Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,904
- 7,746
Nimemsikia komredi Mukama akisema kuwa TV ya CCM iko kwenye mchakato wa kuanzishwa na tayari bodi imeundwa. Ya chadema hata wazo hakuna, Chadema mpo serious kweli?
Nimemsikia komredi Mukama akisema kuwa TV ya CCM iko kwenye mchakato wa kuanzishwa na tayari bodi imeundwa. Ya chadema hata wazo hakuna, Chadema mpo serious kweli?
Chadema ha2jaona sehemu ya kupata fedha ya kuanzisha television SISIEMU choteni fedha zetu 2015 tutakutana...
fedha mnayi, kwa mfano pesa mnayotumia kwenye maandamano na hivi karibuni mwenyekiti wenu yuko marekani
Nimemsikia komredi Mukama akisema kuwa TV ya CCM iko kwenye mchakato wa kuanzishwa na tayari bodi imeundwa. Ya chadema hata wazo hakuna, Chadema mpo serious kweli?
Kamanda,
Nakushukuru kwa maoni na swali lako. Wazo na kuanzisha vyombo vya habari vya chama ikiwemo TV tunalo, na limeshaingizwa katika Mpango Mkakati wa chama 2011-2016. Ziko hatua ambazo tutazichukua mwaka huu kwa kadiri ya ratiba na mpango wa mwaka na ziko hatua ambazo tutazichukua baadaye, kwa kadiri ya mikakati, uwezo na mahitaji ya umma. CHADEMA tunatazama njia za mawasiliano ya umma kwa upana wake zaidi ya vyombo vya habari vilivyozoeleka. Kwa kuanzia tumeanza na TV ya CHADEMA kwenye mtandao www.chadema.tv, unaweza kuingia humo na kupata habari za uchaguzi wa Uzini hivi sasa. Hata hivyo, si kila mipango yetu tunaiweka hadharani kwa kuzingatia kuwa wapinzani wetu ndio hao wako serikalini, ni nchi yetu chama tawala ni chama dola.
Hatahivyo, ukifanya uwiano wa kirasilimali; CHADEMA inawafikia wananchi wengi zaidi iwe kwa mikutano, maandamano au vyombo vya habari kwa namna mbalimbali kuliko CCM. Jiulize kama rasilimali na fursa walizonazo CCM ndizo ambazo ingekuwa nazo CHADEMA tungefikia umma kwa kiwango gani. Bado tunajipanga kwenye kurugenzi ya habari na uenezi kwa kuzingatia mipango ya chama, wakati muafaka ukiwadia tutawaleta pamoja wanachama na wadau wengine kuhusu hili suala la vyombo vya habari vya chama.
Muwe na hakika tu kwamba maoni yenu mliyoyatoa kuhusu suala hili tumeyazingatia na tunayafanyia kazi; tuendelee kuunganisha nguvu ya umma; mpaka kieleweke.
JJ

Mhe mngejitahidi hiyo tv iwepo hewani miezi 6 kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015,suala la 2016 nadhani mngeliondoa kwani halitakuwa na maana tena,mtajimaliza kihabari kama mtaingia kwenye uchaguzi mkuu bila tv,pia kumbuka radio station (fm) ni muhimu sana na gharama zake sidhani kama chama kitashindwa.
JJ
Nguvu hiyo hiyo nguvu ya umma inaweza kuiwezesha CDM kuwa na resources zote ambazo CCM inatamba leo; maana hata CCM walizipata kwa umma huo huo.
Wekeni Mikakati ileteni kwa Umma nasi tutaichangia ifanikiwe. Kwa pamoja tutaing'oa CCM na mafisadi wake.
Asante kwa maoni yako, hata hivyo sikuandika kuwa TV itakuwa hewani mwaka 2016. Mwaka nilioandika ni wa Mpango wa Chama wa miaka mitano, kwa kuwa chama kinapanga zaidi ya uchaguzi. Kinapanga mpaka kuanza kuwatumikia watanzania kama chama kiongozi. Kuhusu lini gazeti, radio, TV na vyombo vingine vitakuwa tayari; ni ratiba ya ndani ambayo kimkakati naomba nisiitangaze kwa sasa. Lakini tunafuata ratiba yetu na tunaitekeleza; katibu mkuu Dr Slaa alitangaza kwamba mwaka 2011 tungeanzisha televisheni ya kwenye mtandao, na mwaka huo tukaanzisha. Vuteni subira kidogo tujipange vizuri zaidi katika kurugenzi ya habari na uenezi, yapo masuala ambayo ratiba yake tutaieleza kwa umma na yapo ambayo itabaki kuwa mikakati ya ndani ya vikao vya chama. Lakini muwe na hakika kwamba suala hili la vyombo vya habari tunalifanyia kazi kwa malengo ya kushinda chaguzi zijazo lakini zaidi kwa malengo ya kulitumikia taifa na kuwezesha mabadiliko ambayo kila mmoja wetu anayahitaji. Hata hivyo nilihitaji maandalizi ya makini kwa ajili ya uendelevu. CCM inaendesha vyombo vyake vya habari kwa kufyonza rasilimali za umma kurusha matangazo ya biashara hata kama vyombo hivyo vinasomwa ama kusikilizwa na watu wachache, huu mtaji haramu sisi hatutakuwa nao kwenye vyombo vya vya chama mbadala. CCM ikiacha kuwa chama dola leo vyombo vyake vikikosa matangazo ya lazima vitadidimia sana, sisi kama chama mbadala ni lazima tufikiri mbali zaidi. Ndio maana tunajikita katika kutumia njia zote za mawasiliano ya umma. Mpango Mkakati na Mpango Kazi wetu vyote vimeweka bayana lini tutaanzia chombo gani kwa ajili gani; hata hivyo hatuwezi kusema yote hadharani kwa wakati mmoja kwa kuwa leseni za vyombo hizo tunazitegemea toka serikali hii hii ambayo chama tawala kwa sasa ni CCM. Lazima tuweke kila kitu chetu sawa ndio tutangaze.
JJ
CCM wana TBC1, TBC2, TBC RADIO, RADIO UHURU, GAZETI LA UHURU, MZALENDO, JAMBO LEO, HABARI LEO you name it. Na kura za JK zikishuka kwa zaidi ya 20%,
Wanasahau kitu kimoja, muhimu sio kinachosemwa, muhimu ni uhalisia. What will a new TV station do, itawambia wananchi mishahara imepanda na umeme umeshuka bei? Waangaike na maisha ya Watanzania, then everything will be ok.