kaka lengo la mediatek ni kutengeneza chip za bei rahisi ili watu wa hali ya chini nao waweze kunufaika ila inapofikia sasa simu za mediatek zinauzwa laki 4 au 5 au 6 na kuendelea inabidi tujiulize lengo limefikiwa? processor za mediatek ukiachana na weakness zake kama kutoweza ku update simu pia ni dhaifu sababu nyingi ni cortex a7 ambayo ina speed ndogo. pia kwenye gpu kwa ajili ya gaming na apps kubwa apps nyingi zimekua optimized kurun kwenye adreno hivyo compability yake na power vr ya meadiatek si nzuri.
usidanganyike na core ukaona simu ina core 8 au core 6 apps nyingi karibia asilimia 80 zimekuwa optimized kufanya kazi kwa core 1 au mbili, kwa lugha nyengine ukiwa na simu ya core nane ukirun app core 1 au mbili zitatumika na core 6 au 7 zitatulia hazifanyi kazi. core nyingi zinaleta sense zikiwa optimized kama alivyofanya samsung au chip mpya za huawei ziitwazo kirin, wao wameeka core nane lakini nne zina cortex a15 na nne zina cortex a7. hekima ya kufanya hivyo ukirun game au apps kubwa cortex a15 inahandle game kubwa then perfomance inakuwa kubwa lakini simu ikiwa inafanya task ndogo cortex a7 inahandle perfomance inakuwa ndogo na kusave battery. hivyo unapata perfomance kubwa na battery inayokaa sana.
so far chip nzuri za simu ni snapdragon 800/801 ambazo ndio best zinatumika simu zote kubwa kama htc m8, xperia z2, galaxy s5, lg g3 simu zinakuwa very smooth kabisa. hivyo hii chip ndio inakuwa recomended na pia ukitaka kujua hawa jamaa wapo level nyengine japo perfomance ni kubwa lakini battery pia inakaa sana simu kama lumia 1520, xperia t2, lg gflex ndo habari ya mjini ikija suala la kukaa na chaji japo kuna simu za mediatek zina 4000mah zinapitwa na qualcom yenye 3000mah.
nazilist hapa kwa perfomance hizi snapdragon
801
800
600
400
200
je tunapondea wachina?
kuna watu wao wanafkiri mtu akiongea hivi tunakandia wachina tu nitakupa case kidogo uelewe
1.case ya kwanza ni xiaomi
hawa jamaa ni wachina pale pale simu yao ya bei ghali ya mediatek ni dola around 130 inaitwa hongmi simu zao zote za kuanzia dola 200 hawatumii mediatek wanatumia either exynos au snapdragon so angalia jinsi wao wenyewe wachina wanavyojua
2.case ya pili ni oppo na oneplus one
hawa pia ni wachina na wametoa simu ya bei rahisi sana around dola 300 ila wametumia snapdragon 800/801
hapo juu just nimekuonesha even wachina wanaosifika kwa simu kali hawatumii mediatek.
watu wanacompare simu za mediatek na samsung na hili ni kosa kubwa sababu touchwiz ya samsung ni nzito sanaaa na haimaanishi ile ndio android, simu nyingi za mediatek zinatumia clone ya touchwiz so mtu akiwa na tecno akicheki na samsung ina touchwiz anaona ile ni android na kuona simu yake ipo fast. kwa comparison nzuri tafuta simu ya htc yenye sense au nexus yenye stock android au samsung yenye stock android then utaona kuwa snapdragon ni next level.
kuhusu price sasa hivi unaweza pata simu ya snapdragon 400 kuanzia dola 150 hivyo kwenye bei za kuanzia 250,000 unapata simu decent ya snapdragon mfano angalia zte redbull, moto g, lumia 630,
kwa hio snapdragon 800/801 ambayo ndio latest simu ya bei rahisi ni oneplus one ambayo ni around dola 300.