SoC02 TEHAMA ina athari hasi katika Jamii zaidi ya tunavyofikiri. Je, nini kifanyike?

Stories of Change - 2022 Competition

Content

New Member
May 21, 2022
4
10
Tunapozungumzia maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na intanet bila shaka hutaacha kuzungumzia jukwaa linalotoa fursa za ajira, kujuajiri (yaani kuuza bidhaa au huduma kupitia internet), kurahisisha mawasiliano katika jamii zetu pamoja na kurahisisha upatikanaji wa taarifa na maarifa katika mambo mbalimbali Kama faida zake.

Hizo ni faida chache tu Kati ya nyingi ambazo zinapatikana katika maendeleo ya teknolojia.

Pamoja na faida hizo lakini pia zipo athari hasi ambazo huweza kuwapata watumiaji wote wa mtandao bila kujali rika wala jinsi kwani.

Siku zinavyozidi songa teknolojia nayo izidi kukua kwa kasi na kuleta mambo mapya ambayo hayakuwepo hapo awali, Mfano teknolojia iliyokuwa ikitumika katika mawasiliano miaka ishirini na tano iliyopita ni tofauti na ya sasa hivyo kuna mazuri mengi yanayotokana na ukuaji huo bila kuacha mbali athari lukuki.

Sambamba na athari hizo, matokeo ya athari hizo huweza kuwa mabaya zaidi kwa kundi rika la watoto ( chini ya miaka 18).

Tupo katika zama ambazo si jambo la kushangaza kabisa kumkuta mtoto wa miaka kumi au hata chini ya hapo akimiliki vifaa kama simu janja na kompyuta na kuvitumia kwa matumizi binafsi kama vile kuingia mtandaoni bila uangalizi kutoka kwa wazazi au walezi.

Hali hiyo huweza kufanya akafikia maudhui yasiyofaa katika intaneti kwani inteneti imebeba maudhui mengi na ya kila namna kupitia tovuti mbali mbali na hata mitandao ya kijamii.

Embu fikiria kwanza, kwa sasa sio jambo gumu kujifunza kutumia silaha kama vile bastola kupitia video za maelekezo katika mtandao wa youtube, kuangalia picha na video za ngono katika mitandao ya kijamii Kama vile Instagram na WhatsApp.

Je itakuwaje kuhusu afya ya akili na saikojia ya mtoto anae angalia mambo hayo kila uchwao ?, Bila shaka ipo mashakani na wakati huo huo tukitarajia wawe ndo taifa la kesho

Achilia mbali mitandao ya kijamii, Kuna vipindi vya watoto maarufu kama 'katuni'. Vipindi hivi huelezea masuala mbalimbali yanayohusu watoto kama vile michezo ya watoto, elimu na hata burudani kwa lugha na picha yenye kufurahisha zaidi watoto.

Vipindi hivi wengi wetu hudhani ni suluhisho la kuwafanya watoto waepukane na madhara ya mitandao ya kijamii. Maudhui ya katuni za kitanzania mengi ni yenye kujenga kwani mara zote huelimisha na kuwaburudisha watoto.

Swala ni kuhusu katuni zinazotengenezwa kutoka mataifa mengine hasa ughaibuni, baadhi huonesha maudhui yasiyo faa kama vile mauaji na mapenzi ya jinsia moja. Mfano; katika moja ya katuni za Superman kuna maudhui yanayo ashiria mapenzi ya jinsia moja kama ambavyo inaonekana katika picha

DC8BB876-68B1-4270-B1EA-5662114D04A4.jpeg


Athari nyingine kwa watoto ni kwamba wawapo katika utumiaji wa simu ama kompyuta ni rahisi zaidi kurubuniwa na kutapeliwa ukilinganisha na makundi rika mengine kutokana na uwezo wao mdogo wa kutafakari taarifa mbalimbali wanazo kutana nazo katika mitandao ya kijamii na hata jumbe za kawaida.

Sote tunaona ni athari kiasi gani zinasababishwa na maendeleo ya teknolojia, Ukubwa wa athari hizo unatuhitaji sote kwa ujumla wananchi na mamlaka hisika kuchukua juhudi madhubuti katika kukabiliana na madhara haya haraka iwezekanavyo.

JE NINI KIFANYIKE ?

Kwanza kabisa tukianza na watoto, kundi ambalo lipo chini ya uangalizi wa wazazi , malezi yetu kwao yawe ni pamoja na kutambua nini wanafanya wawapo mtandaoni.

Hii aimaanishi kuwa nae pamoja ashikapo kifaa cha kielektroniki kama vile simujanja na kompyuta Kwani ni suala lisilowezekana bali unaweza kutambua mwenendo wake awapo mtandaoni kwa kumfungulia barua pepe (email) na kuweka mfumo wa uangalizi wa wazazi, hii itasaidia kupata taarifa zake kstika kifaa chako pindi awapo mtandaoni, pia kuchagua nini afanye na nini asifanye awapo mtandaoni.

Sambamba na hilo wazazi wanatakiwa kuwapa elimu watoto wao juu ya namna sahihi ya matumizi ya namna sahihi ya matumizi ya mitandao, elimu ya kutosha inabidi itolewe kwa watoto kabla ya kuwakabidhi vifaa kama simu na kompyuta kwa matumizi binafsi.

Elimu pia itolewe pia mashuleni, yaani watoto wafundishwe kwa kina juu ya namna sahihi ya matumizi ya teknolojia kama wanavyo fundishwa masomo mengine kwani teknolojia inazidi kukua, miaka kumi ijayo teknolojia haita kua hapa tena , Pia mamlaka husika kama vile mamlaka ya mawasiliano(TCRA) ijikite katika utoaji wa elimu juu ya maswala yanayo husu mstumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na intanet kwa ujumla kwa watoto kwani kundi hili la watoto ni kama limesahaulika katika ufikishaji wa elimu hiyo.

Na kwa upande wa maudhui yanayo rushwa katika runinga, unaweza kuseti kipengele cha uangalizi wa wazazi kupitia visembuzi ili kudhibiti ni maudhui gani angalie au asiangalie.

Hii itasaidia kuepusha uangaliaji wa maudhui yasiyo faa kupitia runinga. Tukija katika kundi lingine la watumiaji wa intaneti ambalo ni watu wazima nasi pia tunapaswa kupatiwa elimu zaidi na zaidi ili kuepuka na athari hizo.

Na si kwa watoto pekee bali hata yoyote yule ambaye anaona kwa namna moja ama nyingine amekumbwa na athari hasi za mitandao, mfano; uraibu wa video/picha za ngono kadhalika Ni vema akafanya haraka kuwaona wataalamu kwa msaada zaidi.

Wataalamu hao wanaweza kuwa watu wa saikolojia ama madaktari walio bobea katika maswala hayo.

Picha: kutoka Google
 
Back
Top Bottom