Tecno mobile Mega Thread

Tecno mobile Mega Thread

hio hadhi ya juu ni yakwako wewe ...sema ivii wanazinunua sababu ni bei rahisi....no one to beat samsung mkuu najua kuna watu watakataa.
 
ubishe usibishe nawambia hakuna smartphone nzuri kwa tz kama tecno .na nis simu ambayo iko juu kwa tz na inapendeka, kama unasema haiko juu wew ni punguwani

najua sababu na wewe unatumia tecno ndio maana tumia simu zingine uone mkuu manake hata mwenye nokia ya tochi huiona ni bora sababu ndio hio tu alionayo.
 
Huwezi kusema na tukakuelewa eti TECNO ni simu yenye hadhi hata GSMARENA haipo, mjomba shiny c kubali tu umepotosha jamii kwa kusema tecno ina hadhi.
 
Last edited by a moderator:
Wataalam mnisaidie, simu yangu Tecno S5 imekuwa 'bricked' ,inashindwa kuwaka, kama kuna mtu yeyote anafahamu link ninayoweza kupata stock rom yake (tecno s5) anisaidie.
 
B2L Mkuu,nimejaribu silent na vibration bado ina fanyaa dzzz pale simu inapoanza kuhesabu sekunde na mwisho wa maongezi ambayo pia inasikika kwa mtu aliyepokea simu.

Huo mlio ni baada ya simu 2 kupokelewa na baada ya kukata hauwezi toka lbd uediti system build prop ambyo ndo inafanya simu inavibrate ( inatoa huo mlio ) baada y kupokea simu
 
Wataalam mnisaidie, simu yangu Tecno S5 imekuwa 'bricked' ,inashindwa kuwaka, kama kuna mtu yeyote anafahamu link ninayoweza kupata stock rom yake (tecno s5) anisaidie.

Ni ngumu kupata kwny net ila km unaweza tafta mtu yyte mwnye simu km hyo ufanye backup ndo iuflash hyo rom au unaweza ifanya ikawaka kwanza kwa kuflash rom yyte y simu ambyo chipset yke n km hyo ambyo n mtk6572. Km vile tecno m3 ili iwake ukiendelea kutafta stock rom yke kwa kuwa haiwaki itabidi uiflash n sp flash tools ndo itawaka
 
Wataalam mnisaidie, simu yangu Tecno S5 imekuwa 'bricked' ,inashindwa kuwaka, kama kuna mtu yeyote anafahamu link ninayoweza kupata stock rom yake (tecno s5) anisaidie.

inakubali kuingia into recovery mode
 
Ni ngumu kupata kwny net ila km unaweza tafta mtu yyte mwnye simu km hyo ufanye backup ndo iuflash hyo rom au unaweza ifanya ikawaka kwanza kwa kuflash rom yyte y simu ambyo chipset yke n km hyo ambyo n mtk6572. Km vile tecno m3 ili iwake ukiendelea kutafta stock rom yke kwa kuwa haiwaki itabidi uiflash n sp flash tools ndo itawaka

Mkuu hata mimi Tecno P5 yangu imezimika ghafla.Naweza kufuata process hii?
 
kila kitu kina hadhi kulingana na mazingira yake kibongobongo tecno ina hadhi mana ni bei rahisi na ina mapungufu machache sana ukilinganisha na hizo simu za milion ambapo mwisho wa siku ratio ni tofauti sana

kitu chenye hadhi ya juu kitauzwaje bei rahisi!!zinduka wewe
 
Mi naona hapa kuna mawili:
1. Watu wengi wanaozisifia simu kama tecno, ni watu ambao wana matumizi madogo sana ya simu.. yaani kupiga, kutuma msg, na ku browse internet na mitandao ya kijamii. Mtu akishaona simu aliyo nayo inaweza kufanya mambo hayo pamoja na labda ku play mziki na kupiga picha (regardless ya quality), ana conclude kwamba hiyo ni simu nzuri sana na haina tatizo lolote. Kitu ambacho kwa level yake ni kweli.. Ikumbukwe kwamba hayo niliyotaja ni mambo basic sana ambayo low- end smartphone yoyote hata ya kichina inaweza kufanya! Kwahiyo mi siwalaumu hawa watu. Huo ndio ukweli wa upeo wao kwenye simu. Mtu wa aina hii hahitaji Galaxy Note 3. Tecno inamfaa kabisa..

2. Kwa upande mwingine nawalaumu sana wauzaji wa simu. Siku hizi ukitembelea maduka mengi ya simu huwezi kukuta low-end smartphones za samsung, htc, motorola n.k.. Simu zote utakazokuta zenye majina makubwa ni zile za bei ghali tuu.. Lakini ukweli ni kwamba kuna simu nzuri tu za samsung, nokia, HTC, Sony n.k ambazo ni za bei ya chini karibu sawa tu na hizo tecno, ila zina ubora wa hali ya juu! Simu hizi hazipo madukani hivyo kuwalazimu watu kuchagua kati ya tecno au Galaxy s5. Kwa uchumi wetu, haishangazi kuona wengi wakiangukia kwenye tecno.
 
Ni kweli Tecno zinauzwa sana ila bado simu hizi zina matatizo makubwa ya reliability. Si jambo la ajabu kununua smart phone ya Tecno na ikaanza kukusumbua siku hiyohiyo pamoja na kuwa na garantii ya miezi 13. Hata hivyo, kadri siku zinavyosogea Mchina anarekebisha mambo.
 
Back
Top Bottom