mtu anasema simu haina fast charging kama simu ina charge yake nzuri na inajaa haraka hiyo Fast charging ni mbwe mbwe tu
IP rating yanini wewe? simu ikitumbukia kwenye maji meisha yeah acha iishe kwani ulinunua simu ili uingie nayo bafuni au kwenda kuogelea nayo swimming pool?
yani ukiangalia wanaoponda tecno ni wapenda show off ila hawana sababu yoyote yakusababisha umsikilize eti sio simu,Mtu aikosoe phantom 8 au phantom 9 basi nimuone?
Mzee TEKINO NI TAKATAKA labda nikiandika kwa herufi kubwa nitaeleweka. Naona unajaribu kuipamba wakati hamna lolote....
Hiyo phantom 8 imetoka mwaka jana mwezi wa 4 ila hata tukiilinganisha na samsung iliyotoka jan 2017 bado hiyo phantom 8 itaonekana takataka.
Mfano mdogo tu... Ni Samsung galaxy a5 2017 vs Phantom 8
1. A5 2017 imetoka mwaka 2017 ikiwa na mashmallow(6.03) lakini imeweza kuwe upgradable mpaka Oreo(8.0) wakati Phantom 8 imetoka 2018 with Nougat(7.0) na hapo ndio mwisho wake.
2. A5 shop inauzwa 700k wakati phantom 8 inauzwa 800k
3. A5 ina IP68 wakati phantom 8 haina chochote. Yaani hata ukidondosha simu kwenye maji kwa bahati mbaya ndio biashara ishakukata.
4. A5 ina 18W fast charging system wakati Phantom 8 haina fast charging kabisa. Yaani wakati mwenzako anacharge simu yake around one hour inakuwa imejaa wewe unacharge masaa matatu. Halafu eti unasema fast charging ni mbwembwe, hiki ni kituko cha karne.
5. A5 2017 ina Superamoled display wakati phatom 8 ina LCD. Haani unanunua simu gharama halafu ina Low quality. Nakuapia ukitumia simu yenye Superamoled hata mara moja tu. Hutotamani kurudi kwenye hizo takataka za LCD.
Hivyoni vichache tu. Na hapo ni melinganisha hiyo phantom na a5 2017 ambayo ni midrange tu. Kama ningelinganisha na High end basi ingekuwa ni kichefuchefu aiseee.