SoC03 Teknolojia, Utawala Bora na Uwajibikaji katika kuleta maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla

Stories of Change - 2023 Competition

Mabula marko

Member
Jul 18, 2022
44
38
20230504_112202.png

Picha na Nathan Mpangala (MWONGOZO WA UTAWALA BORA)

UTANGULIZI
Utawala ni matumizi ya mamlaka ya kisiasa, kiuchumi au vinginevyo katika kusimamia masuala ya nchi na wananchi kwenye ngazi zote, Utawala bora ni matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu usawa na unafuataji utawala wa sheria, shughuli za utawala zimekuwa zikitegemewa sana katika kulinda na kusimamia masilahi mapana ya jamii na taifa ili kuleta maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Katika taifa la Tanzania mfano, na nchi zingine zinazoendelea kutoka Africa na sehemu zingine duniani, tumekuwa tukishuhudia momonyoko wa utawala bora, uadilifu na uwajibikaji kwa jamii nzima na uongozi wake ikiwepo kuongezeka kwa ufujaji wa mali za umma, ukiwakwaji wa haki za binadamu, kugombea madaraka na kusababisha mapigano yanayondoa maisha ya watu wengi na wengine kukimbia makazi yao. Katika nchi yetu tumeshuhudia upungufu mkubwa wa uwazi,uadilifu na uwajibikaji na pia ongezeko kubwa la wimbi la ufisadi katika taasisi za serikali na baadhi ya taasisi binafsi mfano katika sekta ya ardhi, sekta ya fedha na manunuzi ya umma, na sekta ya afya (ikiwemo NHIF), umeme,mahakama na nyinginezo, hali inayosababisha wananchi kutokuwa na Imani na utawala.

20230504_112209.png

Picha na Nathan Mpangala (MWONGOZO WA UTAWALA BORA)

Ukuaji wa teknolojia katika ulimwengu wa sasa katika karne hii ya 21 umeshuhudiwa ukileta mabadiliko makubwa katika Nyanja mbali mbali za maisha ya mwanadamu ikiwemo utawala na shughuli za uzalishaji, ili kuongeza uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu usawa na unafuataji utawala wa sheria. Daima matumizi ya teknolojia hayakwepeki na ni muhimu sana kwa taifa letu ili kuleta tija katika maendeleo, maisha ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Matumizi ya teknolojia ya mtandao wa fundomuunganiko(blockchain technology) katika taasisi za umma na binafsi ni moja ya njia ya kiteknolojia inayoweza kuleta tija, mwanga na ukombozi kwa kuleta vichocheo vya utawala bora na uwajibikaji kwa wafanyakazi ,vingozi na jamii nzima kwa ujumla katika nchi yetu ya Tanzania.

Teknolojia ya mtandao wa fundomuunganiko (blockchain technology) ni nini? ni mfumo wa kuhifadhi taarifa ambao unafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya mtandao wa kompyuta na pia smartphones, huu ni mtandao wa kumbukumbu za shughuli ambazo zimehifadhiwa katika bloki za taarifa ambazo zimeunganishwa kwa mlolongo (chain) wa kumbukumbu, kila bloki ya taarifa ina kumbukumbu za shughuli nyingi tofauti na za bloki nyingine ambazo zimehifadhiwa ndani yake na ni inahakikisha usalama wa taarifa na kuzuia mabadiliko yoyote kwenye kumbukumbu za shughuli zilizohifadhiwa.

Namna gani teknolojia hii hufanya kazi?
Kuthibitisha shughuli: Shughuli zinathibitishwa kwanza kabla ya kuongezwa kwenye mtandao wa fundomuunganiko (blockchain technology). Hii inafanyika kwa njia ya usajili wa shughuli kwenye mtandao wa fundomuunganiko(blockchain technology) ambao unathibitisha shughuli zote zilizofanyika.

Kuhakikisha usalama wa taarifa: Taarifa za kila shughuli zimehifadhiwa kwenye bloki za taarifa ambazo zimeunganishwa kwa mlolongo wa bloki. Kila bloki ina sahihi ya kipekee ya kuchunguza kama kuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika kwenye taarifa ya kumbukumbu zilizohifadhiwa.

Kuhifadhi kumbukumbu: Kumbukumbu za shughuli zilizothibitishwa zinahifadhiwa kwenye bloki za taaarifa kwenye mtandao wa fundo muunganiko (blockchain technology). Kila bloki ina kumbukumbu za shughuli nyingi ambazo zimehifadhiwa ndani yake. Bloki za taarifa zinahifadhiwa kwa njia ya usambazaji, ambayo inamaanisha kuwa kila mtumiaji wa mtandao wa fundomuunganiko (blockchain technology) ana nakala ya kumbukumbu zote zilizohifadhiwa kwenye mtandao.

Kudhibiti mabadiliko ya taarifa: Wakati taarifa za shughuli zimehifadhiwa kwenye mtandao wa fundomuunganiko (blockchain technology), zinakuwa zimehakikishwa na kuwa ngumu kubadilisha. Kila bloki ina sahihi ya kipekee ambayo inazuia mabadiliko yoyote kwenye data ya kumbukumbu zilizohifadhiwa. Hii inaongeza usalama wa kumbukumbu za shughuli kwenye mtandao fundomuunganiko (blockchain technology).

Namna ambavyo teknolojia hii itachochea utawala bora na uwajibikaji katika taifa letu la Tanzania
Teknolojia ya fundomuunganiko (blockchain technology)inaweza kuleta mabadiliko makubwa na kuchochea utawala bora na uwajibikaji nchini Tanzania. Kwa mfano, mtandao huu unaweza kutumika katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika taasisi za serikali na sekta binafsi, kama vile katika sekta ya ardhi, sekta ya fedha na manunuzi ya umma, na sekta ya afya, na zinginezo ambazo kimsingi zimekuwa ndio kinara wa kutolewa lawama na wananchi na wanaharakati wa maendeleo na pia viongozi mbali mbali ikiwemo taasisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).

Katika sekta ya ardhi, teknolojia hii inaweza kutumika kuhakikisha kumbukumbu sahihi za miliki za ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi. Kwa kutumia teknoljia hii, taarifa za umiliki wa ardhi zinaweza kuhifadhiwa kwenye mtandao ambao ni imara na hauwezi kubadilishwa. Hii inaweza kusaidia kuzuia wizi wa ardhi, migogoro ya ardhi na migogoro ya mipaka na pia teknolojia hii inaweza tumika katika sekta ya kilimo na mifugo na kupunguza mawimbi ya migogoro na kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Katika sekta ya fedha na manunuzi ya umma , teknolojia hii inaweza kutumika kusimamia manunuzi na matumizi ya fedha za umma na kudhibiti ufisadi. Kwa kutumia teknolojia hii, taarifa za manunuzi na matumizi yanaweza kuhifadhiwa kwenye mtandao ambao ni imara na hauwezi kubadilishwa. Hii inaweza kusaidia kuzuia ufisadi, kutoa uwazi na uwajibikaji katika manunuzi ya umma na kusimamia matumizi ya rasilimali za umma.

Kwenye sekta ya afya, teknolojia hii inaweza kutumika kusimamia rekodi za wagonjwa, kudhibiti upotevu wa dawa na kuongeza uwazi katika manunuzi ya vifaa vya matibabu. Kwa kutumia teknolojia hii, taarifa za afya zinaweza kuhifadhiwa kwenye mtandao ambao ni imara na hauwezi kubadilishwa. Hii inaweza kusaidia kuboresha usimamizi wa afya, kudhibiti upotevu wa dawa na kuboresha matumizi ya rasilimali katika sekta ya afya.

Sekta ya habari ,uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wa habarai. Ikiwa uhuru wa vyombo vya habari ni chachu ya kuleta utawala bora na uwajibikaji, mtandao wa fundomuunganiko(blockchain technology) unaweza kusaidia uhuru wa vyombo vya habari kwa kutoa fursa ya kuweka rekodi za habari na taarifa za vyombo vya habari kwenye mtandao ambao ni imara na hauwezi kubadilishwa na pia inaweza kuanzishwa kwa magazeti ya mitandaoni ambapo gazeti zima na mtu atalipata na kulisoma mtandao. Hii ina maana kuwa habari na taarifa hizo zinaweza kuthibitishwa kuwa ni sahihi na hazijabadilishwa na mtu yeyote, hivyo kuzipa nguvu Zaidi pia inaweza kusaidia kuongeza usalama wa taarifa za vyombo vya habari, kwa kuhakikisha kuwa ni vigumu kwa mtu yeyote kuziharibu au kuzibadilisha na waandishi wa habari.

Hii inaweza kusaidia kuzuia mashambulizi ya kimtandao au vitisho vya kisiasa dhidi ya vyombo vya habari na waandishi wa habari na Kwa kuwa teknolojia hii inaruhusu kudhibitiwa kwa taarifa, basi vyombo vya habari vinaweza kuhakikisha usalama wa vyanzo vyao vya habari na kuweka rekodi zinazoweza kutumika kama ushahidi wa habari wanazochapisha hivyo inaweza kusaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya vyombo vya habari, hivyo kuchangia katika kuimarisha utawala bora na uwajibikaji nchini Tanzania.

Kudhibiti ufisadi: teknolojia hii inaweza kusaidia kupunguza ufisadi kwa kuhakikisha kuwa shughuli zote zinafuatiliwa kwa karibu na kwamba hakuna mtu anayeweza kubadilisha kumbukumbu za shughuli hizo bila idhini. Hii inaweza kusaidia kudhibiti ufisadi na kuhakikisha kuwa taasisi zinazingatia miongozo na taratibu za kisheria.

.Kuongeza uwajibikaji kwa wadau wote: Kwa kutumia mtandao huu,taasisi zinaweza kuweka kumbukumbu za shughuli zote kwenye mtandao ambao wadau wote wanaweza kuona. Hii inamaanisha kuwa kila mtu anayehusika katika shughuli hizo, ikiwa ni pamoja na taasisi yenyewe, wateja, na washirika, wanaweza kufuatilia shughuli hizo kwa urahisi na kuhakikisha kuwa kila mtu anazingatia wajibu wake.

Sekta ya mahakama, uhuru wa mahakama na demokrasia. teknolojia hii inaweza kutumika katika mhimili wa mahakama katika kutunza kumbukumbu za madai au kesi na pia kurahisha uamuzi wa kesi kwani kwa teknolojia hii taarifa za kesi huhifadhiwa vyema na pia kuna uwezo wa kuwa na majukwaa ya maamuzi ya kesi mahakamani ikiwa tayari katika nchi zilizoendelea wameanza kuwa na mahakama za mtandao kwa kutumia teknolojia hii. Kwa kutumia teknolojia hii itasaidia sana katika kuleta demokrasia kwani tunaweza kuwa na mchakato mzuri wa uchaguzi unaotumia teknolojia hii yenye uwazi na usalama na pia katika mahakama, uhuru wa mahakama utaongezeka na pia mashauri mengi hayatachelewa tena kama hali ilivyo sasa.

20230504_112229.png

Picha na Nathan Mpangala (MWONGOZO WA UTAWALA BORA)

HITIMISHO
Ukuaji wa teknolojia katika dunia ya leo umekuwa msaada katika kurahisisha mahitaji ya kila siku ya mwanadamu matumizi ya teknolojia mbali mbali katika taasisi za umma na binafsi zinachochea kuwepo kwa uwajibikaji na utawala bora katika Nyanja zote za jamii nzima na taifa kwa ujumla na hivyo matumizi ya teknolojia kama hii nashauri yawepo katika taasisi zote za umma na binafsi ili kuchochea utawala bora na uwajibikaji, hivyo teknolojia ya kumbukumbu za vizuizi (blockchain technology) inaweza kusaidia kuleta uwazi, uwajibikaji, na ufanisi na kuchochea utawala bora na uwajibikaji, Matumizi mazuri ya rasilimali za nchi, Maendeleo endelevu, kupungua kwa umasikini, ujinga na maradhi, Kutokomea kwa rushwa, huduma bora za jamii, amani na utulivu, kuheshimiwa kwa haki za binadamu, utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa sheria na taratibu, kuleta ustawi wa wananchi nchini Tanzania.

ASANTENI SANA
 
View attachment 2609403

View attachment 2609404

View attachment 2609405

...hiiii ni ya moto kaka🔥🔥
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom