shauri la kaomba msaada kutoka kwa Wachina ili wasaidie kujenga a parallel bomba kumaliza ukiritimba huu ambao ulikuwa umekubuhu! Nini kijili walipo pata habari kwamba Wachina wanakuja kujenga Bomba mbadala, walilalamika sana si hilo tu walishirikisha World Bank ili wakwamishe Wachina kwa kutoa visingizio vya kubuni tu - hata wafadhili wanao changia bajeti ya TAIFA letu waka jump kwenye bandwagon la kuwasema vibaya Wachina - wote hao i.e World Bank, Wafadhili lao moja i.e kupiga vita Wachina.

Mwanzo nilifikili malumbano haya labda yanasukumwa na mambo ya partisian lakini baada ya kulichunguza kwa umakini naona si kweli. Kwa nini tuone ajabu Wachina kufanya kila kitu, kwani ujenzi wa TAZARA walishirikisha mataifa gani? Hapa nimeuliza mbona Projects karibu zote zanazo husu Japan nchini mwetu, Wajapan ndio ufanya kila kitu na sijawahi kusikia malalamiko kuhusu hilo - why pick on Chinese!
 
Mkuu sisi ndio tulikwenda wenyewe kuomba msaada CHINA tukawalilia hali, wakakubali kutoa mkopo kwa riba nafuu na grace periond nzuri - vile vile wenyewe ndio watafanya kila kitu sisi tunakabidhiwa mradi uliyo kamilika - Serikali ya Uchina haiwezi kuleta watu wababaishaji kwenye miradi inayo husu Serikali kwa Serikali, wanajuwa vizuri Kampuni zipi huko Uchina za kutekeleza mradi kama huu wa kutandaza bomba na pump za kusukuma gesi.

Mbona watu wanawasakama Wachina sana, mbona tumewahi kushuhudia miradi ya ujenzi wa barabara unofadhiliwa na Wajapani lakini Wajapani wanaleta makampuni yao kujenga barabara mfano: Kajima na Konoike bila ya kutangaza tenda, si hilo tu hapo zamani Wajapani waliwahi kutoa fedha za kununulia mchele kwa mashariti kwamba ununuliwe Ujapan kwenyewe hili ni jambo la kawaida tu - why pick on CHINESE!!

Haya tuje kwa mradi wa kujenga Hydro Electric mto Rufiji/Stigler Gorge - Wabrazil watatoa pesa zao, Macontractors wao katika utekelezaji wa mradi huo, Brazil haiwezi kukubali kutoa fedha alafu sisi tujifanye kutafuta Ma-contractos kutoka nchi nyingine, mambo mengine hatuna jinsi mkuu.

Mwisho labda niseme kwamba kuna mradi wa kutandaza mabomba ya gesi huko Pakstani kama sikosei, wahusika wa mradi huu ni Wachina nafikili urefu wake hauna tofauti na huu wa kwetu, gharama za ujenzi na kila kitu hazizidiani na mradi wa hapa kwetu na kumbuka Pakstani hiko karibu na Uchina kijografia kuliko sisi - kuna baadhi ya watu wanafikili Wachina wamejipanga kutuibia?
Siyo kwamba Wachina wamejipanga kutuibia. Ni viongozi wetu wanasiasa ndio waliojipanga kutuibia. Kuna jamaa ameweka thread hapa JF akisema sisi tunalipa kiasi kikubwa zaidi ya Pakistan ingawa ukubwa wa bomba na urefu ni mdogo kulinganishwa na Pakistan. Mikataba iwekwe wazi.
 
Splendid indeed MKuu, hapo umenena - kama kuna Waswahili wanataka kufanya ujanja hapa na pale basi wachukuliwe hatua, lakini tusilahumu Wachina wholesale, bei za mabomba yenye diameter tofauti inajulikana, gharama za kutandaza bomba kwa kilometer moja inajulikana na hii inategemea mabomba yatapitishwa kwenye geographical formation ya aina gani, bei za pump na pump house za kusukumia gezi zinajulikana, gharama za usafirishaji wa mabomba kwa njia ya majini kutoka Uchina kuja hapa kwetu zinajulikana, logistic ya kusafirisha mabomba mpaka kwenye site zinajulikana, mtu ukiwa na information hii ni rahisi kuwakamata wajanja sasa tatizo liko wapi. Eti wachina wanaonga ili wapate miradi, watu wa magaharibi ni wa ajabu sana - Serikali ya Tanzania ndio ilikwenda kuomba mkopo kutoka kwa Wachina, sio mkopo tu walipewa na jukumu la kutekeleza project nzima mpaka mwisho, what's wrong with that if I may ask? Juzi Juzi hapa nilimsikia Waziri Mkuu wa Uchina Tigen-Ping akiseama wazi wazi kwamba kiongozi yeyote akikamatwa anakula rushwa anatwangwa risasi, na Wachina hawana utani katika hilo.
 
Kwenye Ccm hihi hakuna wakumuamini watu wote majizi tuu
 
1. Ilitangazwa lini

2. Consultant alikuwa nani?

3. Estimates zake zinasemaje?

4. Tenda ilitangazwa na idara zipi za serikali?

5. Kampuni ngapi ziliomba hiyo tenda?

6. Majina ha hizo kampuni zilizoomba yako wapi?

7. Evaluation team ya hiyo tender ilihusisha akina nani?

8. Pre qualification stage zilipita kampuni ngapi?

9. Zilizoshindwa zilitolea kwa vigezo vipi?

10 .Technical specs za huu mradi ni zipi?

11. Financial specs za huu mradi mbona siri kubwa?

12. Je kampuni ngapi za wana Mtwara zilihusishwa hata kwenye sub contracting?

13. jE mtwara development agency WALIHUSISHWAJE KWENYE HUU MPANGO?

14. hIZI TUHUMA ZA WATU KULA PESA cHINA NI KWELI?

Huyu Kikwete anatuchezea makida sasa. Ule unyonge tuliokuwa tunabatizwa nao hakuna tena, watanzania sasa tumechachamaa na tunataka kujuwa ukweli.
 
Splendid indeed MKuu,
hapo umenena - kama kuna Waswahili wanataka kufanya ujanja hapa na pale
basi wachukuliwe hatua, lakini tusilahumu Wachina wholesale, bei za
mabomba yenye diameter tofauti inajulikana, gharama za kutandaza bomba
kwa kilometer moja inajulikana na hii inategemea mabomba yatapitishwa
kwenye geographical formation ya aina gani, bei za pump na pump house za
kusukumia gezi zinajulikana, gharama za usafirishaji wa mabomba kwa
njia ya majini kutoka Uchina kuja hapa kwetu zinajulikana, logistic ya
kusafirisha mabomba mpaka kwenye site zinajulikana, mtu ukiwa na
information hii ni rahisi kuwakamata wajanja sasa tatizo liko wapi. Eti
wachina wanaonga ili wapate miradi, watu wa magaharibi ni wa ajabu sana -
Serikali ya Tanzania ndio ilikwenda kuomba mkopo kutoka kwa Wachina,
sio mkopo tu walipewa na jukumu la kutekeleza project nzima mpaka
mwisho, what's wrong with that if I may ask? Juzi Juzi hapa nilimsikia
Waziri Mkuu wa Uchina Tigen-Ping akiseama wazi wazi kwamba kiongozi
yeyote akikamatwa anakula rushwa anatwangwa risasi, na Wachina hawana
utani katika hilo.

inasemwa hata aliyetujengea uwanja wa taifa keshapigwa risasi!
 
Back
Top Bottom