Mkuu hujajua tu ! Jaribu kutumia high end phone utaona utofauti mkubwa , achana na camera achana na charge achana na processors , hivyo vyote achana navyo ila kuna vitu huwa havielezeki mfano uki scroll kwenye iphone na uka scroll kwenye tecno ni vitu viwili tofauti , yan ile response na smoothness ni tofauti kabisa . High end phones una click kwenye app mara moja , ila watu wa tecno kurudi nyuma naonaga wanabonyeza bonyeza ile back button mara kibao . Sasa tumia iphone one ni click moja tu na hamna issue za ku stack stack na kusubirishana. Fungua camera angalia inachukua mda gani ku focus kwenye subject ndo utajua nini maana ya ubora . Hata vitu mnavyoviita vya kawaida mfano wakati wa ku type ile speed ya response ni kitu muhimu sana na ni cha kila siku Ndo maana mtu akitumia high end kurudi chini lazima apate shida. Whatsap ya iphone siyo sawa na whatsap ya tecno na huu ndo ukweli ingawa zote zinatuma Picha na sms . Nimeona tecno wameweka animoji isee ni vituko !
Au simple zaidi labda endesha Swift na endesha Nissan Murano labda , kwenye swift unatumia nguvu nyingi, brake haziko on time yan ukitoka dar Moro uko hoi ila gari nzuri mzee huchoki.. huo ni mfano wa experience tunaoumaanisha
Swala la kusema tecno ni sub standard Kwa sababu haziko gsm arena tulikuwa sahihi 100% , sisi kaka watumiaji wa simu hatuwezi kumsikiliza tecno tu ndo atwambie ubora wa bidhaa zake , tunahitaji third party wa kudhibitisha huo ubora ili tumlinganishe na wengine tuone.
Pale unapokuta model ya simu dukani then ukaitafuta mtandaoni na usipate details za kutosha jua kwamba kuna tatizo ( kiufupi Mteja lazima ajue ananunua nini , ni muhimu sana) kama hujui unanunua nini unaanzia wapi ku negotiate? Yan una negotiate kitu ambacho hukijui? Mtu anakwambia camera Kali tu basi , serious? Unaona neno kamera kali linatosha kumwambia mteja anayejielewa?
GSM arena pale simu inapimwa na kulinganishwa kuangalia kama yaliyomo yamo.
Angalia hapo chini kwenye picha nimeweka 3D Touch ya iPhone ambavyo inaweza nisaidia natumia keyboard kama mouse pad , yan hiyo na move cursor popote Kwa kidole gumba in case nataka ku edit , space , highlight sehem yoyote wakati naandika n.k. Sasa vitu kama hivi kwenye tecno hamna lakini mkiambiwa mnakimbilia oooh hata sisi tunatuma whatsap , sijui fb tunaingia. Issue ni experience gani unaipata kwenye matumizi ya simu yako
View attachment 967011