Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,060
- 43,477
Kama nimekuelewa tokea mwanzo unataka u-prove kwamba simu zote za Tecno zimewekewa tu Jina ila zinamilikiwa na watu tofauti na hilo Jina "TECNO" yaani tuseme ni trade name tu ila simu yenyewe iko.....
Kama ni hivo basi Onesha Phantom A+ Imefanana na simu gani nyingine?
yap nimemaanisha hivyo kaka kwanza nianze na introduction maana najua kuna criticism zitakuja. simu haijalishi imetengenezwa wapi bali tunatakiwa tujali imetengenezwa na nani. manufacture kama apple na samsung wanadesign simu halafu ndio zinapelekwa china kutengenezwa kwa wingi. ule uzuri unaouona kwenye iphone hautokani na foxcon bali ni apple wenyewe waliofanya design.
design ya simu ni kubwa sana na inacost mabilioni ya hela kutengeneza prototype kabla ya kwenda kiwandani kutengeneza kwa wingi. hawa tecno na karibia manufacture wote wa mediatek wao hawadesign simu wala hawana viwanda bali wanakwenda tu china kutoa order na kueka logo zao.
sasa hivi kuna pikipiki zinaitwa mkombozi kuna nyengine zinaitwa mtanganyika zipo mitaani munataka kusema na hawa jamaa wana kiwanda tanzania cha pikipiki? hawa ni kama tecno wanaenda tu kutoa order ya simu huko.
kaka njunwa umenipa challenge ya phantom nilishawah kuonesha simu kama phantom ila sio mbaya nitarudia tu hapa. hebu tuiangalie kwa makini phantom yetu kama sio mtanikosoa
phantom ni hiyo nyeupe na hapo kwenye design ya simu tunaona
1.camera 8mp
2.design yake kuna camera hump ya duara imetokezea kidogo
3.flash nayo ni ya duara ipo pembeni ya camera
4.spika ipo kwa chini
5.juu ya spika kuna description ya maneno toka kiwandani
tumeona nyuma ipoje tuje mbele sasa
1.angalia spika ye mbele hapo juu
2. kioo ukubwa wa inch 5
3. resolution ya 1280x720
njoo internal za ndani
1.ram 1gb
2.internal memory 4gb
3. hsdpa 2100 pekee
ukimaliza hapo njoo angalia simu hizi
angalia position ya camera angalia flash, angalia spika, angalia spika ya mbele zote zina 8mp tena imeandikwa kwa nyuma zote zina 4gb zote ram 1gb zote zina hsdpa 2100 karibia kila kitu kinafanana je ni coincidence?