Television ya CCM iko njiani, ya CHADEMA iko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Television ya CCM iko njiani, ya CHADEMA iko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Feb 5, 2012.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Nimemsikia komredi Mukama akisema kuwa TV ya CCM iko kwenye mchakato wa kuanzishwa na tayari bodi imeundwa. Ya chadema hata wazo hakuna, Chadema mpo serious kweli?
   
 2. A

  Aaron JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,121
  Likes Received: 2,720
  Trophy Points: 280
  Chadema ha2jaona sehemu ya kupata fedha ya kuanzisha television SISIEMU choteni fedha zetu 2015 tutakutana...
   
 3. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni TBC3
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Itakuwa TV ya ccm ipi? mtandao gani utakuwa na nguvu? Naona kama hii TV imeshakufa kabla hata haijaanza!
   
 5. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hela za cdm inaishia kwenye posho za maandamano
   
 6. M

  Makupa JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  fedha mnayi, kwa mfano pesa mnayotumia kwenye maandamano na hivi karibuni mwenyekiti wenu yuko marekani
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  CCM ni mashine nyingine mkuu!! yaani kama ni soccer CCM ni Man UTD na Chadema ni vila squad ....
   
 8. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ya cdm pia iko njiani!wananchi tuko tayari kuchangia chochote!hata kodi.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hivi ni lazima wanachofanya ccm na chadema wafanye?
   
 10. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  upeo mdogo wa kufikiria na kudandia hoja bila kuangalia mbali ndio yatatuletea ya Burundi na Rwanda ktk nchi yetu kwani ikifika ccm ina vyombo vyake vya habari magazeti,radio na tv na pia vyama vingine kuwa navyo je television ya taifa itafanya nini fika ukitambua siasa ni mchezo mchafu je dhamira ya umoja na ushirikiano kwa mustakabali wa taifa letu tutauweka rehani?
   
 11. A

  Aaron JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,121
  Likes Received: 2,720
  Trophy Points: 280
  ktk maandamano ya chadema haitumiki hata shilingi moja... Ni nguvu ya vijana wenyewe hatuitaji posho yoyote kama SISIEMU wanavyofanya... Kwa kudhibitisha esimu huu hao watu unaowaona kirumba wote wametoka vjijini kwa kukodiwa na sisiemu hata maandamano ya asubuhi na kikwete ni watu walio lala kirumba kutoka mikoani... Na kama unakumbuka SLAA alipokuja mza alifukuzwa kwenye uwanja wa furahisha lakini kwa upendo 2lio nao 2kaandamana nae mpaka MAGOMENI...
  SISIEMU 2TESENI 2KISHINDWA HAPA DUNIANI 2TAKUTANA KWA MUUMBA... Mungu ibariki tz kibariki chadema
   
 12. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CCM wawe na TV ngapi tena? kwani ile TBC ni ya nani? Hayo magamba yalishajimilikisha toka kitambo na ndo maana leo ipo live Mwanza bila hata senti.
   
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  CCM wana TBC1, TBC2, TBC RADIO, RADIO UHURU, GAZETI LA UHURU, MZALENDO, JAMBO LEO, HABARI LEO you name it. Na kura za JK zikishuka kwa zaidi ya 20%,

  Wanasahau kitu kimoja, muhimu sio kinachosemwa, muhimu ni uhalisia. What will a new TV station do, itawambia wananchi mishahara imepanda na umeme umeshuka bei? Waangaike na maisha ya Watanzania, then everything will be ok.
   
 14. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #14
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kamanda,

  Nakushukuru kwa maoni na swali lako. Wazo na kuanzisha vyombo vya habari vya chama ikiwemo TV tunalo, na limeshaingizwa katika Mpango Mkakati wa chama 2011-2016. Ziko hatua ambazo tutazichukua mwaka huu kwa kadiri ya ratiba na mpango wa mwaka na ziko hatua ambazo tutazichukua baadaye, kwa kadiri ya mikakati, uwezo na mahitaji ya umma. CHADEMA tunatazama njia za mawasiliano ya umma kwa upana wake zaidi ya vyombo vya habari vilivyozoeleka. Kwa kuanzia tumeanza na TV ya CHADEMA kwenye mtandao www.chadema.tv, unaweza kuingia humo na kupata habari za uchaguzi wa Uzini hivi sasa. Hata hivyo, si kila mipango yetu tunaiweka hadharani kwa kuzingatia kuwa wapinzani wetu ndio hao wako serikalini, ni nchi yetu chama tawala ni chama dola.

  Hatahivyo, ukifanya uwiano wa kirasilimali; CHADEMA inawafikia wananchi wengi zaidi iwe kwa mikutano, maandamano au vyombo vya habari kwa namna mbalimbali kuliko CCM. Jiulize kama rasilimali na fursa walizonazo CCM ndizo ambazo ingekuwa nazo CHADEMA tungefikia umma kwa kiwango gani. Bado tunajipanga kwenye kurugenzi ya habari na uenezi kwa kuzingatia mipango ya chama, wakati muafaka ukiwadia tutawaleta pamoja wanachama na wadau wengine kuhusu hili suala la vyombo vya habari vya chama.

  Muwe na hakika tu kwamba maoni yenu mliyoyatoa kuhusu suala hili tumeyazingatia na tunayafanyia kazi; tuendelee kuunganisha nguvu ya umma; mpaka kieleweke.

  JJ
   
 15. k

  kiche JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mhe mngejitahidi hiyo tv iwepo hewani miezi 6 kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015,suala la 2016 nadhani mngeliondoa kwani halitakuwa na maana tena,mtajimaliza kihabari kama mtaingia kwenye uchaguzi mkuu bila tv,pia kumbuka radio station (fm) ni muhimu sana na gharama zake sidhani kama chama kitashindwa.
   
 16. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  JJ

  Nguvu hiyo hiyo nguvu ya umma inaweza kuiwezesha CDM kuwa na resources zote ambazo CCM inatamba leo; maana hata CCM walizipata kwa umma huo huo.

  Wekeni Mikakati ileteni kwa Umma nasi tutaichangia ifanikiwe. Kwa pamoja tutaing'oa CCM na mafisadi wake.
   
 17. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #17
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Asante kwa maoni yako, hata hivyo sikuandika kuwa TV itakuwa hewani mwaka 2016. Mwaka nilioandika ni wa Mpango wa Chama wa miaka mitano, kwa kuwa chama kinapanga zaidi ya uchaguzi. Kinapanga mpaka kuanza kuwatumikia watanzania kama chama kiongozi. Kuhusu lini gazeti, radio, TV na vyombo vingine vitakuwa tayari; ni ratiba ya ndani ambayo kimkakati naomba nisiitangaze kwa sasa. Lakini tunafuata ratiba yetu na tunaitekeleza; katibu mkuu Dr Slaa alitangaza kwamba mwaka 2011 tungeanzisha televisheni ya kwenye mtandao, na mwaka huo tukaanzisha. Vuteni subira kidogo tujipange vizuri zaidi katika kurugenzi ya habari na uenezi, yapo masuala ambayo ratiba yake tutaieleza kwa umma na yapo ambayo itabaki kuwa mikakati ya ndani ya vikao vya chama. Lakini muwe na hakika kwamba suala hili la vyombo vya habari tunalifanyia kazi kwa malengo ya kushinda chaguzi zijazo lakini zaidi kwa malengo ya kulitumikia taifa na kuwezesha mabadiliko ambayo kila mmoja wetu anayahitaji. Hata hivyo nilihitaji maandalizi ya makini kwa ajili ya uendelevu. CCM inaendesha vyombo vyake vya habari kwa kufyonza rasilimali za umma kurusha matangazo ya biashara hata kama vyombo hivyo vinasomwa ama kusikilizwa na watu wachache, huu mtaji haramu sisi hatutakuwa nao kwenye vyombo vya vya chama mbadala. CCM ikiacha kuwa chama dola leo vyombo vyake vikikosa matangazo ya lazima vitadidimia sana, sisi kama chama mbadala ni lazima tufikiri mbali zaidi. Ndio maana tunajikita katika kutumia njia zote za mawasiliano ya umma. Mpango Mkakati na Mpango Kazi wetu vyote vimeweka bayana lini tutaanzia chombo gani kwa ajili gani; hata hivyo hatuwezi kusema yote hadharani kwa wakati mmoja kwa kuwa leseni za vyombo hizo tunazitegemea toka serikali hii hii ambayo chama tawala kwa sasa ni CCM. Lazima tuweke kila kitu chetu sawa ndio tutangaze.

  JJ
   
 18. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #18
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Endelea,

  Nakubaliana nawe. Tutaunganisha nguvu ya umma katika suala hili la kuadhimisha vyombo vya habari vya chama. Hata hivyo, CCM ya kuchangiwa na umma ilikuwa ya wakati wa Nyerere kwenye mfumo wa chama kimoja iliyojenga majengo na kuchukua viwanja na rasilimali nyingine kwa michango na fedha za umma na baadaye kuiteka kuwa ya chama hicho. Huu ndio mtaji haramu wa kisiasa ambao wanautegemea mpaka sasa. CHADEMA haikuanza na mtaji kama huu. Aidha, vyombo vyao wanavianzisha na kuviendesha kwa kubebwa na dola iwe ni kwa fedha za serikali au kutumia nguvu za kidola kuchangisha fedha kwa wafanyabiashara wakubwa na watu mbalimbali wakiwemo watuhumiwa wa ufisadi. Hivyo, tusitarajie kufanya kama wao; sisi tutapaswa kuunganisha nguvu ya umma kwa maana ya wananchi waliowengi wanaotaka mabadiliko; ndio maana lazima tutekeleze mikakati yetu hatua kwa hatua.

  JJ
   
 19. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  mkuu, umeeleweka hapo.
  Ni vizuri watu wakaelewa kwamba uanzishaji wa vyombo hivi vya habari haviwezi kufanywa kama fashion au 'kumuwahi ccm', lazima kujipanga.
   
 20. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  umesahau wana redio yao nyingine inaitwa CLOUDS FM
   
Loading...