Tecno spark 5, simu yenye kamera 5 kuzinduliwa

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO, inatarajia kuzindua simu yake mpya aina ya TECNO SPARK 5 yenye kamera 5 Ijumaa hii kwa njia ya mtandao, ikiwa ni mara ya pili kuzindua kwa njia hiyo ya mtandao ambayo kwa mara ya kwanza ilitanguliwa na TECNO CAMON 15.

Akizungumza kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam, afisa masoko wa TECNO mtandaoni Bi. Salma Shafii amethibitisha kuwa ni kweli simu hiyo itazinduliwa Ijumaa kwa njia ya mtandao.

“TECNO SPARK 5 ni simu ambayo ina kamera 5 tunatarajia kuizindua Ijumaa hii na imekuja katika wakati muafaka kutokana na kwamba imezingatia ubora, pili imezingatia uchumi wa sasa kwa maana ya bei yake kuwa nafuu sana” Alisema Bi. Salma
sp5.jpg


Mwonekano wa kamera 5 za TECNO SPARK 5

Kwa upande mwingine TECNO SPARK 5 imekuja ikiwa na betri kubwa yenye kutunza chaji kwa muda mrefu zaidi kutokana na kuwa na 5000mAh. Ni simu isiyohitaji kutembea na power bank” Alisema Bi. Salma.

Hata hivyo TECNO SPARK 5 imethibitishwa kuwa ni simu ambayo ina skrini kubwa yenye inchi 7 na inamwezesha mtumiaji kutazama video au kucheza gemu bila kutatizika na kwa muda mrefu kadiri anavyotaka. Simu hiyo yenye teknolojia ya kisasa kabisa imekuja ikiwa na rangi nne kuu; Ice Jadeite, Spark Orange, Vacation Blue na Misty Grey

sp51.jpg

Mwonekano wa pande zote TECNO SPARK 5
sp52.jpg

Mwonekano wa rangi za TECNO SPARK 5

TECNO SPARK 5 imekuja ikiwa katika aina tatu; SPARK 5 Pro, SPARK 5 na SPARK 5 Air. Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa simu hiyo ya SPARK 5 utafanyika katika kurasa za TECNO za mitandao ya kijamii Facebook, Instagram na Twitter tecnomobiletanzania.
 
Tecno kipi kinawakwamisha kuja na simu inayotumia Qualcomm processor?, mtu unanunua simu ndani ya miezi mitatu Camera quality inapungua, gaming tatizo simu ina-overheat, simu ku-stack wakati wa matumizi na ku-poweroff ukiwa unatumia internet.

Ndo maana watu wanabeza na kusifia iPhone and Samsung, naamini kampuni hizi; Oppo, Xiaomi, Redmi, Doogdee, Realme, Vivo (now imeingia Tanzania) zikiamua kukazania soko la Africa kama wanavyofanya kule India basi monopoly ya Tecno lazima itakwisha, Tecno simu ni almost under 250$ lakini quality matatizo matupu!
 
Mnatujazia camera utadhani wapiga picha, hizi simu za mademu za kupiga picha na kutuma Instagram, badoo, snapchat.

Team techno changamkieni fulsa
 
Nadhani Techno wamekosea jukwaaa waende Facebook huku watu wote wanatumia Iphone na samsung

Yataka moyo kutumia Techno device
 
Haishangazi kuona umesifia battery na Camera tuu...
Ndio maana siku zote mtumiaji wa tecno akiwa kweny battle na simu nyingine anapanic, anachosifia ni battery na camera..

Niambieni leo kitu gani mtumiaji wa tecno tunasikia wanajivunia..?
 
Haishangazi kuona umesifia battery na Camera tuu...
Ndio maana siku zote mtumiaji wa tecno akiwa kweny battle na simu nyingine anapanic, anachosifia ni battery na camera..

Niambieni leo kitu gani mtumiaji wa tecno tunasikia wanajivunia..?
Camera yenyewe ni hovyo. Sisi watu weusi ndio tunapenda tecno inatutoa weupe au tunang'aa kutokana na ile high colour saturation ya tecno camera.

Ukiona mtu anasifia tecno camera ujue ni hawa wenzangu wenye rangi nyeusi ili angalau tuonekane weuse au light skin ila ukikutana na sisi ni mablack kweli kweli.

Batter pia ni hovyo.
 
Back
Top Bottom