TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 6,551
- 20,259
Hivi karibuni zimeanzishwa thread nyingi hapa JF za watu wakisifia na wengine kukandia simu za TECNO. Lakini hebu tujiulize, ni kwanini watu wengi wanaangukia kwenye simu hizi ambazo zinaonekana kama ni za ubora wa hali ya chini huku wengine wakizisifia kwamba zina ubora wa hali ya juu?
Kwa maoni yangu mi naona hapa kuna mawili:
1. Watu wengi wanaozisifia simu kama tecno, ni watu ambao wana matumizi madogo sana ya simu.. yaani kupiga, kutuma msg, na ku browse internet na mitandao ya kijamii. Mtu akishaona simu aliyo nayo inaweza kufanya mambo hayo pamoja na labda ku play mziki na kupiga picha (regardless ya quality), ana conclude kwamba hiyo ni simu nzuri sana na haina tatizo lolote. Kitu ambacho kwa level yake ni kweli.. Ikumbukwe kwamba hayo niliyotaja ni mambo basic sana ambayo low- end smartphone yoyote hata ya kichina inaweza kufanya! Kwahiyo mi siwalaumu hawa watu. Huo ndio ukweli wa upeo wao kwenye simu. Mtu wa aina hii hahitaji Galaxy Note 3. Tecno inamtosha kabisa na wala huwezi kumlaumu akiisifia..
2. Kwa upande mwingine nawalaumu sana wauzaji wa simu. Siku hizi ukitembelea maduka mengi ya simu huwezi kukuta low-end smartphones za Samsung, HTC, Motorola n.k.. Simu zote utakazokuta zenye majina makubwa ni zile za bei ghali tuu.. Lakini ukweli ni kwamba kuna simu nzuri tu za samsung, nokia, HTC, Sony n.k ambazo ni za bei ya chini karibu sawa tu na hizo tecno, ila zina ubora wa hali ya juu! Tatizo simu hizi hazipo madukani hivyo kuwalazimu watu kuchagua kati ya tecno au Galaxy s5. Kwa uchumi wetu, haishangazi kuona wengi wakiangukia kwenye tecno. Hebu chukulia mfano wa simu hizi mbili:
TECNO F7 PHANTOM A: Internal Memory 4Gb, RAM 1Gb, Processor 1Ghz, Display 5inch (293ppi) Bei ~ 450,000/=
SAMSUNG GALAXY NOTE 1: Internal memory 16Gb, RAM 1Gb, Processor 1.4Ghz, Display 5.3inch (285ppi) Bei ~ 450,000/=
Tatizo sasa.. Ukitembelea madukani utazikuta TECNO phantom zimejaa tele lakini Note 1 unaweza kumaliza maduka yote bila kuipata..! Nina uhakika ukimuwekea mtu simu hizo mbili side by side ukamuambia achague, matokeo yanaweza kuwa tofauti sana na hali ilivyo sasa.