Tecno mobile Mega Thread

Tecno mobile Mega Thread

vipi nokia tochi nayo ni low end au high end???

Yategemea na mahitaji yako. Waweza iweka kwenye kundi moja wapo kati ya hayo mawili.
> Je haikidhi mahitaji yako ya kupiga na kupokea?
> Je haikidhi mahitaji yako ya kutuma na kupokea sms?
Je jibu ni ndio au hapana?
 
Huwaga n ngumu kwa sababu huwez jua codes za kuandika kwa kuwa ukikosea unaweza ukabrick simu yko

Solution hapo ni kuacha au kuna namna nyingine naweza kufanya.maana sijakupata vizuri sana sana post iliyotangulia hapo juu
 
Okay mmesema mengi sana kuhusu matumizi basics sijui ya techno or whatever sasa orodhesheni basi hayo matumizi yasiyo basic ya hizo simu zingine...via situmii techno...tuone matumizi yasiyo ya kawaida i.e samsung galaxy or whatever....!!

Ndugu umewaza km mimi Asante ngoja tusubiri majibu....!!
 
Mkuu Baba Mkali umeongea kitu ya Maana sana! Watanganyika wengi Tunafanya mambo kwa kutaka Tuonekane2 Kiukweli hawa jamaa Wachina wanajua mahitaji ya Umaskini huu wa kiFRICA ulio7bishwa na Watawala wetu..! so pamoja kufukalishwa lkn hawa jamaa bado wanataka nawasio nauwezo wasiachwe kwenye Ulimwengu wakisasa..! Mimi nadhani kila mtu anunue kitu kutokana na Uwezo na mahitaji yake,,!! lkn kumwambia mtu adundulize hadi afikie uwezo wakununu s5 wakati Mchani yupo cdhani..!
 
Last edited by a moderator:
Hivi karibuni zimeanzishwa thread nyingi hapa JF za watu wakisifia na wengine kukandia simu za TECNO. Lakini hebu tujiulize, ni kwanini watu wengi wanaangukia kwenye simu hizi ambazo zinaonekana kama ni za ubora wa hali ya chini huku wengine wakizisifia kwamba zina ubora wa hali ya juu?

Kwa maoni yangu mi naona hapa kuna mawili:
1. Watu wengi wanaozisifia simu kama tecno, ni watu ambao wana matumizi madogo sana ya simu.. yaani kupiga, kutuma msg, na ku browse internet na mitandao ya kijamii. Mtu akishaona simu aliyo nayo inaweza kufanya mambo hayo pamoja na labda ku play mziki na kupiga picha (regardless ya quality), ana conclude kwamba hiyo ni simu nzuri sana na haina tatizo lolote. Kitu ambacho kwa level yake ni kweli.. Ikumbukwe kwamba hayo niliyotaja ni mambo basic sana ambayo low- end smartphone yoyote hata ya kichina inaweza kufanya! Kwahiyo mi siwalaumu hawa watu. Huo ndio ukweli wa upeo wao kwenye simu. Mtu wa aina hii hahitaji Galaxy Note 3. Tecno inamtosha kabisa na wala huwezi kumlaumu akiisifia..

2. Kwa upande mwingine nawalaumu sana wauzaji wa simu. Siku hizi ukitembelea maduka mengi ya simu huwezi kukuta low-end smartphones za Samsung, HTC, Motorola n.k.. Simu zote utakazokuta zenye majina makubwa ni zile za bei ghali tuu.. Lakini ukweli ni kwamba kuna simu nzuri tu za samsung, nokia, HTC, Sony n.k ambazo ni za bei ya chini karibu sawa tu na hizo tecno, ila zina ubora wa hali ya juu! Tatizo simu hizi hazipo madukani hivyo kuwalazimu watu kuchagua kati ya tecno au Galaxy s5. Kwa uchumi wetu, haishangazi kuona wengi wakiangukia kwenye tecno. Hebu chukulia mfano wa simu hizi mbili:
TECNO F7 PHANTOM A: Internal Memory 4Gb, RAM 1Gb, Processor 1Ghz, Display 5inch (293ppi) Bei ~ 450,000/=
SAMSUNG GALAXY NOTE 1: Internal memory 16Gb, RAM 1Gb, Processor 1.4Ghz, Display 5.3inch (285ppi) Bei ~ 450,000/=
Tecno-F7-Phantom-A-Plus-214x300.jpg
tmobile-samsung-galaxy-note.jpg

Tatizo sasa.. Ukitembelea madukani utazikuta TECNO phantom zimejaa tele lakini Note 1 unaweza kumaliza maduka yote bila kuipata..! Nina uhakika ukimuwekea mtu simu hizo mbili side by side ukamuambia achague, matokeo yanaweza kuwa tofauti sana na hali ilivyo sasa.
Watanzania wanazidi kuwa na akili. kwa nini mtu anunue simu ya bei mbaya kwa kufuata jina wakati ipo kama hiyo yenye kukidhi mahitaji yake kwa bei nafuu. Upende usipende Tecno ni simu bora na shindani vilivyo.
 
Hizi S5 zina matatizo mimi ya kwangu nikiizima ninapoiwasha inaload contact hata lisaa lizima na screen ikisleep ukitaka kuitumia screen inabaki nyeusi mpk utoe betri niiwashe tena ndo ifanye kazi vinginevyo fuction zingine iko poa
 
team tecno..nasema izo za iphone samsung na za bei kubwa zina kipi cha tofauti..mfano kwenye net..store...WABONGO WANAPENDA SHOW OFF ZA KIJINGA JINGA....IM STILL LOVE MY TECNO H5
 
Tehno ni bei nafuu na pia imeniwezesha kukidhi mahitaji yangu ivyo sidhani kama nitatoka huku.
 
Hivi karibuni zimeanzishwa thread nyingi hapa JF za watu wakisifia na wengine kukandia simu za TECNO. Lakini hebu tujiulize, ni kwanini watu wengi wanaangukia kwenye simu hizi ambazo zinaonekana kama ni za ubora wa hali ya chini huku wengine wakizisifia kwamba zina ubora wa hali ya juu?

Kwa maoni yangu mi naona hapa kuna mawili:
1. Watu wengi wanaozisifia simu kama tecno, ni watu ambao wana matumizi madogo sana ya simu.. yaani kupiga, kutuma msg, na ku browse internet na mitandao ya kijamii. Mtu akishaona simu aliyo nayo inaweza kufanya mambo hayo pamoja na labda ku play mziki na kupiga picha (regardless ya quality), ana conclude kwamba hiyo ni simu nzuri sana na haina tatizo lolote. Kitu ambacho kwa level yake ni kweli.. Ikumbukwe kwamba hayo niliyotaja ni mambo basic sana ambayo low- end smartphone yoyote hata ya kichina inaweza kufanya! Kwahiyo mi siwalaumu hawa watu. Huo ndio ukweli wa upeo wao kwenye simu. Mtu wa aina hii hahitaji Galaxy Note 3. Tecno inamtosha kabisa na wala huwezi kumlaumu akiisifia..

2. Kwa upande mwingine nawalaumu sana wauzaji wa simu. Siku hizi ukitembelea maduka mengi ya simu huwezi kukuta low-end smartphones za Samsung, HTC, Motorola n.k.. Simu zote utakazokuta zenye majina makubwa ni zile za bei ghali tuu.. Lakini ukweli ni kwamba kuna simu nzuri tu za samsung, nokia, HTC, Sony n.k ambazo ni za bei ya chini karibu sawa tu na hizo tecno, ila zina ubora wa hali ya juu! Tatizo simu hizi hazipo madukani hivyo kuwalazimu watu kuchagua kati ya tecno au Galaxy s5. Kwa uchumi wetu, haishangazi kuona wengi wakiangukia kwenye tecno. Hebu chukulia mfano wa simu hizi mbili:
TECNO F7 PHANTOM A: Internal Memory 4Gb, RAM 1Gb, Processor 1Ghz, Display 5inch (293ppi) Bei ~ 450,000/=
SAMSUNG GALAXY NOTE 1: Internal memory 16Gb, RAM 1Gb, Processor 1.4Ghz, Display 5.3inch (285ppi) Bei ~ 450,000/=
Tecno-F7-Phantom-A-Plus-214x300.jpg
tmobile-samsung-galaxy-note.jpg

Tatizo sasa.. Ukitembelea madukani utazikuta TECNO phantom zimejaa tele lakini Note 1 unaweza kumaliza maduka yote bila kuipata..! Nina uhakika ukimuwekea mtu simu hizo mbili side by side ukamuambia achague, matokeo yanaweza kuwa tofauti sana na hali ilivyo sasa.

Weye ndugu ulichoona ni simu tu. Mbona huongelei magari? kwa nini watz hawanunui mabenzi wamekazana na vimeo vya kijapani? kwa nini huzungumzii ujenzi wa nyumba, mbona watz wote hawajengi masaki?

Mbona watz wote hawavai nguo special na ready made ila wanavaa mitumba?

Mbona watz wote hawaendi kutibiwa india?
 
Note 3 note 3, zina nini phantom haina. Acha hizi bana
 
NA vp namna ya kutoa logo ya tecno na sauti pindi unapowasha simu?

Naju unaweza kutoa sauti unapowasha na kuzima, kutoa logo bado sijajua.
kuhusu sauti unapotaka kuzima bonyeza POWER button. Utaona option nyingi tu kwa sauti bofya spika X ,itazima kimya na kuwaka kimya.ukiwasha ukitaka sauti unabofya tena power button then unabofya loud kwenye symbol ya spika.
 
kaka note 1 ilitoka 2011 sawa na s2 sasa hv unlocked kkoo hadi laki 3 unazipata. Ukiona mtu anauza laki 6 ujue ana stock ya zamani anataka akulalie. Even s3 ambayo ni bora kwa note 1 haiuzw laki 6 siku hizi

Samahani kidogo mkuu unaposema "unlocked" unamaanisha nini?
 
Weye ndugu ulichoona ni simu tu. Mbona huongelei magari? kwa nini watz hawanunui mabenzi wamekazana na vimeo vya kijapani? kwa nini huzungumzii ujenzi wa nyumba, mbona watz wote hawajengi masaki?

Mbona watz wote hawavai nguo special na ready made ila wanavaa mitumba?

Mbona watz wote hawaendi kutibiwa india?

aliyeturoga watanzania kafa na kapotea bora hata angezikwa yaani magari kutoka japan ndio wanayotumia halafu kukejeli watumiaji wa tecno huu ni ulimbukeni
mtu mahitaji yake yamekamilika kwa kutumia tecno we unamdharau kama hapa tanzania wengi wao ni kupiga kupokea sms na kubrowse basi haya nimiliki simu ya milioni kwa ajili ya vitu nitakavyovipata kwa simu ya laki na nusu ? kwa hali ya kawaida ya maisha ya tz ni ujinga tecno leteni mpaka soko walikimbie au washushe bei

#teamTecno
 
Samahani kidogo mkuu unaposema "unlocked" unamaanisha nini?

Unlocked = Simu ambayo waweza tumia kwa mtandao wowote ule, iwe ni tigo, voda , airtel et sa
Na kwa kawaida unlocked bei yake huwa ni ya juu kidigo ukilinganisha na Simu ambayo ipo LOCKED kwa mtandao fulani.
MFANO : Ascend y300 ambayo ipo LOCKED kwa mtandao tiGo ilikuwa ikuuzwa tsh 195'000 na simu hiyo hiyo ambayo ni UNLOCKED ilikuwa ikiuzwa kati ya 230'000 hadi 260'000 kutegemeana umeikuta wapi.
 
Back
Top Bottom