Temeke na athari za madawa ya kulevya

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,487
20,652
Mimi sio mkazi wa Temeke ila kutokana na shughuli zangu kuna wakati nashinda sana eneo hilo.katika utafiti wangu usio rasim nimegundua vijana wengi wa eneo hilo wanajihusisha na uzaji wa madawa ya kulevya(unga).

Mbaya zaidi vijana wengi wemeshaathirika na matumizi yake.wamechoka sana na kudhoofika miili.eneo ambalo linaoongoza kuwa na suppliers wengi ni mtaa wa wailes.naomba niongee jambo moja hapa hata kama litawakera wengine.

Ni hivi wauza unga wengi wa eneo hilo ni vijana wa kipemba,zaramo na wandengereko (wazawa) hata watumiaji pia. Asilimia kubwa ni vijana wa jamii hizo hizo.

Sijapata jibu kwanini inakuwa hivyo.serikali ipo wapi!!?

Wadau vijana wenzetu wanaangamia Temeke mtaa Wailes.
 
Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,713
Mimi kwa uzoefu wangu wa kuishi Temeke na maeneo mengine nimegundua kuwa vijana wa Temeke wanaongoza Dar kwa kufanya mazoezi ya kukimbia na viungo nyakati za asubuhi na jioni. Tabia hii imeenea mpaka kwa watoto wadogo. Ikifika weekend ndio kabisa wanakuwa wengi sana mabarabarani wakikimbia kwa vikundi. Sijapata jibu ni kwa nini vijana wa Temeke wanazingatia zaidi mazoezi kuliko vijana wa maeneo mengine ya Dar.
 
Laura Mkaju

Senior Member
Jan 31, 2011
194
38
Pamoja na mazoezi yote hayo Temeke bado inaongoza kwa vitendo vya uhalifu, achilia bangi, dawa za kulevya hata vibaka ndio kwenyewe huko. Labda mazingira yake nayaweza kuwa source ya tabia zao.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,641
Hili nalo huwa kila likiniijia kichwani nahisi kuchanganyikiwa.
ila kwenye maswala ya makabila nadhani sio issue sana,
sababu kwa mfano wauzaji wa mexico nao ni wandengeleko?
 
mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,374
7,470
Kwa hilo la madawa ya kulevya Temeke si kama kinondoni,jamani Kinondoni ndio Columbia jamani maeneo yote ya Kinondoni Shamba,Mwanayamala,hapo Mango,Kinondoni Moscow huko kunatisha temeke cha mtoto,kinondoni ndio kitovu cha soko la unga na watumiaji wake
 
B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,251
2,636
hahaha!!wanachukuaa mazoezi ya kunyongaa watu na kukwapuaa pochi,simu na vitu vingene,siunajua ukiwaa mwizi lazima ujue kukimbiaaa..so mazoezi ya kukimbiaa ni mojaa ya kisibitisho
Mimi kwa uzoefu wangu wa kuishi Temeke na maeneo mengine nimegundua kuwa vijana wa Temeke wanaongoza Dar kwa kufanya mazoezi ya kukimbia na viungo nyakati za asubuhi na jioni. Tabia hii imeenea mpaka kwa watoto wadogo. Ikifika weekend ndio kabisa wanakuwa wengi sana mabarabarani wakikimbia kwa vikundi. Sijapata jibu ni kwa nini vijana wa Temeke wanazingatia zaidi mazoezi kuliko vijana wa maeneo mengine ya Dar.
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,666
2,177
TMK imebadilika mambo ya unga toka kinoclain yameanza kuja
Haya ni matokeo ya serikali legelege as wanaoleta madawa wanawafahamu
 
Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
714
357
Ama kwa hakika wanajamii mji wa mwanza sasa hivi biashara ya utumiaji mihadarati umekithiri
hata kufikia kuuzwa hadharani.
Hali inazidi kuwa mbaya
 
kulyunga

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
231
414
Hili nalo huwa kila likiniijia kichwani nahisi kuchanganyikiwa.
ila kwenye maswala ya makabila nadhani sio issue sana,
sababu kwa mfano wauzaji wa mexico nao ni wandengeleko?

Acha kujitoa akili na kujifanya huelewi linlozungumziwa hapa"mexico" na Mndengereko wapi na wapi! Au ndo ukweli umekuumiza? Usihofu ni moja kati ya tabia za ukweli "kugawa" maumivu...
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
18,021
8,845
Kuna tetesi ambazo zinahitaji utafiti wa kina unaohusisha umaskini na matatizo mengi ya kijamii kama magonjwa na matumizi ya madawa ya kulevya. Temeke kwa ujumla imekaaje? Vijana wanapenda kusoma na kujitambua ili kupambana na changamoto za maisha?
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,836
94,366
wilaya ya temeke kuna mitaa inaitwa 1.mtaa wa shoga
2.mtaa wa mateja....

unategemea nini?
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,836
94,366
I realize I do not understand well Temeke. Pale naenda kula ugali kiumeni tu naishia juu kwa juu.

umasikini na shule ndogo ndo main reason
Temeke ndo wilaya pekee dar ambako hakuna ombaomba..
go figure.....
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
18,021
8,845
Mimi kwa uzoefu wangu wa kuishi Temeke na maeneo mengine nimegundua kuwa vijana wa Temeke wanaongoza Dar kwa kufanya mazoezi ya kukimbia na viungo nyakati za asubuhi na jioni. Tabia hii imeenea mpaka kwa watoto wadogo. Ikifika weekend ndio kabisa wanakuwa wengi sana mabarabarani wakikimbia kwa vikundi. Sijapata jibu ni kwa nini vijana wa Temeke wanazingatia zaidi mazoezi kuliko vijana wa maeneo mengine ya Dar.
Interesting! Pengine ndio maana hakuna mabango mengi ya waganga wanaoongeza nguvu za kiume TMK kama ilivyo Ilala na Kinondoni. Hata hivyo, mbona hatuoni wanamichezo hao machachari toka temeke? Wanaenda jeshini na polisi?
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
18,021
8,845
umasikini na shule ndogo ndo main reason
Temeke ndo wilaya pekee dar ambako hakuna ombaomba..
go figure.....

Kwanini hakuna omba omba? Wengi kipato ni cha chini? Kijichi,yale mabangaloo mbona yana tishia masaki na kinondoni? Au sehemu ndogo tu ya wakazi wake ndio wako vizuri?
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom