Tegeta Escrow Account Corruption Scandal: Confidential files you need to read

Tegeta Escrow Account Corruption Scandal: Confidential files you need to read

Duh! nimesoma kidogo tu hapo kwenye pdf No 9 hadi nimesikia kichefuchefu. Hivi wanapodaganyana kuwa maandishi hayo yatakuwa ni siri kati yao hata kama mkataba utakuwa umeisha, wao wanaimani kuwa kabla ya kufa kwao watakuwa wameficha kila kitu ambacho walitaka wengine wasikijue?
Sasa mbona yapo hadharani hata kabla hawajatoka katika ofisi zao japo walikubaliana kuwa zitakuwa nyaraka za siri?

TAFAKARI
 
Pesa zilitunzwa sio sababu ya capacity charges,zilitunzwa sababu ya mgogoro baina ya wanahisa wa iptl

Sasa kama MGOGORO JUU YA CAPACITY CHARGES ulikwisha kwanini IPTL na TANESCO wakutane tena huko Kunduchi kwa majadiliano ambayo hawakuafikiana? Huko kutokuafikiana kulikuwa juu ya nini?
 
Sasa kama MGOGORO JUU YA CAPACITY CHARGES ulikwisha kwanini IPTL na TANESCO wakutane tena huko Kunduchi kwa majadiliano ambayo hawakuafikiana? Huko kutokuafikiana kulikuwa juu ya nini?

kwani we unadhani kwa kampuni mbili zenye mradi mkubwa kama ule tena wa miaka 20 hakuna kitu chochote kingine wasichokubaliana zaidi ya capacity charges?
 
Mimi nataka kujua gharama za viongozi kumsindikiza na kunwaga JK airport...
 
Nimezisoma docs zote, mie naona ni nyaraka za mawasiliano ya kawaida kiofisi kuhusu hayo malipo.

Inabidi tupate mwanga zaidi katika huu 'ufisadi' najaribu kujiuliza maswali haya: Je, huo umeme Tanesco walitumia? na vipi kama malipo yangefanywa kila mwezi kama walivyolipwa wengine akina Symbion na Songas, hiyo pesa isingetumika?

Mkuu,

Ni kweli kabisa hapa hakuna doc yoyote inayoonyesha ufisadi. Kinachoonekana ni mawasiliano ya kawaida ya kutimiza utoaji wa pesa kisheria na taratibu zinazokubalika.
Hata hivyo, hali hii haijaondoa uwezekano wa kutendeka ufisadi uliofichika, kwa mfano facts za makubaliano kati ya TANESCO na IPTL kuhusu malipo yaliyosababisha kufunguliwa kwa Escrow account.(hapa ndipo kodi za wananchi znahusika).
Kutimiza lengo la kifisadi ni lazima kuonyesha taratibu zimefuatwa lakini reality haitakuwepo ukizingatia vitu kama thamani na ubora.
Ni lazima kujua kwamba mikataba yote ya kifisadi ina uhalali wa kisheria lakini inawatesa wananchi!
 
Minamshukuru sana aliyeleta hizi files sababu amesaidia sana kuonesha nikwanamna gani IPTL wanastahili kulipwa Fedha za ESCROW account. Hizi files zinatuonesha waziwazi kwamba KAFULILA alikuwa anatumika kwa kubadilisha maneno kiujanja ujanja na kupotosha ukweli kwamba pesa hizi hazistahili kulipwa kwa IPTL

View attachment 189476

kwakutumia Pdf no. 9 yenye kichwa cha habari:

Capture 14.JPG

Tunagundua kwamba kulikuwepo na makubaliano ya IPTL kulipwa fedha zilizopo kwenye account ya escrow. Lakini vikao vilifanywa kudiscuss masuala muhimu kama kodi, capacity charges na mengineyo:

Capture 17.JPG

Lakini tunaona tena upotoshaji uliokuwa ukifanywa na KAFULILA na timu yake hapa chini:

Capture 15.JPG

Huu ni upotoshaji, mfano kama argument inasema huyu provisional liquidator anaiachia majukumu yote PAP/IPTL ukijumlisha na mitambo, navilevile PAP anajicommite kubeba deni lote la IPTL je kwanini asichukue fedha ya ESCROW??? KWAHIYO TUNAMRUHUSU PAP ABEBE MADENI YA IPTL NA SIYO HAKI NYINGINE ZA IPTL KAMA FEDHA ZA ESCROW????
Capture 16.JPG
Naikumbukwe kwamba wakati fedha ya ESCROW inalipwa tiyari kulikuwa na muafaka wa kupunguza capacity charge:

Capture 19.JPG

Jaribu nawewe sasa kutafakari alafu tuulizane!

Capture 12.JPG
Kwahiyo tusimpe sasa PAP hela ya IPTL iliyopo kwenye ESCROW account?? KAFULILA anajitoa ufahamu nakujifanya hajui kuhusu ESCROW AGREEMENT!!!
Tukumbuke pia hukumu ya Jaji UTAMWA ilibase kwenye Dispute baina ya wabia wa IPTL, Na hukumu ya ICSD ilishatolewa kwa kuzitaka pande zote mbili kukaa na kukokotoa upya mahesabu na pande zote zilikaa na kufanya hivyo, soma kidokezo hapo juu.

http://www.taifaimara.co.tz/?p=410
 
nimesoma kwa umakini nimeona kumbe malipo yamelipwa kihalali na kama kuna utata basi waulizwe walioidhinisha pesa hiyo ambao ni gavana, waziri wa fedha, bot, cag, bunge na waziri mkuu, n.k. lakini inaonekana rugemarila alipewa pesa kihalali na ndomana TRA walimfata ili alipe kodi tena akalipishwa zaidi ya 1/3 na pesa hizo zikaingia benki tayari kwa matumizi halali.

Chezea 1Mil Usd wewe, unafikiri hata mimi ningesema si halali?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pata nyaraka zote kuhusu ufisadi wa Tegeta Escrow Account Scandal hapa chini

hii hali inatisha sana. ee Mungu tuondole janga la CCM katika nchi hii mwaka ujao. Amina.
 
Sijui Mbunge Zitto Kabwe alicomment nini wakati anapost hizi files kwenye facebook account yake, lakini kama dhamira yake ilikuwa kutaka kutuendelezea ule mchezo mchafu basi kwenye hili mimi binafsi na mpuuza nakumwona kama kibaraka wa mabeberu, sababu ya kusema hivi ni moja kwakumbukumbu inaonyesha pia ushiriki wa ZITTO kwenye kuwapotosha wananchi huku akitumia karata yake ya imani ambayo wananchi wanayo juu yake.
Hili sakata la IPTL kabla kina ZITTO na KAFULILA kulidakia,ilikuwa nikampeni ya mabeberu kuilazimisha serikali kuwapa dili ya kuuza umeme kupitia kampuni yao ya SONGAS. Hawakulidhishwa na serikali kutoa dili kwa nchi ya malaysia, mwendelezo wa hili sakata ulipamba moto baada ya watu wenye interest tofauti kudakia na kuanza kuishambulia serikali kuwa kuna ufisadi kwenye mradi wa IPTL,lakini ikumbukwe kuwa hivi nilini mabeberu walifanya kitu kwamaslahi ya nchi maskini na ndio maana Tanzania kwa mara ya kwanza tulipotaka kampuni binafsi ya kwaajiri ya kuzalisha umeme suruhisho letu kama nchi lilikuwa Malaysia kupitia South-south Commision.
Mabeberu kupitia BRIAN COOKSEY walianza kutuandama kwa lugha chafu sababu tu IPTL imeiside line SONGAS:

Capture 20.JPG

Malalamiko yanayotengenezwa na BRIAN COOKSEY yanabase kwenye kutaka kuimbua serikali kuwahaikufanya uamuzi mzuri ilipokubari kuipadili IPTL. Lakini je dili ya SONGAS ingekuwa na tofauti kweli naingelinda maslahi ya wazalendo kweli?? nimataifa mangapi ya kibeperi yamewekeza kwenye sekta kubwakubwa lakini bado wazalendo tunalia na mikataba yao??

Capture21.JPG

Lakini tunaona sasa kwamba pamoja na ubungo gas turbines kufanya kazi bado tunawahitaji IPTL,na BRIAN COOKSEY yupo kimya kabisa toka atoe chapisho lake, hii yote nisababu anajua mabeberu wamepata walichokuwa wanahitaji SONGAS kuwa operational.
Lakini IPTL waliliona hizi hila za BRIAN COOKSEY:

In a long letter to the African (1 June 1998) titled ‘Brian's phobia against South-South Commission', I am dubbed a racist with a ‘pathological hatred of South-South cooperation', with ‘derogatory tendencies towards African governments, leaders and its people.' In a letter to Minister of Planning, Nassoro Malocho, IPTL copied an article that appeared in East African Alternatives, and accuse me of having vested interests in Songas. I am referred to as a ‘dangerous underground advisor,' ‘an academic and business crook,' with ‘prejudices against African and Asian leaders'.

Kilichofuata wote tunajua, waandishi waudaku wakina MIHANGWA wakatafsiri maandishi ya udaku ya BRIAN nakuyasambaza. Nasasa tunamuona ZITTO na KAFULILA wakiyabeba maneno yaleyale na kuyasambaza kwa umma, mfano ZITTO anarudiarudia sana kusema "Wapinzani, vyombo vya habari na civil society vimelikalia kimya sakata hili" nikitu kilekile alichokindika BRIAN kwenye udaku wake:

""Capture23.JPG

Watanzania wenzangu hapa tunachokiona ni mchuano mkali wa kibiashara ambao ndani yake mafisadi wakubwa wa taifa hili wamenunua kesi aliyoiacha BRIAN kibaraka wa mabeberu, na sasa ndugu zetu wenyewe wakina MKONO, MENGI na ROSTAM wanatugawanya kwa maslahi yao wakimtumia mbunge wa KIGOMA KUSINI, DAVID KAFULILA.
Upotoshaji unaofanywa na KAFULILA niwawazi kabisa, niwamakusudi kwa maslahi yake binafsi na ndio maana Katibu Mkuu wa NISHATI ndugu MASWI alisema tena hadharani kuwa KAFULILA na ZITTO wanatumika na wamepewa fedha na MKONO. Sababu nyingine za kutengeneza skendo ya IPTL;
(i) Nikukweli uliowazi hawa wabunge huu nimchezo wao wa siku nyingi kuanda zengwe ambalo mwisho wasiku wanafaidika nalo kwa kupozwa nawahusika, hii nimichezo inachezwa nakamati nyingi za bunge.
(ii) Masakata makubwa kama haya husaidia kuwapa kick wanasiasa tunakumbuka sakata la EPA na RICHMOND. ZITTO na mabilioni ya uswis

Watanzania tusikubali kuwa madaraja yawatu binafsi kujipatia umaarufu wakisiasa na kujiongezea ukwasi walionao.

Capture.JPG
 
Chezea 1Mil Usd wewe, unafikiri hata mimi ningesema si halali?

Atleast tupe maono yako kwa kifupi au wapi unapohisi kuna utata kwenye malipo ya ESCROW account, kama sikukusaidia mimi basi wapo wanajamvi wengine watakao kupa ufafanuzi au kuona unapopatilia shaka. Kama hunachakuchangia lala tu upumzishe akili yako kesho uje nawazo fresh.
 
hii hali inatisha sana. ee Mungu tuondole janga la CCM katika nchi hii mwaka ujao. Amina.

Mkuu umesoma kweli hizo nyaraka?? Umezielewa kweli??? maana kalugha nacho kalichotumika ni mtihani kweli!! Minakuombea kwamungu dua zako zitimie.
Kama ungezielewa hizo nyaraka ungegundua kuwa kumbe utoaji fedha kwenye account ya ESCROW ulifuata utaratibu uliopitia vikao halali katika ngazi mbalimbali. Nakwamba hakuna taratibu zilizopindishwa humo. Halafu nakuuliza swali mkuu " KAMA PAP/IPTL WALIPEWA MITAMBO YA IPTL PAMOJA NAKUBEBA MZIGO WA DENI LA IPTL KUTOKA KWA LIQUIDATOR JE KWANINI IPTL/PAP WASIWE NAHAKI YA KUCHUKUA FEDHA ZA ESCROW ACCOUNT???? lakuzingatia kesi ya ICSD imekwisha na TANESCO na IPTL wamekubaliana juu ya viwango vipya vya capacity charge. JE MLITAKA FEDHA HIZO ZICHUKULIWE NANANI??? lakuzingatia umeme wa IPTL tumetumia bila malipo husika.

Mpe salaam mkuu "Bak" mwambie tunahitaji mchango wake nahuku, alafu aalike ndugu jamaa na marafiki!!
Caution: Aje kuchangia siyo kuropoka
 
Sasa kama MGOGORO JUU YA CAPACITY CHARGES ulikwisha kwanini IPTL na TANESCO wakutane tena huko Kunduchi kwa majadiliano ambayo hawakuafikiana? Huko kutokuafikiana kulikuwa juu ya nini?[/QUOTE

ni jukumu la tanesko kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa,pale wanapohisi kuna umuhimu wa capacity chares kushushwa wana wajibu wa kukutana na wenzao ili kujadiliana na hatimaye kufikia muafaka,mazungumzo haya ya mara kwa mara yamesababisha hadi iptl kukubali kushusha bei ya umeme per unit wanazoziuzia tanesko,kuanzia mwakani,hili ni suala la kawaida
 
kwani we unadhani kwa kampuni mbili zenye mradi mkubwa kama ule tena wa miaka 20 hakuna kitu chochote kingine wasichokubaliana zaidi ya capacity charges?

Kwa mradi mkubwa kama huo gharama na malipo huwa yanakubalika kwa pande zote husika KABLA YA KUSIGN MKATABA; BAADA YA KUSIGN MKATABA KITU KINACHOBAKIA NI UTEKELEZAJI TU!! IWAPO KUTAKUWA NA MAPINGUFU KATIKA UTEKELEZAJI HAYO HUREKEBISHWA KATIKA MKATABA MWINGINE!!! Hawa kukutana huko kunduchi ilikuwa katika mwendelezo wao wa kuhujumu nchi!!
 
Minamshukuru sana aliyeleta hizi files sababu amesaidia sana kuonesha nikwanamna gani IPTL wanastahili kulipwa Fedha za ESCROW account. Hizi files zinatuonesha waziwazi kwamba KAFULILA alikuwa anatumika kwa kubadilisha maneno kiujanja ujanja na kupotosha ukweli kwamba pesa hizi hazistahili kulipwa kwa IPTL

View attachment 189476

kwakutumia Pdf no. 9 yenye kichwa cha habari:

View attachment 189490

Tunagundua kwamba kulikuwepo na makubaliano ya IPTL kulipwa fedha zilizopo kwenye account ya escrow. Lakini vikao vilifanywa kudiscuss masuala muhimu kama kodi, capacity charges na mengineyo:

View attachment 189497

Lakini tunaona tena upotoshaji uliokuwa ukifanywa na KAFULILA na timu yake hapa chini:

View attachment 189498

Huu ni upotoshaji, mfano kama argument inasema huyu provisional liquidator anaiachia majukumu yote PAP/IPTL ukijumlisha na mitambo, navilevile PAP anajicommite kubeba deni lote la IPTL je kwanini asichukue fedha ya ESCROW??? KWAHIYO TUNAMRUHUSU PAP ABEBE MADENI YA IPTL NA SIYO HAKI NYINGINE ZA IPTL KAMA FEDHA ZA ESCROW????
View attachment 189499
Naikumbukwe kwamba wakati fedha ya ESCROW inalipwa tiyari kulikuwa na muafaka wa kupunguza capacity charge:

View attachment 189501

Jaribu nawewe sasa kutafakari alafu tuulizane!

View attachment 189502
Kwahiyo tusimpe sasa PAP hela ya IPTL iliyopo kwenye ESCROW account?? KAFULILA anajitoa ufahamu nakujifanya hajui kuhusu ESCROW AGREEMENT!!!
Tukumbuke pia hukumu ya Jaji UTAMWA ilibase kwenye Dispute baina ya wabia wa IPTL, Na hukumu ya ICSD ilishatolewa kwa kuzitaka pande zote mbili kukaa na kukokotoa upya mahesabu na pande zote zilikaa na kufanya hivyo, soma kidokezo hapo juu.

IPTL: NYUMA YA PAZIA | TAIFA IMARA

Unajua Zitto na Kafulila wanadhani sisi watanzania ni mazombii mbwa hawa!!!
 
Kwa mradi mkubwa kama huo gharama na malipo huwa yanakubalika kwa pande zote husika KABLA YA KUSIGN MKATABA; BAADA YA KUSIGN MKATABA KITU KINACHOBAKIA NI UTEKELEZAJI TU!! IWAPO KUTAKUWA NA MAPINGUFU KATIKA UTEKELEZAJI HAYO HUREKEBISHWA KATIKA MKATABA MWINGINE!!! Hawa kukutana huko kunduchi ilikuwa katika mwendelezo wao wa kuhujumu nchi!!

Hujatafakari sawasawa!! Labda kama unawakilisha mawazo ya kina KAFULILA, Kikao cha kunduchi kilikaa kujadiri hukumu ya Jaji Utamwa iliyotokana na kesi ya madai iliyofunguliwa na mbia wa Mechmer ambaye ni VIPEM, kama unafikiri kunahujuma ilifanywa na kikao hiki basi utakuwa umetafakari kwa kuhemka na akili yake utakuwa umemwazima KAFULILA akushikie. Kidokezo;

jaji utamwa.JPG

View attachment 190049

Mkuu kuna watu wengine wapo kama misukule humu hata uwaelezee vipi hawawezi kukuelewa, wameshikiwa akili na KAFULILA.
 
Back
Top Bottom