Kamanda,
Nakushukuru kwa maoni na swali lako. Wazo na kuanzisha vyombo vya habari vya chama ikiwemo TV tunalo, na limeshaingizwa katika Mpango Mkakati wa chama 2011-2016. Ziko hatua ambazo tutazichukua mwaka huu kwa kadiri ya ratiba na mpango wa mwaka na ziko hatua ambazo tutazichukua baadaye, kwa kadiri ya mikakati, uwezo na mahitaji ya umma. CHADEMA tunatazama njia za mawasiliano ya umma kwa upana wake zaidi ya vyombo vya habari vilivyozoeleka. Kwa kuanzia tumeanza na TV ya CHADEMA kwenye mtandao
www.chadema.tv, unaweza kuingia humo na kupata habari za uchaguzi wa Uzini hivi sasa. Hata hivyo, si kila mipango yetu tunaiweka hadharani kwa kuzingatia kuwa wapinzani wetu ndio hao wako serikalini, ni nchi yetu chama tawala ni chama dola.
Hatahivyo, ukifanya uwiano wa kirasilimali; CHADEMA inawafikia wananchi wengi zaidi iwe kwa mikutano, maandamano au vyombo vya habari kwa namna mbalimbali kuliko CCM. Jiulize kama rasilimali na fursa walizonazo CCM ndizo ambazo ingekuwa nazo CHADEMA tungefikia umma kwa kiwango gani. Bado tunajipanga kwenye kurugenzi ya habari na uenezi kwa kuzingatia mipango ya chama, wakati muafaka ukiwadia tutawaleta pamoja wanachama na wadau wengine kuhusu hili suala la vyombo vya habari vya chama.
Muwe na hakika tu kwamba maoni yenu mliyoyatoa kuhusu suala hili tumeyazingatia na tunayafanyia kazi; tuendelee kuunganisha nguvu ya umma; mpaka kieleweke.
JJ