TECNO wamejitafuta wamejipata kwa hili sio poa

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Usichokijua kuhusu Tecno camon 20 Premier

Tecno wameamua aisee mwaka 2023 ni mapinduzi ya teknolojia tu, Leo nakuletea makala kuhusu Hii simu ya Tecno Camon 20 Premier 5G ambayo iliachiwa mwezi wa tano mwaka huu Ikiwa na feature kedekede unazijua zipi ? Shusha uzi chini

Tecno Camon 20 Premier specs:
Display ni 6.67inches + AMOLED display yenye 120Hz refresh rate
Processor yake ni MediaTek Dimensity 8050
Storage ni 512Gb + Ram 8Gb
Android version 13 + Hios 13
Main Camera 50mp + 108mp + 2mp
Front camera 32mp + 2.5f + 24mm(wide)
Battery lipo 5000mah + fast charging 45W
color Dark welkin, Serenity Blue
gharama yake ni 312k mpaka 400k

Ndani ya box
Tecno hii imekuja na teknolojia mpya aina ya magic skin ambayo inakusaidia kutumia simu yako kwenye mazingira yoyote Yale yani kuanzia kwenye vumbi, mafuta, sehemu za baridi bila kusababisha shida yoyote ile mahali.

Kioo chake kikubwa alafu ni AMOLED display kikiwa na refresh rate 120Hz yenye kukupa uhuru wa kupangusa au kuperuzi kwa raha bila kuganda Ganda kabisa. Inakusaidia kuweza kutumia simu kwenye mazingira ya jua pamoja na kukulinda na mionzi inayotoka kwenye simu.

Kwenye performance usiwe na shaka maana inatumia processor ya mediaTek dimensity 8050 unaweza tumia bila kuganda Ganda kucheza game pia inatumia nguvu ndogo na kuweza kulinda simu na maisha ya betri.

Battery lake liko imara kwenye kukaa na chaji muda mrefu kwani unaweza tumia kucheza game , pia imekuja na 45W fast charging utaweza kuchaji simu na kujaa ndani ya Lisaa moja na dakika mbili kutoka 1% mpaka kufikia .

Fingerprint yake imekuja Ikiwa ndani mbele ya kioo chako kwaiyo utaweza kutoa lock kwenye simu yako kupitia mbele ya kioo, imekuja teknolojia ya 5G kwenye kuperuzi ni moto wa kuotea mbali aiseee.

Imekuja na android version 13 ila unaweza update android version 14 kwa beta kwanza au usubirie mpaka mwezi wa Tisa kupata official Android version 14 kwenye hii simu

Kamera Iko poa Kuna Sensor ya Ois yenye kukusaidia kuweza kuchukua picha au video kwa ubora bila kucheza cheza yani unatoa kitu support portrait ya nguvu aiseee.

ebu tuambie unawaonaje Tecno na matoleo mapya ya Camon series kwa mwaka 2023 wanaweza kuwa washindani wa simu zingine?

View attachment 2654154

images%20(91)%20-%202023-06-11T183520.436.jpg


View attachment 2654158

View attachment 2654156

View attachment 2654157

View attachment 2654159
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom